Hisabati
MATENDO YA KIHISABATI
MATENDO YA KIHISABATI
Kujumlisha nambari jumla isiyozidi 200
Kuongeza vitu ili kupata jumla yake
Kuongeza vitu ili kupata jumla yake
Baada ya somo hili, mwanafunzi aweze:
- Kuhesabu vitu kwa usahihi.
- Kuunganisha makundi mawili au zaidi ya vitu.
- Kutumia alama ya kujumlisha (+) kwa usahihi.
- Kueleza kwa maneno jinsi ya kupata jawabu.
Katika mada hii, mtoto atajifunza:
- Maana ya kujumlisha.
- Kuongeza vitu halisi ili kupata jumla.
- Kuandika sentensi za kihisabati za kujumlisha.
- Kujumlisha nambari ambazo jumla yake haizidi 200.
Neno kuongeza katika hisabati linamaanisha kuchanganya vitu viwili au zaidi ili kupata jumla yake.
Kwa maneno mengine:
Example 6
Una embe mbili na rafiki yako akakupa embe tatu za ziada, je utakuwa na embe ngapi?


Utakuwa na embe tano

Example 7
Una embe mbili na rafiki yako akakupa embe mbili za ziada, je utakuwa na embe ngapi?


Utakuwa na embe tano

Kuongezahutokezea wakati unapata vitu vipya kuunganishwa na vile ulivyo navyo.
Example 8
Ukiwa na machungwa 5 na rafiki yako anakupa mengine 2, utakuwa na machungwa mangapi?
Una machungwa 5
Rafiki anakupa machungwa 2 zaidi
Jumla ya machungwa = 5 ongeza 2 = 7
Example 9
Mfano 1:
Una embe 3

Rafiki yako anakupaembe 2 zaidi

Jumla ya embe = 3 ongeza 2 = 5

picha zimegeuka juu chini chini juu
KUJUMLISHA NAMBARI
Kujumlisha ni kuweka pamoja vitu viwili au zaidi ili kujua jumla yake.Kwa mfano, mtoto unaweza kuwa na
- Kalamu 5 nyumbani
- Akapewa kalamu 3 shuleni
Tutumie neno Skuli badala ya Shule
Unapoziweka pamoja na kuzihesabu, utapata kalamu 8
Hivyo:
5 + 3 = 8
Example 10
Una machungwa 4, unapewa machungwa mengine 3.
4 + 3 = 7
Jumla ni machungwa 7.
Example 11
Kuna kuku 10 kwenye banda la kwanza na kuku 5 kwenye banda la pili.
10 + 5 = 15
Jumla ya kuku ni 15.
Example 12
Mwalimu ana penseli 25 na mwanafunzi anamletea penseli 20.
25 + 20 = 45
Jumla ya penseli ni 45.
Exercise 2
Mazoezi ya Mada Ndogo.
(A) RAHISI
- 2 + 3 = _____
- 6 + 4 = _____
(B) WASTANI
- 15 + 10 = _____
- 24 + 16 = _____
(C) GUMU
- 75 + 25 = _____
- 98 + 12 = _____
HITIMISHO
Mwalimu ahakikishe mtoto:
- Anajumlisha kwa kutumia vitu halisi
- Anaelewa alama ya (+)
- Anaweza kueleza jibu lake kwa maneno
Kutumia alama ya kujumlisha katika kuongeza vitu
Kutumia alama ya kujumlisha katika kuongeza vitu
Baada ya kujifunza mada hii, mtoto ataweza:
- Kutambua alama ya kujumlisha (+).
- Kuongeza makundi mawili ya vitu.
- Kuandika hesabu rahisi za kujumlisha.
- Kuhesabu na kusema jumla kwa usahihi.
- Kueleza kwa maneno jinsi alivyopata jibu.
Katika somo hili, mtoto atajifunza:
- Maana ya alama ya kujumlisha (+).
- Jinsi ya kuitumia alama (+) kuongeza vitu.
- Kuandika hesabu za kujumlisha kwa usahihi.
Tubadilishe neno mtoto na kuweka neno mwanafunzi
Mtoto utajifunza kuwa alama ya kujumlisha (+) hutumika wakati anapotaka kuongeza au kuweka pamoja vitu.
- Hesabu kundi la kwanza la vitu.
- Hesabu kundi la pili la vitu.
- Yaweke makundi hayo pamoja.
- Hesabu jumla ya vitu vyote pamoja.
UTANGULIZI:
Kujumlisha kwa kutumia alama ya kujumlisha (+) ni kuonyesha kuweka vitu pamoja au kuongeza idadi kwa njia fupi kwa kutumia alama ya "+"
Alama ya kujumlisha inaonekanaje?
Alama yake ni: “+” (inaitwa "jumlisha" au "ongeza" ).
Mfano. Kwa kutumia embe.
"Nina embe 3. Rafiki yangu ananipa embe 2 zaidi. Jumla ni embe 5."
Hivyo kwa kutumia alama ya kujumlisha, Tunaandika kwa njia fupi:
3 + 2 = 5
“Tatu ongeza mbili ni sawa na tano."
Kwa vitendo, Uanaweza:
- Kuona embe 3 → andika 3
- Kuona embe 2 zaidi → andika + 2
- Kuweka yote pamoja na kuhesabu → andika = 5
Kwa hiyo, kujumlisha kwa alama (+) ni kuonyesha kwa ufupi kuongeza vitu viwili au zaidi pamoja ili kupata jumla yake.
Example 13
Jumlisha

Hesabu:
2 + 3 = 5
Tambua kuwa alama (+) inaonyesha kuongeza.
Example 14
Nina mawe 4. Ninaongezewa mawe 2.
4 + 2 = 6
Ninapata mawe 6.
Example 15
Kuna watoto 5 darasani. Wanaingia watoto 3 zaidi.
5 + 3 = 8
Jumla ya watoto ni 8.
Example 16
Nina kalamu 10. Rafiki yangu ananipa kalamu 5.
10 + 5 = 15
Ninapata kalamu 15.
Exercise 3
(A) RAHISI
- 1 + 2 = ____
- 3 + 5 = ____
(B) WASTANI
- 6 + 7 = ____
- 9 + 8 = ____
(C) GUMU
- 14 + 6 = ____
- 18 + 12 = ____
HITIMISHO
Mtoto akifanikiwa:
- Kutambua alama (+)
- Kuongeza vitu
- Kuandika hesabu
- Kueleza alichofanya
Basi lengo la somo limefikiwa.
Kujumlisha nambari kwa kutumia alama ya kujumlisha
Kujumlisha nambari kwa kutumia alama ya kujumlisha
UMAHIRI UNAOTARAJIWA
Baada ya somo hili, mwanafunzi aweze
- Kutambua alama ya kujumlisha (+).
- Kuongeza makundi mawili ya vitu.
- Kuandika sentensi rahisi ya kujumlisha.
- Kuhesabu na kusema jumla kwa usahihi.
- Kueleza kwa maneno kile anachofanya (ongeza).
Katika mada hii, mtoto utajifunza:
- Maana ya alama ya kujumlisha (+).
- Jinsi ya kuitumia alama ya (+) kuunganisha vitu.
- Kuandika hesabu za kujumlisha kwa kutumia alama (+).
UTANGULIZI
“Kutumia alama ya kujumlisha (+)” inamaanisha ni kuunganisha au kuongeza idadi mbili au zaidi ili kupata jumla yake. Alama ya + inaonyesha kuwa tunapaswa kuchanganya nambari hizo, au vitu hivyo.
1. 3 + 2 = 5
Hapa, tunachanganya 3 na 2, na jumla yao ni 5
2. 4 + 6 + 1 = 11
Hapa, tunajumlisha nambari tatu: 4, 6, na 1, na jumla ni 11.
Maelezo:
- Alama + inamaanisha “ongeza” au “kujumlisha.”
- Kila nambari inayofuata kwenye kielelezo cha + inaongezwa kwenye ile ya awali.
- Mwisho wa hesabu huonyesha jumla ya nambari zote.
Alama ya kujumlisha (+) hutumika pale tunapotaka kuongeza au kuweka pamoja vitu.
Example 17
Una mawe 4, unaongezewa mawe 2.
4 + 2 = 6
Jumla ni mawe 6.
Example 18
Kuna watoto 5 darasani, wanaingia watoto 3 wengine.
5 + 3 = 8
Jumla ya watoto ni 8.
Example 19
Una kalamu 10, rafiki yako anakupa kalamu 5.
10 + 5 = 15
Jumla ya kalamu ni 15.
Exercise 4
(A) RAHISI
- 1 + 2 = ____
- 3 + 4 = ____
(B) WASTANI
- 6 + 5 = ____
- 9 + 7 = ____
(C) GUMU
- 15 + 10 = ____
- 18 + 12 = ____
HITIMISHO
Mtoto akifanikiwa:
- Kutambua alama (+)
- Kuongeza vitu
- Kuandika hesabu
- Kueleza alichofanya
Basi lengo la somo limefikiwa.
Kutoa nambari baina ya 1 na 200
Kupunguza vitu kupata idadi ya vitu vilivyobaki
Kupunguza vitu kupata idadi ya vitu vilivyobaki
UTANGULIZI.
“Kupunguza vitu katika Hisabati” inamaanisha kuondoa au kutoa sehemu fulani ya vitu ulivyo navyo ili kupata idadi iliyobaki. Katika Hisabati, tunatumia alama ya toa (-) kuonyesha kupunguza au kutoa.
Kwa maneno rahisi:
- Ikiwa una vitu vichache na unapunguza baadhi, unapata vile viliyobaki.
- Hii ni tofauti na kujumlisha, ambapo unaongeza vitu.
Mfano rahisi kwako:
1). 5 - 2 = 3
Ikiwa una mabofu (mapulizo) 5 na unampa rafiki yako mabofu (mapulizo) 2 uliyonayo sasa yatakuwa ni 3.
2). 7 - 4 = 3
Ikiwa una vitabu 7 na unatoa 4 kwa darasa, vitabu vilivyobaki ni 3.
Maelezo:
- Alama - inamaanisha toa au punguza.
unbold
Anza kwa kuangalia na kushika vitu ulivyonavyo, kama mawe, karanga, kalamu au matunda.
Sema ukiwa:
- “Nina pipi 5.”
- “Nimempa rafiki yangu pipi 2.”
- “Zimebaki pipi ngapi?”
Ondoa vitu vilivyotolewa, uvihesabu vilivyobaki, na sema jibu kwa sauti.Aanza kuelewa kuwa kutoa ni kupunguza au kuondoa baadhi ya vitu.
MAELEZO.
Kutoa ni kuondoa au kupunguza baadhi ya vitu kutoka kwenye vitu vingi ili kujua vilivyobaki.
Fanya hatua hivi:
- Hesabu vitu vyote ulivyonavyo.
- Ondoa idadi ya vitu vilivyotolewa.
- Hesabu vilivyobaki.
Example 20
Mfano ukiwa:

Ondoa

5 − 2 = 3
Kumbuka kuwa alama (−) inaonyesha kutoa.
Example 21
Nina mawe 8. Natoa mawe 3.
8 − 3 = 5
Yamebaki mawe 5.
Example 22
Nina kalamu 12. Rafiki yangu anakopa kalamu 4.
12 − 4 = 8
Zimebaki kalamu 8.
Example 23
Kuna kuku 20. Kuku 6 wameuzwa.
20 − 6 = 14
Kuku waliobaki ni 14.
Exercise 5
(A) RAHISI
- 5 − 2 = ____
- 9 − 4 = ____
(B) WASTANI
- 15 − 6 = ____
- 24 − 9 = ____
(C) GUMU
- 40 − 18 = ____
- 85 − 27 = ____
Kutumia alama ya kutoa katika kupunguza idadi ya vitu
Kutumia alama ya kutoa katika kupunguza idadi ya vitu
UTANGULIZI.
“Kupunguza katika mzingira ya kawaida” inamaanisha kutoa au kupunguza idadi ya vitu halisi unavyoviona au kutumia kila siku ili kupata idadi iliyobaki. Hapa, si hesabu tu kwenye karatasi, bali ni kujifunza hesabu kwa kutumia vitu halisi.
Example 24
Kwa mfano:
1. Vitu vya nyumbani
- Una mapeni 6 kwenye begi, ukitumia 2, uliyo nayo sasa ni 4.
- Hapa unapunguza vitu vilivyotumika.
2. Matunda
- Una embe 5 kwenye bakuli, ukila 2, yaliyo baki ni 3.
Vitu vya kuchezea
- Una magari 8, ukitumia magari 3 kucheza, yaliyo baki ni 5.
Ufafanuzi:
Kutoa nambari kwa kutumia alama ya kutoa
Kutoa nambari kwa kutumia alama ya kutoa
Mafumbo rahisi ya Kujumlisha(ja wabu lisizidi 200) na Kutoa (baina ya 1 na 200)
Kubadilisha maneno kuwa nambari
Kubadilisha maneno kuwa nambari
inaoekana hapa haijakamilika
Kubainisha alama za kujumlisha na kutoa katika mafumbo
Kubainisha alama za kujumlisha na kutoa katika mafumbo
inaoekana hapa haijakamilika
Kufumbua mafumbo rahisi
Kufumbua mafumbo rahisi
inaoekana hapa haijakamilika
angalia kwa makini wingi wa neno embe na gari kila sehemu yalipotumika maeno haya
Listening to this topic