Kusoma Darasa la I Syllabus

    1. Kujenga maana ya hadithi kwa kuuliza na kujibu maswali.
      1. Ujenzi wa maana ya hadithi kwa kuuliza na kujibu maswali unafanyika kwa usahihi.
    2. Kujenga taswira ya muda wa tukio na mahali pa tukio katika habari teule.
      1. Ujenzi wa taswira ya muda wa tukio na mahali pa tukio unafanyika kwa usahihi.
    3. Kutabiri maudhui ya habari kwa kutumia picha, jina la kitabu, hadithi na mwendelezo wa hadithi.
      1. Utabiri wa maudhui ya habari unafanyika kwa usahihi kwa kutumia picha jina la kitabu, hadithi na mwendelezo wa hadithi.
    4. Kusoma kifungu linganifu cha habari kwa ufahamu.
      1. Usomaji wa kifungu linganifu cha habari kwa ufahamu unafanyika kwa usahihi.
    5. Kusikiliza kifungu linganifu cha habari kwa ufahamu.
      1. Usikilizaji wa kifungu linganifu cha habari kwa ufahamu unafanyika kwa usahihi.
    6. Kutafsiri na kuelezea picha kwa kutumia chati za picha.
      1. Utafsiri na uelezeaji wa picha unafanyika kwa usahihi.
    1. Kuhusianisha habari/hadithi na uzoefu wa maisha/maarifa ya awali na hadithi nyingine ili kujenga ufahamu na umiliki wa habari katika matini.
      1. Uhusianishaji wa habari/hadithi na uzoefu wa maisha/maarifa ya awali na hadithi nyingine ili kujenga ufahamu na umiliki wa habari kwa usahihi.
    2. Kutumia kifungu cha habari kubaini msamiati mpya uliotumika ili kukuza ufahamu wa kusoma
      1. Ubainishaji wa msamiati mpya na uliotumika kukuza ufahamu wa kusoma unafanyika kwa usahihi.
    3. Kutumia kifungu cha habari kusoma na kujibu maswali, yenye kujibu maswali, yenye kupima ufahamu na kkuza msamiati kwa usahihi
      1. Usomaji wa kifungu cha habari unafanyika kwa usahihi na kujibu maswali yenye kupima ufahamu na kukuza msamiati kwa usahihi.
    4. Kutumia picha katika kifungu cha habari kueleza sifa za wahusika katika hadithi
      1. Uelezaji wa sifa za wahusika katika hadithi unafanyika kwa usahihi.
    5. Kutumia kifungu cha habari kutabiri matukio
      1. Utabiri wa matukio kwa kutumia kifungucha habari unafanyika kwa usahihi.
    1. Kusoma kifungu linganifu cha habari kwa kufuata vituo na sauti ya hisia. (Nukta, mkato, alama ya kuuliza na alama ya mshangao).
      1. Usomaji wa kifungu linganifu cha habari kwa kufuata vituo na sauti ya hisia unafanyika kwa usahihi.
    2. Kusoma kifungu linganifu cha habari kwa kasi inayostahili.
      1. Usomaji wa kifungu linganifu cha habari kwa kasi inayostahili unafanyika kwa usahihi.
    3. Kusoma kifungu cha habari kwa kuzingatia matamshi sahihi ya maneno.
      1. Usomaji wa kifungu cha habari kwa kuzingatia matamshi sahihi ya maneno unafanyika kwa usahihi.
    1. Kuunda na kusoma sentensi zinazotokana na maneno yaliyoundwa na silabi za herufi mwambatano na silabi za aina nyingine kwa kutumia kadi za maneno.
      1. Uundaji na usomaji wa sentensi zinazotokana na maneno yaliyoundwa na silabi za herufi mwambatano na silabi za aina nyingine kwa kutumia kadi za maneno umefanyika kwa usahihi.
    2. Kutenganisha kwa kutamka sauti mojamoja zilizounda maneno yanayotokana silabi za herufi na mwambatano na silabi za aina nyingine.
      1. Utenganishaji kwa kutamka sauti moja moja zilizounda maneno yanayotokana silabi za herufi na mwambatano na silabi za aina nyingine unafanyika kwa usahihi.
    3. Kuunganisha silabi za herufi mwambatano na silabi za aina nyingine ili kuunda maneno na kuyatamka
      1. Uunganishaji wa silabi za herufi mwambatao na silabi za aina nyingine ili kuunda maneno na kuyatamka unafanyika kwa usahihi.
    4. Kuunganisha na kuzitamka herufi mwambatano saba na herufi za irabu ili kupata silabi kwa kutumia kadi za herufi na kuzitamka.
    5. Kuhusianisha sauti na herufi mwambatano saba (ny, nd, sh, ng, th, kw, mb) kwa kutumia kadi za herufi mwambatano.
      1. Uhusianishaji wa sauti na herufi mwambatano saba (ny, nd, , sh, ng, th, kw, mb) kwa kutumia kadi za herufi mwambatano unafanyika kwa usahihi.
    6. Kuunda na kusoma sentensi zinazoundwa na maneno yanayotokana na silabi za konsonanti za kila kundi kwa kutumia kadi za maneno.
      1. Uundaji na usomaji wa sentensi zinazotokana na maneno yanayotokana na silabi za konsonanti za kila kundi unafanyika kwa usahihi.
    7. Kuhusianisha herufi ndogo na kubwa zote kwa kuzisoma katika maneno.
      1. Uhusianishaji wa herufi ndogo na kubwa zote kwa kuzisoma katika maneno unafanyika kwa usahihi.
    8. Kutenganisha kwa kutamka sauti moja moja zilizounda maneno yanayotokana na herufi 24 kwa kutumia kadi za herufi.
      1. Utenganishaji wa sauti moja moja zilizounda maneno yanayotokana na herufi 24 kwa kutumia kadi za herufi unafanyika kwa usahihi.
    9. Kuunganisha silabi zinazotokana na herufi zote ishirini na nne ili kuunda maneno na kuyatamka.
      1. Uunganishaji wa silabi zinazotokana na herufi zote ishirini na nne ili kuunda maneno na kuyatamka unafanyika kwa usahihi.
    10. Kutenganisha kwa kutamka sauti za konsonanti na irabu zilizounda silabi.
      1. Utenganishaji wa sauti za konsonanti na irabu zilizounda silabi kwa kuzitamka unafanyika kwa usahihi.
    11. Kubaini majina ya vitu yanayoanza na silabi za irabu na kutenganisha silabi kwa kutamka.
      1. Ubainishaji wa majina ya vitu yanayoanza na silabi za irabu na utenganishaji wa silabi kwa kutamka unafanyika kwa usahihi.
    12. Kubaini majina ya wanafunzi yanayoanza na silabi za irabu katika darasa na kutenganisha silabi hizo kwa kuzitamka.
      1. Ubainishaji wa majina ya wanafunzi yanayoanza na silabi za irabu na utenganishaji wa silabi hizo kwa kuzitamka unafanyika kwa usahihi.
    13. Kubaini silabi zinazoundwa na irabu.
      1. Ubainishaji wa silabi zinazoundwa na irabu unafanyika kwa usahihi.
    14. Kuunganisha na kutamka sauti za konsonanti na irabu ili kuunda silabi.
      1. Uunganishaji na utamkaji wa sauti za konsonanti na irabu ili kuunda silabi unafanyika kwa usahihi.
    15. Kuhusianisha sauti na konsonanti (b, m, k, d, n); (l, t, p, s, f, j); (g, y z h, r, w, v, ch) kwa kutumia kadi za herufi.
      1. Uhusianishaji wa sauti na herufi za konsonanti kwa kuonesha kadi na kutamka umefanyika kwa usahihi
    16. Kutenganisha sauti za irabu zilizounda maneno kwa kuzitamka.
      1. Utenganishaji wa sauti za irabu zilizounda maneno kwa kuzitamka unafanyika kwa usahihi.
    17. Kuunganisha na kutamka sauti za irabu ili kuunda maneno.
      1. Uunganishaji na utamkaji wa sauti za irabu ili kuunda maneno unafanyika kwa usahihi.
    18. Kuhusianisha sauti na herufi za irabu (a e i o u) kwa kutumia kadi kuzitamka.
      1. Uhusianishaji wa sauti na herufi za irabu kwa kuzionesha katika kadi na kuzitamka unafanyika kwa usahihi.
    1. Kusimulia hadithi.
      1. Usimuliaji wa hadithi unafanyika kwa usahihi.
    2. Kusimulia matukio mbalimbali kuhusu sherehe
      1. Usimuliaji wa matukio mbalimbali kuhusu sherehe unafanyika kwa usahihi.
    3. Kuanzisha na kuendeleza mazungumzo kuhusu mchezo teule baina ya wanafunzi wawili.
      1. Uanzishaji na uendelezaji wa mazungumzo baina ya wanafunzi wawili kuhusu mchezo teule unafanyika kwa usahihi.
    4. Kutumia lugha ya heshima katika kuomba ruhusa na kuomba vitu.
      1. Lugha ya heshima katika kuomba ruhusa na kuomba vitu inatumika kwa usahihi.
    5. Kusalimiana na kuagana kati ya watoto na watu wazima na watoto wenyewe kwa wenyewe.
      1. Kusalimiana na kuagana na watu wote kunafanyika kwa usahihi.
    6. Kujitambulisha mwenyewe na kutambulisha watu wengine.
      1. Utambulisho wa mtoto mwenyewe na utambulisho wa watu wengine unafanyika kwa usahihi.