Historia ya Tanzania na Maadili (New) Form 3 Syllabus

    1. Kumudu historia ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
      1. Kufafanua chimbuko la Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
      2. Kueleza muundo na misingi ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
      3. Kutathimini Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika kujenga umoja na maadili ya Kitaifa
    1. Kuchambua chimbuko la Azimio la Arusha na matokeo yake kiuchumi, kisiasa, kiutamaduni na kimaadili
      1. Kujadili chimbuko la Azimio la Arusha
      2. Kufafanua misingi na mchango wa Azimio la Arusha katika ujenzi wa Taifa kiuchumi, kisiasa, kijamii na kimaadili
      3. Kutathmini changamoto za Azimio la Arusha kiuchumi, kisiasa, kijamii na kimaadili
    2. Kueleza nafasi ya Tanzania katika kujenga uhusiano wa kikanda
      1. Kufafanua dhana ya uhusiano wa kikanda na ujenzi wa Taifa
      2. Kueleza mchango wa Tanzania katika kukuza uhusiano wa kikanda na kujenga utaifa (EAC & SADC)
      3. Kubaini changamoto za uhusiano wa kikanda katika ujenzi wa Taifa
    1. Kumudu misingi ya utafiti wa kihistoria
      1. Kueleza dhana, misingi na maadili ya utafiti wa kihistoria
      2. Kuchambua hatua na mchakato wa utafiti wa kihistoria
    2. Kutumia misingi ya utafiti wa kihistoria kufanya kazi mradi
      1. Kubuni na kufanya kazimradi kuhusu historia ya Tanzania na maadili