Kuandika Darasa la II Syllabus

    1. Kunakili hadithi fupi na kuweka alama nne za uandishi
      1. Hadithi zinanakiliwa na kuwekwa alama za uandishi kwa usahihi
    2. Kuandika aya kuhusu taarifa fulani kwa mtiririko wa matukio kwa kuzingatia alama za uandishi
      1. Uandishi wa aya kuhusu taarifa fulani kwa kuzingatia alama za uandishi unafanyika kwa usahihi.
    3. Kuandika sentensi fupi kwa kuzingatia matumizi ya alama ya mkato (,), nukta (.), kuuliza (?) na mshangao (!) kwa usahihi.
      1. Uandikaji wa sentensi na habari fupi zinazoonesha matumizi ya alama nne za uandishi ( . , ? !) unafanyika kwa usahihi.
    1. Kuandika sentensi zenye maneno yanayojumuishaherufi mwambatano (sh, ny, ng, nd, th, mb, kw) kwa kunakili na kwa imla.
      1. Uandikaji wa sentensi zenye maneno yanayojumuisha herufi mwambatano (sh, ny, ng, nd, th, mb, kw) kwa kunakili na kwa imla unafanyika kwa usahihi.
    2. Kuandika kifungu linganifu cha habari kwa kunakili na imla.
      1. Uandikaji wa kifungu linganifu cha habari kwa kunakili na imla unafanyika kwa usahihi.
    3. Kutumia alama nne za uandishi katika kuandika sentensi. (Nukta, mkato, alama ya kuuliza na ya mshangao).
      1. Utumiaji wa alama za uandishi (nukta, mkato, alama ya kuuliza na alama ya mshangao) katika kuandika sentensi unafanyika kwa usahihi.
    4. Kuandika herufi kubwa na maneno yenye herufi kubwa za irabu (A, E, I, O, U) na konsonanti za kundi la kwanza. ( B, M, K, D, N) na makundi mengine.
      1. Uandikaji wa herufi kubwa na maneno yenye kubwa za irabu (a, e, i, o, u) na konsonanti za kundi la kwanza. ( b, m, k, d, na makundi mengine unafanyika kwa usahihi.
    5. Kuandika konsoanti na maneno yenye konsonanti hiyo katika daftari la mwandiko (Daftari lenye mistari mikubwa na midogo).
      1. Uandikaji wa konsonanti kumi na tisa na maneno yake katika daftari la mwandiko unafanyika kwa usahihi.
    6. Kuchora michoro ya konsonanti na kuandika konsonanti (b, m, k, d, n); (l,t,p,ch,s,f,j); (g,y, z, h, r, w, v ch,).
      1. Uchoraji wa michoro ya konsonanti na kuandika konsonanti unafanyika kwa usahihi.
    7. Kuandika maneno yanayoundwa na herufi za irabu
      1. Uandikaji wa maneno yanayoundwa na herufi za irabu unafanyika kwa usahihi.
    8. Kuchora michoro ya irabu na kuumba herufi za irabu.
      1. Uchoraji wa michoro ya irabu na uumbaji wa herufi za irabu unafanyika kwa usahihi.
    1. Kutumia kadi au chati ya maneno kuunda sentensi zenye maneno yanayozidi sita
      1. Uundaji wa sentensi zenye maneno zaidi ya sita kwa kutumia kadi au chati ya maneno uafanyika kwa usahihi.
    2. Kutumia chati ya sakaneno kuunda maneno yenye silabi zaidi ya nne
      1. Uundaji wa maneno yenye silabi zaidi ya nne kwa kutumia chati ya sakaneno unafanyika kwa usahihi.
    3. Kutumia picha za vitu na kuandika maneno
      1. Uandikaji wa maneno kwa kutumia picha za vitu unafanyika kwa usahihi.
    4. Kuandika majina ya kwanza ya wanafunzi katika darasa
      1. Uandikaji wa majina ya kwanza ya wanafunzi wa darasa unafanyika kwa usahihi.
    5. Kuunda maneno yenye maana yanayotokana na silabi za kundi la pili la konsonanti (l, t, p, s, f, j) na la tatu (g, y, z, h, r, w, v, ch) na irabu
      1. Uundaji wa maneno yenye maana yanayotokana na silabi za kundi la pili la konsonanti na la tatu na irabu unafanyika kwa usahihi.
    6. Kuunda maneno yenye maana yanayotokana na kundi la kwanza la konsonanti (b, m, k, d, n) na irabu
      1. Uundaji wa maneno kwa kutumia silabi zilizojengwa na konsonanti sita za kundi la kwanza la irabu unafanyika kwa usahihi.
    7. Kuunda silabi mwambatano zenye konsonanti tatu na irabu moja
      1. Uundaji wa silabi mwambatano zenye konsonanti tatu na irabu moja unafanyika kwa usahihi.
    8. Kuunda silabi kwa kutumia konsonanti mbili na irabu moja
      1. Uundaji wa silabi kwa kutumia konsonanti mbili na irabu moja unafanyika kwa usahihi.
    1. Kuandika maneno kwa mwandiko wa kuunga
      1. Uandikaji wa maneno kwa mwandiko wa kuunga unafanyika kwa usahihi.
    2. Kutumia kalamu kuumba herufi za kuunga ili kukuza mwandiko
      1. Uandikaji wa herufi za mwanzo za majina ya picha teule za wanyama, matunda na vifaa vya ndani kwa mwandiko wa kuunga unafanyika kwa usahihi.
    3. Kuandika herufi za mwanzo za majina ya picha teule za matunda, wanyama, na vifaa vya ndani kwa mwandiko wa kuunga
      1. Uandikaji wa herufi za mwanzo za majina ya picha teule za matunda, wanyama, na vifaa vya ndani kwa mwandiko wa kuunga kwa usahihi.
    1. Kuchora kwa kutumia penseli na daftari na kupaka rangi ili kujenga stadi za kutumia penseli na daftari.
      1. Uchoraji kwa kutumia penseli na daftari na kupaka rangi ili kujenga stadi za kutumia penseli na daftari unafanyika kwa usahihi.
    2. Kuchora kwa kunakili, kufuatisha na kubuni michoro kwa kutumia chaki na kibao ili kupata maumbo mazuri zaidi na stadi za kutumia vifaa
      1. Uchoraji kwa kunakili, kufuatisha na kubuni michoro kwa kutumia chaki na vibao unafanyika kwa usahihi.
    3. Kuchora michoro mbalimbali mchangani kwa vidole na vijiti ili kupata dhana ya herufi inayotakiwa kuandika na stadi za uumbaji wa maumbo.
      1. Uchoraji wa michoro mbalimbali mchangani kwa vidole na vijiti ili kupata dhana ya herufi inayotakiwa kuandikwa na stadi za uumbaji wa maumbo unafanyika kwa usahihi.