Kusoma Darasa la II Syllabus

    1. Kusoma kifungu cha habari kwa muundo stahili na hisia ili kujenga ufasaha wa kusoma.
      1. Usomaji wa kifungu cha habari kwa mwendo stahili na hisia ili kujenga ufasaha unafanyika kwa usahihi.
    2. Kusoma hadithi rahisi ili kuendeleza ufasaha katika kusoma
      1. Usomaji wa hadithi rahisi ili kuendeleza ufasaha unafanyika kwa usahihi.
    3. Kusoma hadithi fupi kwa kuzingatia alama za uandishi [mkato (,) , nukta (.), alama ya kuuliza (?) na mshangao (!)] kujenga ufasaha wa kusoma.
      1. Usomaji wa hadithi fupi kwa kuzingatia alama za uandishi unafanyika kwa usahihi.
    4. Kusoma kwa kutembeza macho haraka katika mistari iliyounda kifungu cha habari ili kujenga ufasaha wa kusoma
      1. Usomaji wa kutembeza macho haraka katika mistari iliyounda kifungu cha habari ili kujenga ufasaha wa kusoma
    5. Kusoma kwa ufasaha herufi, silabi, maneno, sentensi kwa kutumia chati na vifungu vya habari
      1. Usomaji wa herufi, silabi, maneno na sentensi kwa kutumia chati mbalimbali na vifungu vya habari unafanyika kwa ufasaha.
    1. Kutenganisha maneno yanayoundwa na herufi mwambatano na maneno sahili katika sentensi.
      1. Utenganisha wa maneno yanayoundwa na herufi mwambatano na maneno sahili katika sentensi unafanyika kwa usahihi.
    2. Kuunganisha maneno yenye kuundwa na herufi mwambatano na maneno sahili ili kuunda sentensi.
      1. Uunganishaji wa maneno yenye kuundwa na herufi mwambatano na maneno sahili ili kuunda sentensi unafanyika kwa usahihi.
    3. Kutenganisha silabi za herufi mwambatano na silabi sahili katika maneno yaliyoundwa na silabi tatu.
      1. Utenganishaji wa silabi za herufi mwambatano na silabi sahili katika maneno yaliyoundwa na silabi tatu unafanyika kwa usahihi.
    4. Kuunganisha silabi za herufi mwambatano na silabi sahili katika kuunda maneno yenye silabi tatu.
      1. Uunganishaji wa silabi za herufi mwambatano na silabi sahili katika kuunda maneno yenye silabi tatu unafanyika kwa usahihi.
    5. Kutenganisha sauti za herufi mwambatano na irabu zinazounda silabi.
      1. Utenganishaj i wa sauti za herufi mwambatano na irabu zinazounda silabi zinafanyika kwa usahihi.
    6. Kuungaisha sauti za herufi mwambatao na irabu katika kuunda silabi.
      1. Uuganishaji wa sauti za herufi mwambatao na irabu katika kuunda silabi kwa usahihi
    7. Kuhusianisha sauti na herufi mwambatano (dhDH, thTH, ng'NG', mbwMBW, ngwNGW, chwCHW, ndwNDW) kwa kutumia kadi za herufi mwambatano.
      1. Uhusianishaji wa sauti na herufi mwambatano ( dhDH, thTH, ng'NG', mbwMBW, ngwNGW, chwCHW, ndwNDW) kwa kutumia kadi za herufi mwambatano unafanyika kwa usahihi.
    8. Kutengaisha maneno yanaounda sentensi.
      1. Utenganishaji wa maneno na kutamka maneno yanayounda sentensi unafanyika kwa usahihi.
    9. Kuunganisha maneno iii kuunda sentensi.
      1. Utenganishaji na utamshaji wa silabi zinazounda maneno yenye silabi tatu unafanyika kwa usahihi.
    10. Kutenganisha na kutamka silabi zinazounda maneno yenye silabi tatu.
      1. Utenganishaji na utamkaji wa silabi zinazounda maneno yenye silabi tatu unafanyika kwa usahihi.
    11. Kuhusianisha sauti na konsonanti (bB, mM, kK, dD, nN); (IL, tT, pP, sS, tF,jJ); (gG, yY, zZ, hH, rR, wW, vVchCH) kwa kutumia kadi za herufi.
      1. Uhusianishaji wa sauti na konsonanti unafanyika kwa usahihi kwa kutumia kadi za herufi.
    12. Kutenganisha sauti za irabu zinazounda maneno yenye silabi mbili.
      1. Sauti za irabu zinazounda maneno yenye silabi mbili zinatenganishwa kwa usahihi.
    13. Kuunganisha silabi mbili zinazoundwa na sauti za irabu ( a, e, i, o, u) na kuunda maneno yenye maana.
      1. Silabi mbili zinazoundwa na sauti za irabu zinaunganishwa na kuunda maneno yenye maana sahihi.
    1. Kubaini sauti za mwanzo za maneno.
      1. Ubainishaji wa sauti za mwanzo za maneno unafanyika kwa usahihi.
    2. Kubaini silabi katika maneno yaliyoundwa na silabi mbili.
      1. Ubainishaji wa silabi zilizounda maneno yenye silabi mbili unafanyika kwa usahihi.
    3. Kubaini maneno yanayounda sentensi kwa kupiga makofi.
      1. Ubainishaji wa maneno yanayounda sentensi tofauti kwa kupiga makofi unafanyika kwa usahihi.
    4. Kubaini sauti zitolewazo na viungo vya mwili na vifaa vingine vinavyotoa sauti.
      1. Sauti zitolewazo na viungo vya mwili na vitu vingine vinavyotoa sauti zinabainishwa kwa usahihi.
    5. Kubaini sauti za wanyama na ndege.
      1. Sauti za wanyama na ndege zinabainishwa kwa usahihi.
    1. Kuunganisha sauti zinazounda maneno yenye silabi tatu kutokana na maneno yaliyotamkwa kwa kutenganishwa
      1. Uunganishaji wa sauti zinazounda maneno yenye silabi tatu kutokana na maneno yaliyotamkwa kwa kutenganishwa.
    2. Kubainisha kwa kutaja sauti za mwanzo na sauti za mwisho katika maneno yenye silabi tatu.
      1. Kubainisha kwa kutaja sauti za mwanzo na sauti za mwisho katika maneno yenye silabi tatu unafanyika kwa usahihi.
    3. Kubaini kwa kutamka sauti zilizounda maneno teule.
      1. Ubainishaji kwa kutamka sauti zilizounda maneno teule unafanyika kwa usahihi.