Fasihi ya Kiswahili (New) Form 3 Syllabus

    1. Kuonesha uelewa wa kazi za fasihi ya Kiswahili ya kitaifa
      1. Kufafanua dhana ya fasihi ya Kiswahili ya kitaifa
      2. Kuchambua sifa za fasihi ya Kiswahili ya kitaifa kwenye ‘Wimbo wa Taifa’, wimbo wa ‘Tanzania Tanzania’, wimbo wa ‘Tazama Ramani’ na wimbo wa ‘Mashujaa wa Zanzibar’
      3. Kujadili sifa za fasihi ya kitaifa kwenye fasihi ya watoto
      4. Kubainisha sifa za fasihi ya kitaifa kwenye ngano
      5. Kutunga shairi lenye sifa za fasihi ya kitaifa
    2. Kuhakiki kazi mbalimbali za fasihi ya Kiswahili
      1. Kuhakiki fani na maudhui katika kazi za fasihi ya watoto
      2. Kuhakiki fani na maudhui ya kifasihi katika filamu za Kiswahili
      3. Kuhakiki fani na maudhui katika vichekesho
    1. Kujenga ujumi na falsafa ya Kiafrika katika kazi za fasihi
      1. Kufafanua dhana na vipengele vya ujumi na falsafa ya Kiafrika katika fasihi
      2. Kubainisha ujumi na falsafa ya Kiafrika katika methali za Kiswahili
      3. Kuhakiki tamthiliya zenye ujumi na falsafa ya Kiafrika
    2. Kutumia kazi za fasihi katika kujenga hoja zenye mantiki
      1. Kuchanganua mambo ya kuzingatia wakati wa kujenga hoja kimantiki kutokana na kazi za fasihi
      2. Kuandika insha za kisanaa zenye hoja za kimantiki
      3. Kutumia fasihi kuwasilisha hoja kimantiki katika midahalo
    1. Kutathmini mbinu za kisanaa za utunzi wa kazi za kifasihi
      1. Kufafanua mbinu za kisanaa katika utungaji wa kazi za kifasihi
      2. Kulinganisha matumizi ya mbinu za kisanaa katika kazi mbalimbali za kifasihi
      3. Kujadili mbinu za kisanaa katika ngano
    2. Kutunga kazi sahili za kifasihi
      1. Kufafanua kanuni za utunzi wa mashairi
      2. Kutunga mashairi sahili
      3. Kufafanua kanuni za utunzi wa kazi za fasihi ya watoto
      4. Kutunga kazi sahili za fasihi ya watoto