Hisabati
Nambari Nzima
Reading settings
Text size
Line spacing
Colours
Nambari Nzima
Utambuzi wa kuhesabu nambari
UTANGULIZI WA MADA KUU
Mada ya Namba Nzima humsaidia mwanafunzi wa Darasa la Kwanza kujenga uelewa wa msingi wa kuhesabu, kutambua idadi, na kuoanisha namba na vitu halisi vinavyomzunguka. Kupitia mada hii, mwanafunzi hujifunza kuwa namba huwakilisha kiasi cha vitu katika maisha ya kila siku kama vile matunda, viti, kalamu, samaki na vitu vingine vinavyopatikana katika mazingira ya Zanzibar. Mada hii huandaa msingi wa kujifunza hesabu za juu zaidi baadaye.

Kuhesabu vitu (kuanzia1 hadi 200)
UTANGULIZI WA MADA NDOGO
Katika mada hii ndogo, mwanafunzi hujifunza kuhesabu vitu kwa usahihi kuanzia 1 hadi 200 kwa kutumia vitu halisi, picha na michezo. Lengo ni kumsaidia mwanafunzi kuunganisha namba na idadi ya vitu, kupanga vitu, na kuhesabu vitu vya aina tofauti kwa njia rahisi, ya kuvutia na inayomshirikisha kikamilifu.
Maana ya Kuhesabu Vitu Moja Moja- Kuhesabu vitu moja moja ni tendo la kutaja namba kwa sauti huku ukigusa au kuonyesha kila kitu kimoja kwa wakati wake.
Ufafanuzi kwa Mtoto:
Tunapohesabu, tunagusa au tunaonyesha kila kitu kimoja na kusema namba moja. Hakuna kitu kinachorukwa, wala kuhesabiwa mara mbili.
Mfano wa Maisha Halisi: Mtoto akihesabu embe, anagusa embe moja na kusema “moja”, kisha embe la pili “mbili”, na kuendelea hivyo.

Kuainisha vitu kwa kuhesabu.
kulinganisha vitu kwa uzito
hesabati maandalizi On air
Kuainisha vitu kwakuhesabu.
Hii ni stadi ya kuunganisha kitu kimoja na namba moja tu. Mwanafunzi hujifunza kuwa kila namba huwakilisha kitu kimoja.
Ufafanuzi kwa Mtoto:
Tubadilishe neno mtoto kwa kuweka neno mwanafunzi
Kila kitu kinapata namba yake. Kitu kimoja = namba moja.
Mfano 1
Mfano wa Maisha Halisi: Mwalimu anaweka penseli 5 mezani. Mwanafunzi anaonyesha penseli ya kwanza akisema “1”, ya pili “2”, hadi “5”.

Kuhesabu Vitu kwa Mpangilio Sahihi (1, 2, 3, …)
Mtoto hujifunza kutaja namba kwa mpangilio sahihi bila kuruka au kurudia namba. Hii humsaidia kujenga ufasaha wa kuhesabu hadi 200 kulingana na uwezo wake.
Tunapohesabu, tunaanza na moja, kisha mbili, tatu, nne…
Mfano 2
Mfano wa Maisha Halisi: Mtoto anahesabu wanafunzi waliokaa mstari kuanzia wa kwanza hadi wa mwisho.

Shughuli 1
Chunguza picha kwa uangalifu, halafu hesabu vitu tafauti kama wanavyo hesabu hao watoto

Video ya wimbo wa kuhesabu (1–20 au zaidi) kwa Kiswahili.
Kuhesabu kwakupanga vitu kulingana na sifa zake.
Maudhui (Contents)
- Kupanga vitu kwa rangi, aina au ukubwa.
- Kuhesabu kila kundi baada ya kupanga.

Kuhesabu vitu tafauti.
Kuhesabu vitu tofauti kwa watoto wa Darasa la Kwanza
Kuhesabu vitu tofauti ni shughuli ya msingi ya Hisabati inayolenga kuwasaidia watoto wa Darasa la Kwanza kutambua namba kwa kuhesabu vitu halisi vinavyowazunguka.
Maudhui Pamoja na Picha na Video
Picha inaonesha matumizi ya nambari katika kuhesabu vitu tafauti

Picha ina onesha matumizi ya nambari katika kuhesabu vitu tafauti

Kusoma Nambari (kuanzia1 hadi 200)
Utangulizi:
Kusoma nambari (1–200) ni msingi wa hisabati, kwani hutumika kila siku katika kuhesabu, kupima muda, kufanya biashara na kutambua nafasi. Uelewa huu hujenga msingi wa kufanya hesabu rahisi na kulinganisha nambari.
Matokeo mahususi
Kubainisha maumbo ya nambari
Kupanga nambari kwa mtiririko wake
Maudhui: Kupanga nambari kwa mtiririko ni kitendo cha kupanga nambari kufuata mpangilio sahihi kuanzia ndogo hadi kubwa au kubwa hadi ndogo.
Ujuzi huu humsaidia mwanafunzi kutambua mfuatano wa nambari, kulinganisha nambari, na kuhesabu kwa usahihi katika maisha ya kila siku.

Mfano 3
Panga nambari zifuatazo kwa mtiririko
23, 36, 30, 29, 31, 27, 24, 35, 25, 34, 28, 26, 29, 31, 33, 32
Jawabu: 23, 24, 25, 26, 27, 28, 29, 30, 31, 32, 33, 34, 35, 36.
Kusoma nambari kwa usahihi
Kusoma nambari kwa usahihi ni msingi muhimu wa kujifunza hesabu. Mwanafunzi anapaswa kutambua kila nambari kwa jina lake sahihi, bila kuchanganya tarakimu.
Mifano ya kusoma nambari kwa usahihi:
Mfano 4
Kitendo cha kwanza

- 7 — soma: saba
- 15 — soma: kumi na tano
- 28 — soma: ishirini na nane
- 40 — soma: arobaini
- 63 — soma: sitini na tatu
- 105 — soma: mia moja na tano
- 119 — soma: mia moja na kumi na tisa
- 140 — soma: mia moja na arobaini
- 108 — soma: mia moj na nane
- 199 — soma: mia moja na tisini na tisa
Nambari ni ni ndogo sana kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum (LSN)
Mfano 5
Kitendo cha pili
Kuoanisha kadi ya nambari na maneno

Kuandika Nambari (kuanzia 1 hadi 200).
Kuandika nambari kwa kufuata hatua
Shughuli 2
Soma kwa uangalifu hatua za uandishi wa nambari
- Anza juu ya mstari.
- Shusha kalamu taratibu.
- Fuata umbo la nambari vizuri.
- Maliza chini ya mstari.
- Rudia kuandika mpaka uizoe.

Kutafautisha muandiko wa nambari
Shughuli 3
Soma kwa uangalifu:Kutafautisha muandiko wa nambari maana yake ni kujua tofauti ya namna kila nambari inavyoandikwa na kuonekana.
- 1 → mstari mmoja wima
- 2 → huanza kwa mviringo juu na kumalizia mstari wa kulala
- 3 → ina miviringo miwili
- 4 → ina mstari wa kulala na wa kushuka
- 5 → huanza juu kwa mstari wa kulala na kuzunguka chini
- 6 → duara chini
- 7 → mstari wa kulala juu na mshazari
- 8 → duara mbili
- 9 → duara juu na mstari chini
- 0 → duara moja

Kuandika nambari kwa usahihi
Shughuli 4
Soma na uandike nambari kwa usahihi

Zoezi 1
Fanya mazoezi yafuatayo kwa usahihi

Listening to this topic