Sayansi Darasa la V Syllabus

    1. Kutambua mifumo mbalimbali ya mwili wa binadamu
      1. Kubaini mitindo inayofaa ya maisha inayoweza kuepusha kasoro katika mfumo wa utoaji taka mwilini
      2. Kuchora mfumo wa mmeng’enyo wa chakula
      3. Kueleza njia za uzazi wa mpango
      4. Kuainisha sehemu za mfumo wa mmeng’enyo wa chakula
      5. Kubaini mitindo ya maisha inayoweza kusababisha kasoro katika mfumo wa utoaji taka mwilini
      6. Kueleza dhana ya balehe kwa msichana na mvulana
      7. Kueleza dhana ya mfumo wa utoaji taka mwilini
      8. Kutofautisha kasoro zinazoweza kutokea katika mfumo wa uzazi wa kike na kiume
      9. Kubaini mfumo wa Uzazi
      10. Kubaini kasoro zinazoweza kutokea katika mfumo wa damu
      11. Kufafanua mfumo wa damu
    2. Kufuata kanuni za afya ili kujenga afya bora
      1. Kuchanganua makundi mbalimbali ya watu wanaohitaji huduma ya afya
      2. Kueleza njia za kujikinga na maambukizi ya VVU
      3. Kueleza njia za maambukizi ya magonjwa ya mlipuko
      4. Kubaini magonjwa ya kurithi
      5. Kueleza dhana ya magonjwa ya mlipuko (chanzo dalili na athari)
      6. Kupanga vyakula vinavyounda mlo kamili
      7. Kueleza athari za VVU na UKIMWI katika familia, jamii na Taifa
      8. Kueleza dhana ya mlo kamili
      9. Kueleza tabia zinazosaidia kutunza afya
      10. Kubaini kanuni za afya
      11. Kueleza uhusiano uliopo kati ya magonjwa ya ngono na virusi vya UKIMWI
      12. Kueleza umuhimu wa usafi na usalama wa lishe kwa mtu anayeishi wa VVU na UKIMWI
    3. Kufuata kanuni za usafi ili kuwa na afya na mazingira bora
      1. Kufanya vitendo vya kutoa huduma ya kwanza kwa aliyevunjika mfupa, aliyeumwa na nyoka, aliyezama kwenye maji na anayetapika au kuharisha
      2. Kutoa huduma ya kwanza kwa mtu aliyeumwa na wadudu hatari au wenye sumu
      3. Kutoa huduma ya kwanza kwa mtu aliyeungua na moto au kimiminika cha moto
      4. Kuainisha vyanzo vya uchafu na taka
      5. Kuangamiza wadudu wanaoeneza magonjwa
      6. Kueleza dhana ya huduma ya kwanza
      7. Kudumisha usafi wa mwili na unadhifu wa mavazi
      8. Kueleza umuhimu wa kudumisha usafi na unadhifu wa mavazi
      9. Kutunza vifaa vya kufanyia usafi wa mwili na mavazi
      10. Kueleza umuhimu wa kufanya usafi wa mwili na mavazi
    1. Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      1. Aina za Antena/Dishi na namna Zinavyotumika
      2. Sifa za Antena na Dishi
    2. Stadi za Kisayansi
      1. Muundo wa Mashine Tata
      2. Taratibu za Kutunza Mashine Tata
    3. Majaribio ya Kisayansi
      1. Namna ya Kuzima Moto
      2. Jaribio la Tabia za Tindikali na Nyongo
      3. Vichocheo vya Kutu, namna ya Kuzuia Kutu