Hisabati

FEDHA
♿ Accessibility: | | | |

FEDHA

Thamani ya fedha za Tanzania (kuanzia shilingi 1 hadi shilingi 2000)
Utangulizi
Fedha ni kitu muhimu kinachotumiwa na watu katika maisha ya kila siku kununua na kuuza vitu mbalimbali. Watoto hukutana na fedha wanaponunua peremende, kalamu, daftari au chakula. Watu wazima pia hutumia fedha kupata mahitaji yao ya kila siku.
Tumia picha sahihi za sarafu
Tumia "watoto hutumia fedha" badala ya "watoto hukutana na fedha"
Kubainisha alama zilizomo katika sarafu na noti
Kubainisha alama zilizomo katika sarafu na noti
Tumia picha zifuatazo kubainisha alama maalum zinazopatikana katika fedha halali (sarafu na noti za elfu moja na elfu mbili)
1.
2
3.
tumia picha sahihi ya sarafu
4.
5
Kuelezea thamani ya sarafu na noti
Kuelezea thamani ya sarafu na noti
Utangulizi
Kujifunza thamani ya fedha huwasaidia wanafunzi kuelewa uwezo wa kununua bidhaa na mabadiliko ya kiuchumi, huku kikiwajengea uwezo wa kutambua sarafu na kutumia rasilimali kwa busara katika maisha ya kila siku.Sasa tujifunze thamani ya sarafu na noti.Kwa kutumia picha zifuatazo, jaza jadweli lifuatalo
Liko wapi jadweli husika?
1.
2.
3.
4.
5.
6.
Kusiriba sarafu zenye thamani tafauti
Kusiriba sarafu zenye thamani tafauti
Hatua za kusiriba sarafu (kwa matumizi ya darasani, hasa darasa la kwanza):
1. Tafuta vifaa
  • Sarafu yoyote (yenye Thamani ya shilingi: 50, 100, 200, 500)
  • Karatasi nyeupe
  • Penseli iliyochongwa vizuri
2. Weka sarafu
  • Weka sarafu juu ya uso tambarare
3. Funika kwa karatasi
  • Weka karatasi juu ya sarafu na uishikilie isitembee.
4. Siriba kwa penseli/krayoni
  • Pitisha penseli juu ya karatasi taratibu hadi alama za sarafu zionekane.
5. Endelea hadi picha ionekane vizuri
  • Hakikisha umesiriba pande zote za sarafu.
6. Tazama matokeo
  • Angalia picha iliyojitokeza; jadili alama, maandishi au picha zilizo kwenye sarafu.
Je, umeona nini, endelea kufanya hivyo kwa sarafu zoteZoezi
neno "zote" limechanganyika na neno "zoezi" Yatenganishe ili kupata maana iliyokusudiwa
Exercise 12
Jibu maswali yafuatayo
  1. Umeona nini baada ya kusiriba sarafu?
  2. Umbo la picha ya sarafu ni lipi?
  3. Taja alama moja uliyoyaona kwenye picha ya sarafu.
  4. Je, maandishi ya sarafu yalionekana? (Ndiyo / Hapana)
Matumizi ya Fedha za Tanzania
Umahiri Unaotarajiwa Kuupata kwa Mada Ndogo hii.
Mada hii inajenga umahiri wa mwanafunzi katika nidhamu, uaminifu, na uwajibikaji wa fedha, ikimwezesha kufanya maamuzi sahihi ya matumizi kulingana na mahitaji, kushirikiana na wengine katika biashara, na kujieleza kwa ujasiri kuhusu utunzaji wa rasilimali.
Matokeo Mahsusi ya Ujifunzaji
Baada ya kujifunza mada ndogo hii, utaweza:
  • Kutambua maana ya matumizi ya fedha.
  • Kutaja njia mbalimbali za kutunza fedha.
  • Kutofautisha kati ya matumizi mazuri na matumizi mabaya ya fedha.
  • Kueleza kwa maneno rahisi kwa nini ni muhimu kutunza fedha.
Kujadili njia za kutunza fedha
Kujadili njia za kutunza fedha
Utangulizi.
Fedha ni sehemu muhimu ya maisha ya kila siku ya binadamu. Kila siku unakutana na fedha unapokuwa dukani, nyumbani au skuli. Katika mada hii, utajifunza kwa vitendo halisi namna bora ya kutumia na kutunza fedha ili ujenge misingi imara ya nidhamu ya kifedha tangu ukiwa mdogo.
Maswali:
  • Kwa nini unatumia fedha?
  • Kama ningekupa shilingi 1,000, ungetumia kununua nini?
  • Chagua kitu muhimu: Ungechagua peremende (pipi) au mkate? Kwa nini?
Maelezo
Matumizi ya fedha ni namna unavyotumia pesa ulizonazo kupata mahitaji yako. Kwa mfano, kununua kalamu, daftari au chakula kidogo. Kutunza fedha ni tabia njema inayokusaidia kutotumia pesa zote mara moja.
tusichanganye matumizi ya neno 'Fedha' na 'Pesa' ili kupata mtiririko mzuri
Njia za Kutunza Fedha:
  • Kuweka pesa kwenye kopo au sanduku la akiba.
  • Kutumia fedha kwa kununua vitu muhimu tu.
  • Kuepuka kupoteza, kuchana au kuchafua fedha.
Katika Mazingira Halisi:
  • Nyumbani: Wazazi hukusaidia kuweka akiba badala ya matumizi yasiyo ya lazima.
  • Skuli: Unajifunza kutumia pesa kwa nidhamu.
  • Dukani: Unachagua kununua kitu muhimu kuliko vitu vingi visivyo na lazima.
Mifano ya Matumizi ya Fedha
  1. Asha anaweka shilingi 300 kwenye kopo la akiba (kibubu) na kutumia shilingi 200 kununua kalamu.
  2. Juma anachagua kununua daftari badala ya peremende (pipi).
  3. Mariam anaweka fedha salama kwenye pochi.
Kuhifadhi na kuweka akiba
Kuhifadhi na kuweka akiba
Matokeo Mahsusi ya Ujifunzaji
Baada ya kujifunza mada hii, mwanafunzi ataweza:
  • Kueleza maana ya kuhifadhi fedha na kuweka akiba.
  • Kutaja njia mbalimbali za kuhifadhi na kuweka akiba.
  • Kutofautisha kati ya kutumia fedha zote na kuweka akiba.
  • Kuonesha tabia ya kuhifadhi na kuweka akiba katika maisha ya kila siku.
Utangulizi.
Kuweka akiba ni kama kupanda mbegu. Unajifunza uvumilivu, nidhamu na kupanga maisha ya baadaye.
Nini Utajifunza kwa Ufupi.
  • Maana ya kuhifadhi fedha.
  • Maana ya kuweka akiba.
  • Njia rahisi za kuweka akiba.
  • Umuhimu wa akiba kwa sasa na baadaye
Maelezo.
Kuhifadhi fedha ni kuweka pesa mahali salama. Kuweka akiba ni kutenga sehemu ya pesa kwa matumizi ya baadaye. Tabia hii humsaidia mtoto kuwa na malengo, kujizuia na kujiamini. Unaweza kuhifadhi fedha kwa kuweka kwenye pochi, chupa au kopo la akiba (kisanduku Bubu).
tusichanganye matumizi ya neno 'Fedha' na 'Pesa' ili kupata mtiririko mzuri
Mifano ya Maisha Halisi
  1. Amani anaweka nusu ya pesa kwenye kopo (kibubu).
  2. Neema anatumia pochi kuhifadhi pesa.
  3. Baraka anaweka akiba kununua begi la skuli.
Kutumia fedha kwa kuuza na kununua bidhaa
Kutumia fedha kwa kuuza na kununua bidhaa
Utangulizi.
Michezo ya kuigiza kama mchezo wa duka humwezesha mtoto kujifunza kwa vitendo kuhusu kuuza na kununua bidhaa, uaminifu na matumizi sahihi ya fedha.
Kwa mfano:Je!
“Umewahi kwenda dukani kununua bidhaa?”
“Ulinunua bidhaa gani?
Hebu tumia dakika kidogo kucheza na mwenzako mchezo wa duka. Ili ujikumbushe kuuza na kununua.
SEHEMU YA 1: Mnunuzi Anafika Dukani
(Mnunuzi anaingia huku akiwa na pochi yake)
Mnunuzi: "Hodi! Habari ya kazi muuzaji?"
Muuzaji: "Salama! Karibu sana dukani. Unahitaji nini leo?"
Mnunuzi: "Nataka kununua biskuti moja na penseli moja. Ni shilingi ngapi?"
Muuzaji: "Biskuti ni shilingi 200 na penseli ni shilingi 300. Jumla ni shilingi 500."
SEHEMU YA 2: Malipo na Bidhaa Sahihi
(Mnunuzi anatoa pesa na kumpa muuzaji)
Mnunuzi: "Haya, chukua shilingi 500 hizi hapa."
Muuzaji: (Anahakiki pesa) "Asante. Umetoa pesa sahihi kabisa. Ngoja nikupe biskuti yako na penseli yako." (Muuzaji anachukua biskuti na penseli na kumpa mnunuzi kwa uaminifu).
SEHEMU YA 3: Mtihani wa Pesa ya Bandia
(Mnunuzi anajifanya anataka kuongeza kitu kingine, lakini anatoa pesa ya bandia kwa makusudi)
Mnunuzi: "Ah, nimesahau! Nataka na hii siagi ya shilingi 2000. Chukua pesa hii." (Anampa karatasi iliyochorwa vibaya).
Muuzaji: (Anaitazama pesa kwa makini, kisha anaitikisa kichwa) "Hapana mteja wangu! Pesa hii siyo halali. Hii ni pesa ya bandia, haina alama sahihi na haina thamani hapa dukani."
Mnunuzi: "Oh! Kumbe ni lazima niwe mwangalifu na pesa ninazobeba."
Muuzaji: "Ndiyo, ni muhimu kutumia pesa halali ili biashara iendelee na kila mmoja awe mwaminifu."
SEHEMU YA 4: Hitimisho.
Muuzaji: "Je, ungependa chenji yako ya shilingi 100 nikuwekee kwenye Kopo lako la Akiba?"
Mnunuzi: "Ndiyo! Maana si pesa zote hutumika mara moja. Niwekee baki yangu kwenye kopo!"
Mambo ya Kusisitiza Baada ya Mchezo
  • Umakini
  • Uaminifu
  • Hesabu na maamuzi sahihi
Matokeo Mahsusi ya Ujifunzaji
Baada ya mada hii, mwanafunzi ataweza:
  • Kueleza maana ya kuuza na kununua bidhaa.
  • Kutumia fedha kwa usahihi.
  • Kushiriki michezo ya kuigiza.
  • Kuonesha uaminifu na nidhamu ya fedha.
Maelezo.
Kununua ni kutoa fedha kupata bidhaa, na kuuza ni kumpa mtu bidhaa ili kupata fedha. Shughuli hizi hujenga ujuzi wa maisha, mawasiliano na maamuzi.Katika mazingira yetu, shughuli hizi hutokea dukani, sokoni, skuli au nyumbani.
Listening to this topic