Hisabati

NYAKATI NA SAA
♿ Accessibility: | | | |

NYAKATI NA SAA

Nyakati
Utangulizi
Katika maisha ya kila siku, huwa tunaona mwanga wa jua, giza, pia tunaamka na kulala. Mambo haya hutokea kwa mpangilio maalum unaoitwa nyakati za siku. Mada hii itakusaidia kutambua na kubainisha nyakati hizi kwa kutumia mazingira unayoyaona kila siku. Kwa kujibu masuali haya yanaweza kukusaidia kuzijua nyakati mbalimbali wewe mwenyewe.
  • Je kawaida unaamka saa ngapi?
  • Siku unazokwenda skuli unakunywa chai wakati gani?
  • Je unakwenda skuli wakati gani?
  • Wakatihuo unaitwaje?
  • Je unarudi skuli saa ngapi?
  • Wakati huo unaitwaje?
  • Baada ya kurudi skuli unakwenda wapi?
  • Wakati huo unaitwaje?
  • Unaweza kutaja nyakati nyengine unazozijuwa?
Umahiri Unaotarajiwa.
Baada ya somo hili utaweza kukuza umahiri wako kwa kutambua na kutaja nyakati za siku ambazo humsaidia mtu kujieleza, kufikiri kimantiki, na kulinganisha mazingira ili kupanga shughuli na kutatua matatizo kwa usahihi kulingana na wakati husika.
Kubainisha nyakati katika siku
Kubainisha nyakati katika siku
Kubainisha Nyakati katika siku.
Nini Utajifunza kwa Ufupi.
Utajifunza:
  • Majina ya nyakati nne za siku.
  • Mpangilio wa nyakati kuanzia asubuhi hadi usiku.
Maelezo.
Nyakati za Siku ni mgawanyo ya muda ndani ya siku (saa 24) kulingana na mzunguko wa jua na shughuli za binadamu.
Siku imegawanyika katika nyakati nne kuu. Kila wakati una dalili zake ambazo unaweza kuziona au kuzihisi. Nyakati hizo ni Asubuhi, Mchana, Jioni na Usiku.
Hizo zote zinaitwa nyakati, na mpangilio wake uko hivi:
Asubuhi – ni mwanzo wa siku, jua huchomoza.
Mchana – jua huwa kali, kuna mwanga mwingi.
Jioni – jua huzama, mwanga hupungua.
Usiku – kuna giza, watu hulala.
Example 27
Jua likichomoza, ni asubuhi.
Example 28
Jua likiwa kali juu, ni mchana.
Example 29
Kukiwa na giza, ni usiku.
Kulinganisha vitendo katika nyakati za siku
Kulinganisha vitendo katika nyakati za siku
Utangulizi
Ingawa siku ina nyakati tofauti, pia ina vitendo tofauti.
Mara nyingi watoto wengi huwa wanafanya vitendo vile vile asubuhi, mchana, jioni na usiku. Mada hii itakusaidia kulinganisha vitendo kulingana na wakati wa siku.
  • Unaweza kueleza vitendo vyako vya kila siku?
  • Eleza kila kitendo unachofanya na wakati wake.
Nini Utajifunza kwa Ufupi.
Utajifunza:
  • Vitendo vya asubuhi, mchana, jioni na usiku.
  • Tofauti za vitendo katika nyakati mbalimbali.
Maelezo.
Kwa kila siku huwa unafanya Vitendo tofauti kulingana na wakati. Ila mara nyingi huwa vinalingana kwa Watoto wengi kulingana na eneo (Nchi au Kanda za nchi fulani) wewe na wenzako huwa mnafanya vitendo gani?
Je mnafanya vitendo kama hivi:
Vitendo vya Kila Siku
Asubuhi (12:00 asubuhi – 5:59 asubuhi)
  • Kumbuka kuamka mapema.
  • Kuoga na kupiga mswaki meno yako.
  • Kula kifungua kinywa.
  • Kuandaa vitu vya skuli.
  • Kuenda skuli au kusoma nyumbani.
Mchana (6:00 mchana – 8:59 mchana)
  • Kula chakula cha mchana.
  • Kupumzika kidogo baada ya chakula.
  • Kuenda Madrasa (Chuoni) kujifunza dini.
  • Kucheza na marafiki nyumbani.
  • Kufanya kazi ndogo ndogo za skuli au nyumbani.
Jioni (9:00 jioni – 12:59 jioni)
  • Kucheza nje au kushiriki michezo ya ndani.
  • Kusaidia wazazi kwa shughuli ndogo ndogo nyumbani.
  • Kula chakula cha jioni (usiku).
  • Kusoma vitabu au kufanya mazoezi ya nyumbani.
Usiku (1:00 usiku – 5:59 usiku)
  • Kuoga kabla ya kulala.
  • Kusoma hadithi au kusikiliza wazazi wakisoma.
  • Kuandaa nguo na vitu vya kesho.
  • Kulala ili kujiandaa kwa siku mpya.
Kwa kifupi:
  • “Kuamka ni asubuhi.”
  • “Kula chakula cha mchana ni mchana.”
  • “Kucheza ni jioni.”
  • “Kulala ni usiku.”
Example 30
Asubuhi tunaamka, usiku tunalala.
Example 31
Mchana tunajifunza, jioni tunapumzika.
Example 32
Mchana kuna mwanga, usiku kuna giza.
Exercise 10
Andika kitendo unachofanya asubuhi.
Exercise 11
Linganisha mchana na usiku.
Kufumbua mafumbo ya nyakati
Kufumbua mafumbo ya nyakati
Utangulizi
Wewe unapenda mafumbo. Mafumbo ya nyakati hukusaidia kufikiri na kuchagua wakati sahihi. Mada hii inakusudia uweze kutatua mafumbo rahisi ya nyakati.
Nini utajifunza kwa Ufupi.
  • Kujibu mafumbo ya nyakati.
Maelezo.
Mafumbo katika Hisabati.
Fumbo ni swali lililoandikwa kwa njia ya maelezo au hadithi badala ya nambari pekee.
Lengo lake ni kumpima mwanafunzi uwezo wa kutumia akili kubadili maneno kuwa hesabu.
Fumbo halikwambii moja kwa moja "jibu”, “jumlisha" au "toa". Unapaswa kugundua mwenyewe kutokana na maelezo.
Example 33
Mimi huonekana pale jua linapochomoza na kuamsha viumbe vyote. Mimi ni wakati gani?
Jibu: Asubuhi.
Mifano.
  1. Mimi ni wakati wa kuamka – Asubuhi.
  2. Mimi ni wakati wa kulala – Usiku.
  3. Mimi ni wakati wa kula chakula cha mchana – Mchana.
  4. Mimi ni wakati wa kucheza baada kurudi skuli. - jioni
Saa
Utangulizi
Ili kuelewa mpangilio wa shughuli za kila siku kama asubuhi, mchana na usiku, ni muhimu kujifunza dhana ya saa mapema. Somo hili linatumia mazingira halisi ya mwanafunzi kuelezea saa kwa kina, kuanzia kutambua saa kamili na nusu saa.
Mada ndogo hii inakusudia kukusaidia kuelewa maana ya saa na kutambua saa kamili na nusu saa kwa kutumia mazingira yako ya kila siku.
Umahiri Unaotarajiwa.
Mwanafunzi anatarajiwa kujifunza kutambua na kutumia saa katika mazingira ya nyumbani, skuli na jamii kwa ujumla. Atajengewa uwezo wa kuelewa mpangilio wa muda wa siku, kutamka na kusoma saa kwa usahihi, kuchora saa rahisi, na kutatua matatizo yanayohusu muda. Hatimaye, ataweza kutafsiri alama na michoro ya saa ili kutumia dhana ya muda kwa ufanisi katika maisha ya kila siku
Matokeo Mahsusi.
Kubainisha aina za saa
Kubainisha aina za saa
Nini Utajifunza kwa Ufupi.
Katika mada mdogo ya saa, utajifunza maana ya saa, kusoma saa kamili, nusu saa na aina mbalimbali za saa. Pia utajifunza matumizi na umuhimu wake katika kupanga shughuli za kila siku.
  • Saa → kifaa kinachotuonyesha wakati maalum unaopimika kwa kiwango cha saa, dakika na sekunde
  • Muda → ni kipindi kinachoonyesha mfululizo wa matukio au hali fulani au dhana ya wakati kwa ujumla.
Tofauti kati ya Saa na Muda
SaaMuda
Huonyesha wakatiHuonyesha kipindi
Hutumia saaHutumia dakika au saa
Mfano: Saa 2 asubuhiMfano: Dakika 20
Hitimisho:
Saa hutuambia ni saa ngapi?
Muda hutuambia kitendo kimechukua muda gani?
Maelezo.
Saa ni kipimo cha wakati katika siku. Ni chombo kinachotumika kuonyesha au kutambua wakati. Saa hutusaidia kujua ni muda gani tufanye shughuli fulani kama kuamka, kula, kusoma, kucheza na kulala. Katika mazingira yetu ya kila siku, saa huonekana katika sehemu nyingi, kama nyumbani, skulini, ofisini, sokoni au hata kwenye simu za wazazi.
Kuna aina mbalimbali za saa ambazo unaweza kuzitambua kirahisi ila kwa sasa tuzigawe katika aina mbili:
  • Saa za mishale (mshale): Huonyesha wakati kwa kutumia mishale.
  • Saa za kidijitali (digitali): Huonyesha wakati kwa kutumia nambari,
Example 34
Saa moja kamili kwa saa ya Mshale (Mshale)
Example 35
Saa moja kamili kwa saa ya Kidigitali.
Example 36
Mfano:
  1. Saa ya mkononi anayoivaa mzazi au mlezi yenye mishale.
  2. Saa ya kidijitali iliyo kwenye simu au redio.
  3. Saa ya kubwa ya Kidigitali katika uwanja wa Mpira.
Hitimisho.
Saa ni muhimu kwa kujenga uelewa wa dhana ya wakati. Kwa kutumia mifano halisi, masuali yenye viwango tofauti na mazoezi yanayohusisha mazingira ya kila siku, unaweza kuelewa aina za saa na umuhimu wake katika maisha yako.
Kusoma saa (kamili na nusu) kwa mtindo wa saa kumi na mbili
Kusoma saa (kamili na nusu) kwa mtindo wa saa kumi na mbili
Utangulizi.
Baada ya kuzijua aina za saa, hatua inayofuata ni kujifundisha kusoma saa. Kusoma saa hukusaidia kuelewa muda halisi wa kufanya shughuli zako za kila siku. Unatakiwa kusoma saa kamili na nusu saa kwa kutumia mtindo wa saa kumi na mbili, kwa lugha rahisi na inayohusiana na mazingira yako.
Nini Utajifunza kwa Ufupi.
Utajifunza kusoma saa kamili na nusu saa kwa kutumia saa ya mishale (mshale) na saa ya digitali katika mfumo wa saa kumi na mbili.
Maelezo.
Mtindo wa saa kumi na mbili hugawanya siku katika saa 12 zinazojirudia mara mbili: mchana na usiku. Katika mfumo huu, kusoma saa huanza na kuelewa mishale ya saa.
  • Mshale mfupi huonyesha saa.
  • Mshale mrefu huonyesha dakika.
Kusoma Saa Kamili.
Saa ya Mshale.
Saa kamili husomwa pale mshale mrefu unapokuwa kwenye nambari 12.
Example 37
Mshale mfupi ukiwa kwenye 2 na mshale mrefu kwenye 12:
Example 38
Mshale mfupi ukiwa kwenye 9 na mshale mrefu kwenye 12:
Kusoma Saa Kamili. Saa ya Kidigitali.
Kwa saa ya kidigitali ni rahisi kusoma kwani huonesha muda husika kwa nambariri.
Nambari za awali ni SAA na Nambariri zinazofuata ni DAKIKA.
Example 39
Kusoma Nusu Saa
Kwa saa ya mshale, nusu saa husomwa pale mshale mrefu unapokuwa kwenye nambariri 6.
Example 40
Mshale mfupi ukiwa kati ya 1 na 2, mshale mrefu kwenye 6:
Kwa saa ya Digitali, nusu saa husomwa pale, nambariri ya upande wa DAKIKA inaponesha 30.
Example 41
Nambari za awali ni 12 na Nambariri zinazofuata ni 30.
Example 42
Saa 3 kamili – Mshale mfupi uko kwenye 3 na mshale mrefu uko kwenye 12.
Example 43
Saa 5 kamili – Mshale mfupi uko kwenye 5 na mshale mrefu uko kwenye 12.
Example 44
Saa 4 na nusu – Mshale mfupi uko baina ya 4 na 5 na mshale mrefu uko kwenye 6.
Hitimisho
Kusoma saa kamili na nusu saa kwa mtindo wa saa kumi na mbili ni hatua muhimu katika kujijengea uelewa wa dhana ya wakati. Kwa kutumia mbinu za vitendo, mifano halisi na masuali ya viwango tofauti, utajifunza kwa urahisi na kwa kujiamini.
Kuchora nyuso za saa (za akrabu na tarakimu)
Kuchora nyuso za saa (za akrabu na tarakimu)
Baada ya somo uweze:
  • Kuchora uso wa saa kwa usahihi.
  • Kutambua na kuandika tarakimu za saa kuanzia 1 hadi 12.
  • Kuchora na kutaja mshale (mshale mmkubwa na mshale mdogo).
Utangulizi.
Umejifunza maana ya saa kwa ujumla. Sasa unaweza kusoma saa. Saa ya Mshale na saa ya kidigitali. Jee!
  • “Unajuaje muda wa kwenda skuli?”
  • “Unajuaje muda wa kula na muda wa kulala?”
Unajua kwa kungalia uso wa saa unaeleza nini? Ikiwa saa ya mshale au saa ya kidigitali.
Saa hutengenezwa kwa maumbo mbalimbali, kuna saa za duara, pembe nne na hata pembe tatu. Umbo la saa halizuii kuweza kuisoma saa hiyo. Sasa onesha uwezo wako wa kuchora nyuso mbalimbali za saa.
Example 45
Mfano wa saa za pembe nne na pembetatu.
Nini Utajifunza Kwa Ufupi
Katika somo hili, utajifunza:
  • Sehemu za saa (uso wa saa, tarakimu, mshale).
  • Jinsi ya kuchora uso wa saa kwa usahihi.
Maelezo.
Saa ni kifaa kinachotusaidia kujua muda. Tunatumia saa kujua muda wa kuamka, kwenda skuli, kucheza, kula na kulala. Ili uweze kuchora saa nzuri ni lazima ujuwe vitu vinavyoonekana katika uso wa saa.
Saa (Mshale) ina:
  1. Uso wa saa – huu mara nyingi ni mviringo kama duara. ( zipo za maumbo mengine)
  2. Tarakimu – nambari kuanzia 1 hadi 12.
  3. Mishale –Mshale mkubwa (huonyesha dakika), Mshale mdogo (huonyesha saa)
Unaweza kuona saa ya Mshale darasani, nyumbani au kwa wazazi wako.
Example 46
Mfano wa uso wa saa ya mshale.
Saa (Digitali) ina:
  1. Uso wa saa – huu mara nyingi ni mviringo kama duara. ( zipo za maumbo mengine).
  2. Tarakimu – nambariri kuanzia 1 hadi 12.Tarakimu za Mwanzo. (huonyesha saa), Tarakimu za Mwisho. (huonyesha dakika)
Unaweza kuona saa ya kidigitali darasani, nyumbani au kwenye simu za wazazi wako.
Example 47
Mfano wa uso wa saa ya kidigitali.
Mzunguko wa namba 1 mpaka 12.
Vipengele vya Kuchora:
1. Duara: Chora duara kamili (unaweza kutumia mfuniko wa kopo au kibati).
2. Namba: Pangilia namba 12, , 3, 6 na 9 kwanza ili kupata uwiano mzuri, kisha jaza namba nyingine.
Mishale: Mshale mfupi: Huonyesha saa (Hours).
Mshale mrefu: Huonyesha dakika (Minutes).
Kufumbua mafumbo ya saa
Kufumbua mafumbo ya saa
Utangulizi.
Umejifunza saa za aina mbili, na umeona saa zenye maumbo mbalimbali. Jee unaweza kuniambia:
  • “Saa hii inaonyesha muda gani?”
  • “Ni saa ngapi huwa unakwenda skuli?”
Sawa. Hebu niambie vipi unaweza kufumbua mafumbo ya saa, yaani kusoma muda unaoonyeshwa na saa katika mafumbo.
Nini Utajifunza kwa Ufupi.
Katika mada hii, utajifunza:
  • Maana ya mafumbo ya saa.
  • Jinsi ya kusoma muda kamili kwenye saa.
  • Kutaja muda kwa maneno rahisi.
Maelezo.
Mafumbo ya saa ni kazi za kufikiri zinazokusaidia kujua muda sahihi unaoonyeshwa na saa. Kumbuka!. Saa ina mishale miwili:
  • Mshale mdogo huonyesha saa.
  • Mshale mmkubwa huonyesha dakika.
Kwa sasa, tunazingatia saa kamili na nusu saa, ambapo mshale mkubwa husimama kwenye nambari 12, kwa saa kamili.
Example 48
Mfano:
  • Mshale mdogo ikisimama kwenye 3 na mshale mkubwa kwenye 12, muda ni saa tatu kamili. Unaweza kutumia ujuzi huu kujua muda wa:
  • Kwenda skuli
  • Kula chakula
  • Kulala
Kwa nusu saa, ambapo mshale mkubwa husimama kwenye nambari 6, kuonesha ni nusu ya saa kamili. Mshale mdogo husimama baina ya nambari mbili zinazofatana.
Listening to this topic