Hisabati

SEHEMU
♿ Accessibility: | | | |

SEHEMU

Utangulizi
Katika mada hii, mwanafunzi utajifunza kuhusu sehemu. Kupitia dhana ya sehemu, utaweza kuelewa kugawanya kitu kimoja katika sehemu sawa. Kupitia Muundo wa Sehemu pia utaweza kujifunza jinsi sehemu zinavyoonekana kwa kutumia picha na maumbo.
Dhana ya Sehemu
Sehemu ni kipande au kiasi kinachowakilisha kipande au mivunjiko ya kitu kizima kilichogawanywa katika vipande sawa.
Kitu kizima kikigawanywa katika sehemu sawa, kila kipande kinaitwa sehemu.
Kuelezea dhana ya sehemu kwa kutumia maumbo
Kuelezea dhana ya sehemu kwa kutumia maumbo
sehem. nusu na robo.
Example 25
Mifano ya Sehemu
Kila kipande chenye rangi katika michoro ifuatayo ni sehemu ya kitu kizima.
Kila kipande katika picha hii ni sehemu ya kitu kizima
Kubainisha sehemu kwa kutumia vitu halisi
Kubainisha sehemu kwa kutumia vitu halisi
kutoka katika picha ya hapo juu tunaweza kuona Sehemu za vitu mabali mbali:
  1. Ndizi: Ndizi moja ikigawanywa vipande viwili sawa, kila kipande ni sehemu ya ndizi.
  2. Andazi: Andazi likigawanywa vipande viwili sawa, kila kipande ni sehemu ya andazi.
  3. Fenesi: Fenesi moja likikatwa nusu mbili sawa, kila nusu ni sehemu ya fenesi.
  4. Karatasi: Karatasi moja ikikatwa vipande viwili sawa, kila sehemu ni sehemu ya karatasi.
  5. Nanasi: Nanasi likikatwa vipande sawa, kila kipande ni sehemu ya nanasi.
Katika picha zifuatazo kila kipande ni sehemu ya kitu kizima
Kutafautisha sehemu kwa kutumia vitu tafauti
Kutafautisha sehemu kwa kutumia vitu tafauti
kwa kuangalia picha zifuatazo tunaweza kujifunza kutofautisha sehemu za vitu tafauti. Upande wa kushoto unaonesha kitu kizima na upande wa kulia unaonesha sehehemu za kitu kizima.
Muundo wa sehemu
Kubainisha muundo wa sehemu
Kubainisha muundo wa sehemu
Muundo wa Seheme huandikwa kwa kutumia namba mbili zilizotenganishwa na mstari wa mlalo au mshazari:
Kiasi cha Juu: Huonyesha ni vipande vingapi unavyozungumzia. Hii ni sehemu zilizochukuliwa.
Kiasi cha Chini: Huonyesha jumla ya vipande vyote sawa vilivyounda kitu kile kizima.
Angalizo: Asili inaelezea kitu kinachogawanywa au kitu kizima.
Asili ya sehemu huandikwa chini ya mstari wa kugawa
Kiasi kinaelezea idadi ya sehemu zilizochukuliwa kutoka kwenye kitu kizima
Kiasi ya sehemu huandikwa juu ya mstari wa kugawa
Katika Maumbo yafuatayo sehemu zilizotiwa rangi ni kiasi, na idadi ya sehemu zilizogawanywa ni asili
Katika Maumbo yafuatayosehemu zilizotiwa rangi ni kiasi, na idadi ya sehemu zilizogawanywa ni asili
Exercise 6
Kwa kutumi maumbo yafuatayo, pigia duara sehemu sahihi
Exercise 7
Kwa kutumia maumbo yafuatayo, andika asili na kiasi kwenye vijumba mbele ya kila umbo.
Kusoma sehemu 1/2, 1/3, 1/4, 1/5,1/6 na 1/8 kwa kutumia michoro na tarakimu
Kusoma sehemu 1/2, 1/3, 1/4, 1/5,1/6 na 1/8 kwa kutumia michoro na tarakimu
Activity 5
Soma kwa uangalifu sehemu zifuatazo
Soma sehemu hizi
Kuandika sehemu 1/2, 1/3, 1/4, 1/5,1/6 na 1/8 kwa kutumia michoro na tarakimu
Kuandika sehemu 1/2, 1/3, 1/4, 1/5,1/6 na 1/8 kwa kutumia michoro na tarakimu
Andika ya sehemu hizi:
Activity 6
Soma kwa uangalifu, jinsi ya kuandika sehemu kwa kutumia tarakimu kwa kulinganisha michoro
Example 26
Picha zifuatazo zinaonesha jinsi ya kuandika sehemu
Exercise 8
Paka rangi maumbo yafuatayo ili yaendani na sehemu uliyopewa
Exercise 9
Kwa kutumia maumbo yafuatayo oanisha kwa usahihi mchoro na tarakimu za sehemu kwa kupiga mstari kutoka kwenye mchoro mpaka kwenye tarakimu sahihi ya sehemu
nambari zipo hafifu (faint)
Listening to this topic