Hisabati

VIPIMO
♿ Accessibility: | | | |

VIPIMO

Vipimo vya asili vya urefu (Nyanda, dhiraa, pima na hatua)
Utangulizi
Katika maisha yetu ya kila siku, tunatumia vipimo kuelewa ukubwa, urefu, au uzito wa vitu vinavyotuzunguka. Kwa mwanafunzi wa Darasa la Kwanza, somo hili linamsaidia kuanza kulinganisha vitu kwa macho na vitendo kabla ya kutumia zana rasmi.
Matokeo Mahususi:
Kubainisha vipimo vya asili vya urefu
Kubainisha vipimo vya asili vya urefu
Vipimo vya asili vya ujazo.
Vipimo vya asili vya urefu ni njia rahisi za kupima urefu kwa kutumia mwili wa binadamu.Mfano, mtoto anaweza kupima kwa kutumia kiganja cha mkono (nyanda), mkono (ziraa), hatua za miguu au pima.Picha zifuatazo zinaonesha vipimo vya asili vya urefu:
Swali la Utambuzi:
Taja sehemu mbili za mwili wa binadamu ambazo tunaweza kuzitumia kama vipimo vya asili vya urefu
Kulinganisha vipimo vya asili vya urefu
Kulinganisha vipimo vya asili vya urefu
Vipimo vya asili hutofautiana kulingana na ukubwa wa kitu kinachopimwa. Kila kipimo kina matumizi yake maalum na husaidia kutofautisha kati ya vitu vidogo na vikubwa. Angalia aina ya kipimo na maelezo husika:
  • Pima ni kubwa Zaidi. Hupima urefu mkubwa kama mkeka, kamba.
  • Hatua ni kubwa kuliko ziraa. Hupima vitu virefu kidogo kama darasa.
  • Ziraa ni kubwa kuliko nyanda. Hupima vitu vya kati kama deksi au mlango.
  • Nyanda ni ndogo Zaidi. Hupima vitu vidogo kama kitabu, meza ndogo.
Kupima urefu kwa kutumia vipimo vya asili
Kupima urefu kwa kutumia vipimo vya asili
Jifunze kupima urefu kwa kutumia vipimo vya asili kwa kutumia picha zifuatazo:
Zoezi la kulinganisha:
Baina ya kiganja cha mkono (nyanda) na mkono (ziraa), ni kipimo kipi ambacho ni kirefu zaidi ya kingine? Eleza kwa nini.
Vipimo vya Asili vya Ujazo
Utangulizi
Vipimo vya asili vya ujazo ni vipimo vya kupima kiasi cha vitu hasa vimiminika au punje kwa kutumia vyombo vya kawaida vya mazingira yetu.
Mifano ya vipimo vya asili vya ujazo
  • Kopo – hupimia kiasi kidogo ( maharage, mafuta)
  • Ndoo – hupimia maji au mchanga
  • Beseni – hupimia maji mengi au nafaka
  • Pipa – hupimia kiasi kikubwa cha maji aumafuta
  • Gunia – hupimia nafaka au mazao
  • Kibaba – hupimia nafaka (kama mahindi, mchele)
  • Pishi – hupimia mazao au nafaka (kama karafuu, mchele, mtama)
Matokeo mahususi:
Kubainisha vipimo vya asili vya ujazo
Kubainisha vipimo vya asili vya ujazo
Picha zifuatazo ni vipimo vya asili vya ujazo:
Kulinganisha vipimo vya asili vya ujazo
Kulinganisha vipimo vya asili vya ujazo
Chunguza jozi za vipimo vifuatavyo. Andika kipimo chenye ujazo mkubwas katika kila jozi.
Kupima ujazo kwa kutumia vipimo vya asili
Kupima ujazo kwa kutumia vipimo vya asili
Vipimo vya asili vinaweza kutumika kupimia ujazo endapo Vipimo vya kisasa vitakosekana. Angalia picha mbalimbali zinazoonesha Vipimo vya asili na ujibu maswali yanayofuata.
Mazoezi:
  1. Swali la Utambuzi wa Zana: Taja vyombo vitatu vya nyumbani unavyoweza kuvitumia kupima ujazo wa maji au maziwa kwa kutumia njia ya asili.
  2. Swali la Kulinganisha Ujazo: Ikiwa unataka kujaza maji kwenye ndoo kubwa, je, utatumia vikombe vingi zaidi au kijiko kimoja?
  3. Swali la Vitendo na Makadirio: Chukua kiganja chako cha mkono na ukijaze mchanga, kisha uumwage kwenye kikombe. Je, unahitaji viganja mingapi ili kikombe hicho kijae kabisa?
  4. Mama anataka kumpa mtoto mdogo dawa ya maji. Je, ni kipimo kipi cha asili kilicho sahihi zaidi kutumika kati ya kijiko na bakuli kubwa?
Listening to this topic