Sayansi Darasa la III Syllabus

    1. Kufanya majaribio ya kisayansi kwa usahihi
      1. Kufanya majaribio kuchunguza mwali wa mwanga unavyopinda ukitua katika lenzi
      2. Kufanya vitendo vya kuzalisha umeme kwa kutumia dainamo na seli
      3. Kutumia vipimo rasmi katika jaribio la kisayansi
      4. Kufanya majaribio kuchunguza nishati ya mwanga inapotua katika kioo mbinuko na mbonyeo
      5. Kufanya majaribio kuhusu nishati jadidifu
      6. Kutumia vipimo visivyo rasmi
      7. Kueleza dhana ya vipimo katika kufanya majaribio ya kisayansi
      8. Kufanya majaribio kuhusu nishati ya umeme
      9. Kufanya majaribio kupima joto la maji na joto la mwili wa binadamu
    2. Kumudu stadi za kisayansi
      1. Kufanya vitendo vya kutumia mashine rahisi
      2. Kufanya vitendo vya kutunza vifaa vya kurahisisha kazi
      3. Kukokotoa kiasi cha kazi
      4. Kueleza dhana ya kazi
      5. Kufahamu vifaa vya kurahisisha kazi
      6. Kufanya vitendo vya kuonesha jitihada, mzigo na egemeo katika wenzo
      7. Kubaini mashine rahisi
      8. Kubaini vifaa vya kurahisisha kazi
      9. Kukokotoa thamani ya mzigo, jitihada katika roda
      10. Kubaini mashine sahili za roda (gurudumu kapi)
    3. Kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      1. Kueleza namna ya kutumia simu katika kujifunza
      2. Kufanya vitendo vya kucheza michezo katika kompyuta (gemu) mbalimbali zinazokuza stadi za (KKK)
      3. Kutumia simu na kompyuta kutafuta taarifa za kisayansi
      4. Kufanya vitendo vya kutumia injini pekuzi kutafuta taarifa za kisayansi na kiteknolojia
      5. Kufanya vitendo vya kutumia kompyuta (programu andishi)
      6. Kutumia simu
      7. Kueleza dhana ya mawasiliano
      8. Kueleza tahadhari za kuzingatia wakati wa kutumia kompyuta
      9. Kufanya vitendo vya kutumia barua pepe
      10. Kueleza dhana ya barua pepe
      11. Kueleza dhana ya kompyuta
      12. Kueleza athari za mtandao wa intaneti
      13. Kueleza dhana ya usalama wa mtandao wa intaneti
      14. Kufanya vitendo vya kutumia programu jedwali
    1. Kutambua nadharia za kisayansi na kiteknolojia
      1. Kufanya vitendo vya kudhihirisha muundo wa maada katika uyeyushaji mweneo (osmosis)
      2. Kutengeneza modeli/kifani kinachoweza kupaa na kuelea katika hewa
      3. Kutofautisha dhana ya badiliko la kiumbo na badiliko la kikemikali katika maada
      4. Kufanya vitendo kuhusu kani zinavyo sababisha mabadiliko katika maada
      5. Kufanya vitendo vya kudhihirisha muundo wa maada katika uyeyushaji mweneo (difyusion)
      6. Kutengeneza modeli/kifani kinachoweza kuelea katika maji
      7. Kueleza kani zinazosababisha mabadiliko katika maada
      8. Kufanya majaribio ya badiliko la kiumbo na kikemikali
      9. Kufanya vitendo vya kubaini sifa za maada
      10. Kueleza dhana ya maada
    2. Kutambua aina anuai za nishati na matumizi yake
      1. Kueleza dhana ya mashine tata
      2. Kueleza matumizi ya nishati ya sauti, joto na mwanga
      3. Kufanya jaribio kuhusu tabia ya mwanga unapotua katika kioo bapa
      4. Kueleza namna mbalimbali ya kuzalisha nishati ya umeme
      5. Kufanya vitendo vya kubaini kanuni za sumaku
      6. Kufanya vitendo vya kuchunguza jinsi sauti, joto, na mwanga unavyosafiri
      7. Kueleza dhana ya nishati
      8. Kufafanua dhana ya nishati jadidifu
      9. Kufanya majaribio kuhusu sakiti mfuatano na sakiti sambamba
      10. Kueleza dhana ya kukinga sakiti na majengo dhidi ya umeme mkubwa
      11. Kufanya majaribio ya kuonesha matumizi ya lenzi mbonyeo na lenzi mbinuko
      12. Kufanya vitendo vya kuthibitisha kanuni ya Ohm katika mkondo wa umeme
    3. Kuchunguza vitu vilivyopo katika mazingira
      1. Kueleza namna ya kuthamini viumbe hai na vitu katika mazingira
      2. Kufafanua dhana ya kujirekebisha kwa viumbe hai kulingana na mazingira
      3. Kufanya vitendo vya kutunza udongo
      4. Kubaini vitendo vinavyosababisha athari katika udongo
      5. Kueleza kutegemeana kwa vitu na viumbe hai katika mazingira
      6. Kueleza namna ya kuchukua tahadhari za kujikinga na vitu na viumbe hatari au wenye sumu
      7. Kubaini vitu na viumbe hai vilivyopo kwenye mazingira
      8. Kufafanua dhana ya uzazi katika wanyama na mimea
      9. Kutofautisha aina za udongo
      10. Kueleza namna mmea unavyo jitengenezea chakula chake (usanishaji chakula)
      11. Kufanya jaribio la kuthibitisha usanishaji chakula katika mmea
      12. Kubaini mahitaji muhimu katika ukuaji wa mmea
      13. Kufafanua gesi zinazounda hewa