Hisabati

MAUMBO
♿ Accessibility: | | | |

MAUMBO

Maumbo bapa
Dhana ya Maumbo Bapa
Umahiri Unaotarajiwa
Baada ya kumaliza mada hii utaweza kuchunguza vitu vilivyo katika mazingira yako na kufikiri kimantiki kwa kulinganisha maumbo mbalimbali, kisha kuwasiliana kwa kutaja na kueleza maumbo uliyoyaona ili uweze kutambua maumbo bapa katika mazingira halisi na kuyahusisha na vitu vinavyokuzunguka. Aidha, utaweza kueleza kwa maneno rahisi umbo la kitu chochote kile, na hatimaye utaweza kuchora na kutaja maumbo bapa kwa usahihi kulingana na uelewa ulioupata
Kuanisha maumbo bapa
Kuanisha maumbo bapa
Utangulizi.
Angalia vitu vilivyoopo hapa mbele: (sahani, kifuniko cha chupa, kitabu, sanduku, picha).
  • “Hiki kitu kinafanana na nini?”
  • “Je, hiki ni cha mviringo au cha pembe?”
Shika, na sema ulichokiona.
Hayo yote ni maumbo ila sio maumbo bapa.
“Maumbo bapa ni maumbo tunayoweza kuyachora kwenye karatasi. Hayana unene.”
Kama:
  • Duara
  • Mraba
  • Mstatili
  • Pembetatu
“Yepi yanafanana kwa rangi?”
“Yepi yanafanana kwa pembe?”
“Yepi yanafanana kwa umbo?”
“Jee haya ni maumbo gani?”
“Haya hapa maumbo yanayofanana yapo pamoja.”
“Jee maumbo haya yanayofanana na kitu gani?”
“Katika maumbo haya yanayofanana. Taja sifa mbili ulizozigundua”
“Taja vitu mbalimbali vinavyofanana na maumbo hayo”
  • Vilivyopo skuli na
  • Vilivyopo nyumbani.
Hayo ni maumbo mraba.
“Jee haya ni maumbo gani?”
“Haya hapa juu ni maumbo yanayofanana yapo pamoja.”
“Jee maumbo haya yanafanana kwa kitu gani? ”
“Taja vitu mbalimbali vinavyofanana na maumbo hayo?”
  • Vilivyopo skuli na
  • Vilivyopo nyumbani.
“Jee maumbo haya yanayofanana kwa kitu gani? ”
  • Vilivyopo skuli na
  • Vilivyopo nyumbani.
Hayo ni maumbo ya Duara.
“Jee maumbo haya yanayofanana kwa kitu gani?”
  • Vilivyopo skuli na
  • Vilivyopo nyumbani.
Hayo ni maumbo ya Pembetatu.
Maelezo.
Maumbo bapa ni maumbo ya Hisabati ambayo hayana unene.
Ni maumbo yanayoonekana yakiwa yamelala juu ya uso wa tambarare kama karatasi, ubao au sakafu. Maumbo haya yako kila mahali katika maisha yako.
Maumbo bapa ni maumbo tunayoweza kuyachora kwenye karatasi na kuyaona kwa macho, lakini hatuwezi kuyashika kwa unene.
Maumbo bapa yana urefu na upana tu, hayana kina wala unene.
Mifano ya maumbo bapa
  • Duara – mfano: sahani, mpira wa karatasi
  • Mraba – mfano: kigae cha sakafuni
  • Mstatili – mfano: mlango, kitabu
  • Pembetatu – mfano: paa la nyumba
Jibu maswali yafuatayo.
  • “Je, umewahi kuona sahani nyumbani. Inafanana na umbo gani?”
  • “Ubao wa darasani una umbo gani?”
  • “Mlango wa darasa una umbo gani?”
Mfano halisi:
Ukichora duara kwenye karatasi, hilo ni umbo bapa, lakini mpira wa kuchezea si umbo bapa kwa sababu una unene.
Kwa ufupi:
Maumbo bapa ni maumbo yasiyo na unene kama duara, mraba, mstatili na pembetatu.
Utajifunza Nini kwa Ufupi.
Katika mada hii, utajifunza:
  • Maana ya maumbo bapa.
  • Aina za maumbo bapa kama vile duara, mraba, mstatili na pembetatu.
  • Mifano ya maumbo bapa katika maisha ya kila siku.
Mifano.
  1. Sahani ya chakula ina umbo la duara.
  2. Ubao wa darasani una umbo la mstatili.
  3. Kigae cha sakafuni kina umbo la mraba.
Mazoezi kwa mwanafunzi
Kupanga maumbo bapa
Kupanga maumbo bapa
Utangulizi.
Unavijua vitu hivi.
  • Sahani
  • Kitabu
  • Kigae cha sakafuni
  • Alama ya pembetatu
Jee:
  • “Vitu hivi vinafanana kwa kitu gani?”
  • “Tunaweza kuviweka pamoja kulingana na maumbo yao?”
“Unajua”:
“Leo tutajifunza kupanga maumbo bapa.”
Utajifunza Nini kwa Ufupi.
tuweke nafasi (space) baina ya neno "mwanafunzi" na "atajifunza"
Katika mada hii, mwanafunziatajifunza:
  • Kupanga maumbo bapa yanayofanana
  • Kupanga maumbo kwa kuzingatia idadi ya pande
  • Kupanga maumbo kwa kutumia rangi, ukubwa au aina
tuweke nafasi kati ya maneno
Maelezo.
Kupanga maumbo bapa ni kitendo cha:
  • Kuweka maumbo yanayofanana pamoja
  • Kutenganisha maumbo yasiyofanana
Panga maumbo kama unavyopanga:
  • Viatu
  • Vifaa vya kuchezea
  • Kalamu za rangi
Mifano ya Upangaji:
  • Duara zote pamoja
  • Maumbo yenye pande tatu pamoja
  • Maumbo yenye pande nne pamoja
Maumbo bapa yanayotumika:
  • Duara
  • Mraba
  • Mstatili
  • Pembetatu
Mifano.
  1. Kupanga sahani zote pamoja kwa sababu ni duara.
  2. Kuweka milango na vitabu pamoja kwa sababu ni mstatili.
  3. Kupanga maumbo yenye pande tatu pamoja (pembetatu).
HITIMISHO.
“Leo tumejifunza kupanga maumbo bapa!”
Tunapanga:
  • Duara pamoja
  • Mraba pamoja
  • Pembetatu pamoja
Kuhusisha dhana ya maumbo bapa katika mazingira halisi
Kuhusisha dhana ya maumbo bapa katika mazingira halisi
Utangulizi.
Jee!
  • “Umeona umbo la dirisha nyumbani?”
  • “Sahani tunayotumia kula ina umbo gani?”
  • “Ubao wa darasani una umbo gani?”
Vitu vingi vinavyokuzunguka vina maumbo bapa, leo utajifunza kuyatambua na kuyaona katika mazingira yako ya kawaida.
Matokeo Mahsusi ya Ujifunzaji
Uweze:
  • Kutaja maumbo bapa (mstatili, mraba, duara, pembetatu)
  • Kutambua maumbo bapa kwenye vitu halisi vya mazingira yake
  • Kulinganisha maumbo bapa kulingana na muonekano wake
Utajifunza Nini kwa Ufupi.
Katika mada hii, utajifunza:
  • Maana ya maumbo bapa
  • Aina za maumbo bapa
  • Mahali maumbo bapa yanapopatikana katika maisha ya kila siku
Maelezo.
Maumbo bapa ni maumbo ambayo hayana unene, yana urefu na upana tu. Maumbo haya tunaweza kuyaona kwa macho na kuyagusa kwenye vitu vingi vinavyotuzunguka.
Kwa mfano:
  • Duara linaonekana kwenye sahani, saa ya ukutani na matairi
  • Mraba unaonekana kwenye vigae vya sakafuni na madirisha
  • Mstatili unaonekana kwenye mlango, ubao wa darasani na vitabu
  • Pembetatu unaonekana kwenye paa la nyumba na alama za barabarani
Maumbo yote hayo uso wake wa juu ni bapa.
Mifano.
  1. Duara – Sahani ya chakula
  2. Mraba – Kigae cha sakafuni
  3. Mstatili – Mlango wa darasa
  4. Pembetatu - Sambusa
Maumbo bapa (Mstatili, Mraba, Pembe Tatu na Duara)
Kuhusisha vitu vyenye mfanano na maumbo bapa
Kuhusisha vitu vyenye mfanano na maumbo bapa
Utangulizi.
Umejifunza dhana ya maumbo bapa. Unayakumbuka maumbo bapa yoyote uliyojifunza? Taja maumbo hayo. Ndio, Mstatili, mraba, pembetatu na duara.
Sasa jibu masuali yafuatayo:
  1. “Je, umeona mlango wa darasa una umbo gani?”
  2. “Unaweza kupata umbo bapa kwenye mlango wa darasa?”
  3. “Umbo bapa hilo linaitwaje?”
  4. “Sahani tunayotumia kutilia chakula ina umbo gani?”
  5. “Ubao wa darasani una umbo gani?”
Ndio, umejifunza maumbo bapa ya aina mbalimbali.
Jee unaweza kutaja vitu vyenye mfanano na maumbo bapa uliyojifunza?
Taja vitu vyenye umbo bapa vilivyoopo:
  • Darasani.
  • Nyumbani.
Umahiri Unaotarajiwa.
Baada ya somo hili, mwanafunzi ataweza kutambua na kulinganisha maumbo bapa na vitu vya mazingira yake, kuchora maumbo hayo kwa usahihi na kujiamini, pamoja na kutumia vifaa rahisi kuyatengeneza ili kuimarisha stadi za mikono na uelewa wa kijiometri.
Matokeo Mahsusi ya Ujifunzaji.
Mwanafunzi aweze:
  • Kutambua mstatili, mraba, pembetatu na duara
  • Kuhusisha maumbo hayo na vitu vya nyumbani, shuleni na mtaani.
  • Kueleza kwa maneno rahisi umbo la kitu.
Utajifunza Nini kwa Ufupi
Katika mada hii, utajifunza:
  • Maana ya maumbo bapa.
  • Aina nne za maumbo bapa.
  • Mfanano kati ya maumbo bapa na vitu halisi.
Maelezo:
Maumbo bapa ni maumbo yasiyo na unene. Yana urefu na upana tu. Maumbo haya tunaweza kuyaona kwa urahisi kwenye vitu vingi vinavyotuzunguka.
Aina za Maumbo Bapa
  1. Mstatili- Hili ni umbo lenye pande nne. Pande mbili ni ndefu na pande mbili ni fupi.Mfano wa mazingira: mlango wa darasa, ubao wa darasani, kitabu.
  2. Mraba- Huu ni umbo lenye pande nne zinazolingana kwa urefu.Mfano wa mazingira: kigae cha sakafuni, dirisha dogo.
  3. Pembetatu- Huu ni umbo lenye pande tatu.Mfano wa mazingira: paa la nyumba, bendera.
  4. Duara- Huu ni umbo la mviringo lisilo na pembe.Mfano wa mazingira: sahani, saa ya ukutani, mpira. Kwa kutumia mifano ya mazingira halisi, mtoto anaelewa kwa urahisi na anaweza kukumbuka maumbo kwa muda mrefu.
Mifano.
  1. Sahani – Duara
  2. Mlango – Mstatili
  3. Kigae cha sakafuni – Mraba
Kuchora aina za maumbo bapa
Kuchora aina za maumbo bapa
Utangulizi.
Katika somo lililopita, umeona, umeshika, umejibu masuali mbalimbali kuhusu maumbo bapa. Sasa angalia vitu mbalimbali vilivyomo katika darasa na vilivyochorwa vyenye maumbo bapa.
“Ni nani anaweza kunionesha umbo la sahani?”
“Ubao wa darasani una umbo gani?”
“Je, tunaweza kuchora maumbo haya kwenye daftari?”
Matokeo Mahsusi ya Ujifunzaji
badilisha neno "mtoto" na uweke "mwanafunzi"
Mtoto aweze:
  • Kuchora mstatili, mraba, pembetatu na duara
  • Kutaja jina la kila umbo analochora
  • Kuhusisha mchoro na vitu halisi vya mazingira yake
Utajifunza Nini kwa Ufupi
Katika mada hii, mtoto utajifunza:
  • Jinsi ya kushika penseli vizuri
  • Hatua za kuchora kila umbo bapa
  • Kuchora maumbo bapa kwa nadhifu
Maelezo.
(a) Kuchora Mstatili
Mstatili una pande nne; pande mbili ni ndefu na mbili ni fupi.Unaweza kuchora mstari mrefu juu, mstari mfupi pembeni, mstari mrefu chini, na mstari mfupi pembe ya pili.
Hili ni umbo la mstatili.
Jee unaweza kulichora?
Mfano katika mazingira: Mlango, ubao wa darasa, kitabu.
(b) Kuchora Mraba
Mraba una pande nne zote sawa.Unaweza kuchora mistari minne iliyo sawa kwa urefu na upana.
Mfano katika mazingira: kigae cha sakafuni cha “60x60” au “40x40”, dirisha dogo.
Hili ni umbo la Mraba.
(c) Kuchora Pembetatu
Pembetatu ina pande tatu.Uanza kwa kuchora mstari wa chini, kisha mistari miwili ikikutana juu.
Mfano katika mazingira: Paa la nyumba, Sambusa.
Hili ni umbo la Pembetatu.
(d) Kuchora Duara
Duara ni umbo la mviringo lisilo na pembe.Unaweza kuchora mstari wa mviringo bila kukatika.
Hili ni umbo la Duara
Mfano katika mazingira: Sahani, saa, mpira.
Mifano.
  1. Duara – sahani ya chakula
  2. Mstatili – mlango wa darasa
  3. Pembetatu – paa la nyumba
Kutengeneza vitu mbali mbali vyenye maumbo bapa
Kutengeneza vitu mbali mbali vyenye maumbo bapa
Utangulizi.
Angalia vitu hivi: karatasi, makopo matupu, vifuniko vya chupa, udongo au plastiki.
Jibu maswali:
  • “Unaweza kutengeneza vitu gani kwa kutumia maumbo bapa?”
  • Unaweza kukata maumbo mbalimbali kutokana na kitu kinachohitajika?
  • “Unaweza kutengeneza umbo la mraba kwa karatasi?”
  • “Je, tujaribu kutengeneza maumbo kwa mkono wako?”
Matokeo Mahsusi ya Ujifunzaji.
Mtoto aweze:
  • Kutengeneza umbo la mstatili, mraba, pembetatu na duara.
  • Kuhusisha umbo alilotengeneza na kitu halisi.
  • Kueleza kwa maneno rahisi alichotengeneza.
Utajifunza Nini kwa Ufupi.
Katika mada hii, utajifunza:
  • Jinsi ya kutumia karatasi, udongo au vifaa vya kawaida
  • Kutengeneza maumbo bapa kwa vitendo
  • Kujifunza kwa kufanya (learning by doing)
Maelezo.
Kutengeneza maumbo bapa hukusaidia kuelewa maumbo kwa vitendo badala ya kusikia tu. Kutumia vifaa vinavyopatikana kwa urahisi nyumbani au shuleni.
(a) Kutengeneza Mraba
Kata karatasi au tumia vijiti kutengeneza umbo lenye pande nne sawa.
Mfano wa mazingira: kigae cha sakafuni, kisanduku kidogo.
Kumbuka. Uso wa juu wa umbo ndio bapa, kwani umbo bapa halina unene
(b) Kutengeneza Mstatili
Tumia karatasi kukata umbo lenye pande nne, mbili ndefu na mbili fupi.
Mfano wa mazingira: mlango, kitabu.
(c) Kutengeneza Pembetatu
Pinda karatasi au tumia vijiti vitatu kutengeneza umbo la pembetatu.
Mfano wa mazingira: paa la nyumba.
Kumbuka. Uso wa juu wa umbo ndio bapa, kwani umbo bapa halina unene.
(d) Kutengeneza Duara
Mtoto atumie kifuniko cha chupa au akande udongo kwa umbo la mviringo.
Mfano wa mazingira: sahani, saa.
Endele kufanya mazoezi ya kuchora maumbo uliyojifunza. Mazoezi hukujengea ujasiri, ubunifu na uelewa wa kina wa maumbo bapa.
Mifano 3.
  1. Duara – kifuniko cha chupa kilichotumiwa kama mfano.
  2. Mraba – umbo la karatasi lililokatwa.
  3. Pembetatu – umbo lililotengenezwa kwa vijiti.
  4. Kutengeneza nyumba kwa maumbo bapa.
  • Umeona nini?
  • Tengeneza na wewe kama hiyo.
Listening to this topic