Kuandika Darasa la I Syllabus

    1. Kuandika kwa kunakili kifungu cha habari kwa mwandiko wa chapa wenye vikonyo katika daftari la mwandiko.
      1. Uandikaji kwa kunakili kifungu cha habari kwa mwandiko wa chapa wenye vikonyo katika daftari la mwandiko unafanyika kwa usahihi.
    1. Kuandika hadithi fupi yenye aya mbili (kila aya maneno 15) kutokana na chati ya picha
      1. Uandishi wa hadithi kulingana na chati ya picha unafanyika kwa usahihi
    2. Kutunga hadithi fupi yenye kueleweka na ushikamani kwa kutumia kadi za picha
      1. Uandishi wa hadithi fupi yenye kueleweka na ushikamani unafanyika kwa usahihi.
    3. Kutunga hadithi fupi yenye kueleweka na ushikamani
      1. Utungaji wa hadithi fupi yenye kueleweka na ushikamani unafanyika kwa usahihi.
    1. Kutunga hadithi yenye mfuatano mzuri wa matukio. kwa kuandika.
      1. Utungaji wa hadithi yenye mfuatano mzuri wa matukio kwa kuandika unafanyika kwa usahihi.
    2. Kuandika sentensi zenye kuonesha mfuatano wa matendo ya siku.
      1. Uandikaji wa sentensi zenye kuonesha mfuatano wa matendo ya siku unafanyika kwa usahihi.
    3. Kuandika kwa kupanga sentensi zilizo changanywa ili kupata mfuatano wa matukio.
      1. Uandikaji kwa kupanga sentensi zilizochanganywa ili kupata mfuatano wa matukio unafanyika kwa usahihi.
    4. Kuandika hadithi fupi yenye mfuatano wa matukio kutokana na picha zilizopangwa kwa mfuatano.
      1. Uandikaji wa hadithi fupi yenye mfuatano wa matukio kutokana na picha zilizopangwa kwa mfuatano, unafanyika kwa usahihi.
    1. Kutunga sentensi zenye maneno yasiyozidi sita zenye kueleweka na ushikamani kwa kuandika.
      1. Utungaji wa sentensi zenye maneno yasiyozidi sita, zenye kueleweka na ushikamani kwa kuandika unafanyika kwa usahihi.
    2. Kuandika neno au maneno yaliyokosekana katika sentensi ili kukamilisha maana.
      1. Uandikaji wa neno au maneno yaliyokosekana katika sentensi unafanyika kwa usahihi.
    3. Kutunga sentensi zinazotokana na neno moja teule kwa kuandika.
      1. Utungaji wa sentensi kwa kuandika kwa kutumia neno moja teule unafanyika kwa usahihi.
    4. Kuandika sentensi sahihi kutokana na vifungu vya maneno yaliyochanganywa.
      1. Uandikaji wa sentensi sahihi kutokana na vifungu vya maneno yaliyochanganywa unafanyika kwa usahihi.
    5. Kuandika kwa kuunganisha sehemu mbili za sentensi ili kupata maana kamili.
      1. Uandikaji kwa kuunganisha sehemu mbili za sentensi ili kupata maana kamili unafanyika kwa usahihi.
    1. Kuandika hadithi fupi anayoifahamu kwa mtiririko wa matukio wenye mantiki
      1. Uandishi wa hadithi fupi anayoifahamu kwa mtiririko wa matukio wenye mantiki sahihi.
    2. Kupanga sentensi zilizochanganywa ili kuleta mtiririko wenye mantiki
      1. Upangaji wa sentensi zilizochanganywa ili kuleta mtiririko ulio sahihi.
    3. Kuunda sentensi zenye mtiririko mzuri kwa kutumia picha teule.
      1. Uundaji wa sentensi zenye mtiririko mzuri kwa kutumia picha teule unafanyika kwa usahihi.
    4. Kupanga sentensi tano zenye maneno kadiri ya mtiririko wa matukio kwa usahihi.
      1. Upangaji wa sentensi tano zenye maneno kadiri ya mtiririko wa matukio kwa usahihi.