Kiswahili Darasa la III Syllabus

    1. Kutumia msamiati katika kusoma na kuchanganua mawazo yaliyo wasilishwa katika matini mbalimbali
      1. Kusoma sentensi na kubaini maneno yanayoonesha umiliki na kubadili sentensi hizo kuwa katika kinyume
      2. Kusoma sentensi na kubaini maneno ya ulinganishi wa vitu na watu (kama, sawa na, kama vile, sawasawa) ili kujenga dhana ya ulinganishi
      3. Kusoma kifungu cha habari na kubaini majina ya miti
      4. Kusoma na kubaini majina ya wanyama wanaokula majani na kueleza sifa na faida zao
      5. Kusoma na kubaini majina ya wanyama wanaokula nyama na kuelezea sifa na faida zao katika jamii
    2. Kusoma kwa ufasaha na kuonesha uelewa wa matini mbalimbali
      1. Kusoma kimya kifungu cha habari na kujibu maswali
      2. Kusoma ili kubaini mawazo makuu kutoka katika habari teule
      3. Kubaini taarifa mahususi za kila siku kutoka katika majarida, matangazo na ratiba mbalimbali na kufanya ufupisho wake
      4. Kubaini wahusika katika kifungu cha habari na kuwatolea ufafanuzi
      5. Kubaini miundo kutoka katika kifungu cha habari kinachohusu watoto wanaoishi katika mazigira magumu
      6. Kusoma ngonjera kwa sauti ya kutamba na kubaini maudhui yake
      7. Kusoma tenzi kwa sauti ya kishairi na kubaini ujumbe wake
      8. Kusoma mashairi kwa sauti ya kishairi na kubainisha mawazo makuu yaliyojitokeza
    3. Kusikiliza na kuonesha uelewa wa jambo alilolisikiliza
      1. Kuchambua kauli taarifa kwa kubainisha nafsi na nyakati za utendaji
      2. Kuchambua kauli halisi kwa kubainisha nafsi na nyakati za utendaji
      3. Kubaini maudhui yaliyomo katika igizo dhima na kuchambua hoja kuu zilizojitokeza
      4. Kutegua vitendawili na kuonesha umuhimu wake katika jamii