Kuandika

Uundaji wa maneno
♿ Accessibility: | | | |

Uundaji wa maneno

Kutumia kadi au chati ya maneno kuunda sentensi zenye maneno yanayozidi sita
Uundaji wa sentensi zenye maneno zaidi ya sita kwa kutumia kadi au chati ya maneno uafanyika kwa usahihi.
Kutumia chati ya sakaneno kuunda maneno yenye silabi zaidi ya nne
Uundaji wa maneno yenye silabi zaidi ya nne kwa kutumia chati ya sakaneno unafanyika kwa usahihi.
Kutumia picha za vitu na kuandika maneno
Uandikaji wa maneno kwa kutumia picha za vitu unafanyika kwa usahihi.
Kuandika majina ya kwanza ya wanafunzi katika darasa
Uandikaji wa majina ya kwanza ya wanafunzi wa darasa unafanyika kwa usahihi.
Kuunda maneno yenye maana yanayotokana na silabi za kundi la pili la konsonanti (l, t, p, s, f, j) na la tatu (g, y, z, h, r, w, v, ch) na irabu
Uundaji wa maneno yenye maana yanayotokana na silabi za kundi la pili la konsonanti na la tatu na irabu unafanyika kwa usahihi.
Kuunda maneno yenye maana yanayotokana na kundi la kwanza la konsonanti (b, m, k, d, n) na irabu
Uundaji wa maneno kwa kutumia silabi zilizojengwa na konsonanti sita za kundi la kwanza la irabu unafanyika kwa usahihi.
Kuunda silabi mwambatano zenye konsonanti tatu na irabu moja
Uundaji wa silabi mwambatano zenye konsonanti tatu na irabu moja unafanyika kwa usahihi.
Kuunda silabi kwa kutumia konsonanti mbili na irabu moja
Uundaji wa silabi kwa kutumia konsonanti mbili na irabu moja unafanyika kwa usahihi.
Listening to this topic