Kiswahili
FASIHI SIMULIZI
Reading settings
Text size
Line spacing
Colours
FASIHI SIMULIZI
Utangulizi:
Fasihi simulizi ni sanaa ya lugha inayowasilishwa kwa njia ya mazungumzo, usimulizi, uimbaji au utendaji mbele ya hadhira. Hadhira ni watu wanaosikiliza au kutazama kinachowasilishwa. Fasihi simulizi hutumika kuburudisha, kuelimisha, kuonya na kuhifadhi mila na desturi za jamii.
Mfano 1
Mifano ya fasihi simulizi ni:
Hadithi, Methali, Vitendawili, Nyimbo na mashairi yanayowasilishwa kwa kughani au kuimbwa. Kughani shairi ni kulitamka kwa sauti yenye mpangilio na mahadhi yanayofaa.
Katika mada hii, utasikiliza na kusoma mashairi, kubainisha sifa zake, kufafanua ujumbe wake na kueleza mafunzo yanayopatikana ndani yake.
Mashairi
Kubainisha mashairi
Utangulizi:
Je, umewahi kumsikiliza mtu akighani shairi? Huenda ulisikia maneno yaliyopangwa kwa mahadhi na yenye ujumbe maalumu. Mashairi yanaweza kuzungumzia maisha ya nyumbani, skuli, mazingira na mambo mengine yanayoihusu jamii.
Umahiri
Mwanafunzi aweze kusikiliza au kusoma tungo mbalimbali, kubainisha shairi na kueleza sifa zinazomsaidia kulitambua.
Dhana: Mashairi
Shairi ni utungo wa kisanaa unaotumia lugha iliyoteuliwa na kupangwa kwa namna maalumu ili kuwasilisha mawazo, hisia au ujumbe.
Shairi linaweza kuwasilishwa kwa kughani au kuimbwa. Katika somo hili, tutazingatia mashairi mafupi yanayofaa kusikilizwa, kusomwa na kughaniwa na wanafunzi.
Nini Utajifunza kwa Ufupi
- Maana ya shairi.
- Sifa zinazosaidia kubainisha shairi.
- Maana ya mshororo, ubeti, vina na mizani.
- Kubainisha shairi katika tungo mbalimbali.
Maelezo ya Lengo Mahsusi
Kubainisha shairi ni kulitambua kwa kuzingatia namna lilivyopangwa, lugha iliyotumika na jinsi linavyowasilishwa.
Zingatia vipengele vifuatavyo:
- Mshororo: Mstari mmoja wa shairi.
- Ubeti: Kundi la mishororo katika shairi.
- Vina: Silabi zenye sauti zinazofanana katika sehemu zinazolingana za mishororo, hasa katikati au mwishoni.
- Mizani: Idadi ya silabi katika mshororo au sehemu yake.
- Ujumbe: Jambo ambalo shairi linawasilisha.
- Mahadhi: Mpangilio wa sauti unaojitokeza wakati wa kughani au kuimba shairi.
Mashairi ya kimapokeo huzingatia urari wa vina na mizani. Hata hivyo, si mashairi yote yanayofuata mpangilio huo. Kwa hiyo, usitumie kufanana kwa vina peke yake kuamua kuwa utungo ni shairi.
Ufundishaji na Ujifunzaji
Shughuli 1
Kitendo cha 1: Sikiliza na Ubainishe
Soma kifungu kifupi cha habari, kisha aghani shairi.
Kifungu cha Habari.
Mvua Kubwa
Asubuhi moja, mvua kubwa ilinyesha kijijini kwetu. Maji yalijaa barabarani na baadhi ya njia hazikupitika. Watu walibaki ndani wakisubiri mvua ipungue. Watoto hawakuruhusiwa kucheza karibu na misingi. Baada ya mvua kupungua, wakazi walishirikiana kuondoa taka zilizoziba njia za maji.
Ghani shairi.
Mvua kubwa kijijini, Maji mengi mitaroni,
Watu wote wako ndani, Tusicheze misingini.
Watu wote wako ndani, Tusicheze misingini.
Ikikoma, safisheni, Taka ziwekwe pipani,
Taka zisiwe njiani, Usafi tuuthamini.
Taka zisiwe njiani, Usafi tuuthamini.
- Sikiliza tungo zote mbili.
- Bainisha utungo ambao ni shairi.
- Eleza sifa mbili zilizokusaidia kuutambua.
- Linganisha jibu lako na la mwenzako.
Shughuli 2
Kitendo cha 2: Kadi za Tungo
Fanyeni kazi katika vikundi vidogo.
- Pokeeni kadi zenye hadithi fupi, methali na mashairi.
- Zitenganisheni kwa kuzingatia aina za tungo.
- Chagueni kadi yenye shairi.
- Bainisheni ubeti na mishororo yake.
- Mwasilisheni majibu yenu darasani.
Upimaji:
Vipi uameweza kubainisha shairi, kutoa sababu na kutambua ubeti na mshororo.
Vipi uameweza kubainisha shairi, kutoa sababu na kutambua ubeti na mshororo.
Mfano 2
Mifano:
Mashairi yafuatayo yana ubeti mmoja wenye mishororo minne kila moja.
Mfano 3
Mfano wa 1: Usafi
Usafi tuuthamini, Nyumbani na darasani,
Takataka jalalani, Si njiani si majini.
Takataka jalalani, Si njiani si majini.
Maradhi tuepukeni, tuwe wasafi jamani
Usafi ni jambo jema, sote tuudumisheni.
Mfano 4
Mfano wa 2: Ushirikiano
Tushirikiane sote, kwa pamoja tusomeni,
Tupende masomo yote, tujifunze kwa undani.
Tuulizeni lolote, ili tuende usoni.
Kazi zetu tugawane, wenzetu tuwasikize.
Kazi zetu tugawane, wenzetu tuwasikize.
Mfano 5
Mfano wa 3: Mazingira
Miti yetu tuipande, maji yetu tuyatunze,
Mazingira tuyalinde, ili nasi yatutunze
Kanuni tusizipinde, zote na tuzitangaze
Fukwe tuzisafishe, Viumbe vyote vilindwe.
Fukwe tuzisafishe, Viumbe vyote vilindwe.
Mfano 6
Mfano wa 4: Elimu
Twendeni skuli mapema, vitabu tuvithamini,
Tujitahidi kusoma, masomo yote jamani.
Elimu kwetu lazima, sote tuitafuteni.
Tusikize darasani, na maswali tuulize.
Tusikize darasani, na maswali tuulize.
Zoezi 1
Maswali na Majibu:
- Mshororo ni nini? Ni mstari mmoja wa shairi.
- Eleza tofauti kati ya mshororo na ubeti. Mshororo ni mstari mmoja; ubeti ni kundi la mishororo.
- Soma shairi la Usafi Bainisha idadi ya beti na mishororo yake. Lina ubeti mmoja wenye mishororo minne.
- Linganisha shairi la Usafi na kifungu cha habari. Taja tofauti mbili za mpangilio na uwasilishaji. - Shairi limepangwa kwa mishororo na linaweza kughaniwa kwa mahadhi.
Kifungu cha habari kwa kawaida hupangwa kwa sentensi na aya. - Mwanafunzi anasema, “Kila utungo wenye mistari minne ni shairi.” Je, unakubaliana naye? Toa sababu. - Hapana. Idadi ya mistari pekee haitoshi; tunazingatia pia lugha,
mpangilio na uwasilishaji wa utungo. - Tunga shairi fupi lenye mishororo miwili kuhusu skuli. - Mfano: Twendeni skuli mapema,
/ Vitabu tuvithamini. Majibu mengine yenye ujumbe unaoeleweka
yakubalike.
Zoezi 2
Maswali ya Jumla.
- Shairi ni nini?
- Ubeti ni nini?
- Taja vipengele viwili vya shairi.
- Shairi la Usafi lina mishororo mingapi?
- Vina vya mwisho vya shairi la Usafi ni vipi?
Majibu ya Maswali ya Jumla
- Ni utungo wa kisanaa unaotumia lugha iliyoteuliwa na kupangwa kwa namna maalumu kuwasilisha mawazo, hisia au ujumbe.
- Ni kundi la mishororo katika shairi.
- Kwa mfano, ubeti na mshororo. Vina, mizani na ujumbe pia yakubalike.
- Lina mishororo minne.
- Ni ni, inayojitokeza mwishoni mwa tuuthamini, darasani, jalalani na majini.
Hitimisho
Mashairi hutambuliwa kwa kuzingatia lugha, mpangilio na namna yanavyowasilishwa. Kusikiliza, kusoma na kughani mashairi kunakusaidia kubainisha sifa zake.
Kufafanua mashairi
Utangulizi:
Baada ya kubainisha shairi, tunahitaji kuelewa linazungumzia nini. Kufafanua shairi ni kueleza maana ya maneno, mishororo na ujumbe wake kwa lugha rahisi.
Unapofafanua, usirudie tu maneno ya shairi. Eleza unachokielewa kwa maneno yako mwenyewe.
Umahiri
Mwanafunzi aweze kueleza maana ya maneno na mishororo ya shairi, kubainisha ujumbe wake na kuufafanua kwa kutumia ushahidi kutoka katika shairi.
Dhana: Kufafanua Mashairi
Kufafanua shairi ni kueleza maana yake kwa undani unaofaa, bila kubadilisha ujumbe uliomo.
Nini Utajifunza kwa Ufupi ?
- Maana ya maneno yaliyotumika katika shairi.
- Maana ya mishororo.
- Jambo kuu linalozungumziwa.
- Kufafanua ujumbe kwa maneno yako mwenyewe.
Maelezo ya Kufafanua Shairi.
Fuata hatua hizi unapofafanua shairi:
- Sikiliza au soma shairi lote. Pata wazo la jumla.
- Tambua maneno usiyoyafahamu. Tumia muktadha, kamusi au msaada wa mwalimu.
- Eleza kila mshororo. Tumia sentensi rahisi.
- Unganisha maana za mishororo. Tambua jambo kuu linalozungumziwa.
- Toa ushahidi. Taja maneno au mshororo unaounga mkono ufafanuzi wako.
Kwa mfano, mshororo “Takataka jalalani” una maana kwamba takataka ziwekwe mahali panapofaa kukusanyiwa, badala ya kutupwa ovyo.
Ufundishaji na Ujifunzaji
Shughuli 3
Kitendo cha 1: Mshororo kwa Maneno Yangu
Fanyeni kazi wawili wawili.
- Chagueni shairi moja kati ya mifano mitano.
- Soma mshororo mmoja kwa sauti.
- Mwenzako aeleze maana yake.
- Badilishaneni nafasi.
- Hakikisheni kuwa maelezo yenu yanaendana na shairi.
Shughuli 4
Kitendo cha 2: Ujumbe wa Shairi
Katika kikundi:
- Someni shairi lote.
- Jadilini jambo kuu linalozungumziwa.
- Chagueni mshororo unaothibitisha jibu lenu.
- Mwasilisheni ufafanuzi mfupi darasani.
Upimaji wa umahiri:
Aangalia kama umeweza kuafafanua maneno kwa usahihi, kueleza ujumbe na kutoa ushahidi kutoka katika shairi.
Aangalia kama umeweza kuafafanua maneno kwa usahihi, kueleza ujumbe na kutoa ushahidi kutoka katika shairi.
Mfano 7
Mifano:
Mfano 8
Mfano wa 1: Kufafanua Shairi la Usafi
Mshororo: “Usafi tuuthamini.”
Ufafanuzi: Tuone usafi kuwa jambo muhimu na tuuzingatie katika maisha yetu. Shairi linatuhimiza kutunza usafi nyumbani na darasani, na kutotupa takataka njiani au majini.
Mfano 9
Mfano wa 2: Kufafanua Shairi la Ushirikiano
Mshororo: “Kazi zetu tugawane.”
Ufafanuzi: Kila mmoja apate jukumu la kufanya ili kazi ikamilike kwa ushirikiano. Shairi linatuhimiza kufanya kazi pamoja na kusikilizana.
Mfano 10
Mfano wa 3: Kufafanua Shairi la Mazingira
Mshororo: “Fukwe zetu zisafishwe.”
Ufafanuzi: Sehemu za ufukweni zitunzwe na kuondolewa taka. Shairi linatuhimiza kupanda miti, kutunza maji na kulinda viumbe.
Mfano 11
Mfano wa 4: Kufafanua Shairi la Urafiki
Mshororo: “Moyoni pasiwe chuki.”
Ufafanuzi: Tusihifadhi hisia za kuwachukia wengine. Shairi linatuhimiza kuishi kwa urafiki, kuheshimiana na kuepuka ugomvi.
Mfano 12
Mfano wa 5: Kufafanua Shairi la Elimu
Mshororo: “Maswali tuyaulize.”
Ufafanuzi: Tuulize maswali tunapohitaji maelezo au tunapotaka kuelewa zaidi. Shairi linatuhimiza kwenda skuli mapema, kutunza vitabu na kusikiliza darasani.
Zoezi 3
Maswali na Majibu ya Ngazi Sita za Bloom
| Ngazi | Swali au kazi | Jibu au mwongozo |
|---|---|---|
| 1. Kukumbuka | Kufafanua shairi ni nini? | Ni kueleza maana ya maneno, mishororo na ujumbe wake. |
| 2. Kuelewa | Eleza maana ya “Vitabu tuvithamini.” | Tuone vitabu kuwa muhimu, tuvitunze na kuvitumia kujifunza. |
| 3. Kutumia | Fafanua “Maji yetu tuyatunze” kwa maneno yako. | Tuhifadhi maji na tuepuke kuyachafua au kuyapoteza ovyo. |
| 4. Kuchambua | Linganisha ujumbe wa mashairi ya Ushirikiano na Urafiki. | Yote yanahimiza uhusiano mzuri. Ushirikiano linasisitiza kufanya kazi pamoja; Urafiki linasisitiza kuheshimiana na kuepuka ugomvi. |
| 5. Kutathmini | Mwanafunzi anasema, “Shairi la Elimu linatuhimiza kunyamaza bila kuuliza maswali.” - Je, ufafanuzi huo ni sahihi? Thibitisha. | Si sahihi. Mshororo “Maswali tuyaulize” unatuhimiza kuuliza ili kuelewa. |
| 6. Kuunda | Andika sentensi mbili zinazofafanua shairi la Mazingira. | Mfano: Shairi linatuhimiza kutunza mazingira. Linatuelekeza kupanda miti, kutunza maji, kusafisha fukwe na kulinda viumbe. |
Zoezi 4
Maswali ya Jumla ya Lengo Mahsusi
- Taja hatua ya kwanza ya kufafanua shairi.
- Utafanya nini ukikutana na neno usilolifahamu?
- Eleza maana ya “Kwa pamoja tusomeni.”
- Shairi la Urafiki linazungumzia jambo gani kuu?
- Kwa nini ni muhimu kutoa ushahidi kutoka katika shairi?
Majibu ya Maswali ya Jumla
- Kusikiliza au kusoma shairi lote.
- Kutumia muktadha, kamusi au kuuliza mwalimu.
- Tujifunze kwa kushirikiana na kusaidiana.
- Kuishi kwa urafiki, kuheshimiana na kuepuka ugomvi.
- Ili kuonesha kuwa ufafanuzi unaendana na maneno na ujumbe wa shairi.
Hitimisho
Kufafanua shairi kunahitaji kusikiliza au kusoma kwa makini. Maelezo yako yawe rahisi, yaeleweke na yaungwe mkono na maneno yaliyomo katika shairi.
Kueleza mafunzo yanayopatikana katika mashairi
Utangulizi:
Mashairi yanaweza kutuburudisha na kutufundisha. Baada ya kufahamu ujumbe wa shairi, tunaweza kueleza tunachojifunza na namna ya kukitumia katika maisha ya kila siku.
Kwa mfano, shairi linalohimiza ushirikiano linaweza kutufundisha kusaidiana katika kazi za darasani.
Umahiri
Uweze kubainisha mafunzo katika shairi, kuyathibitisha kwa kutumia mishororo yake na kueleza namna ya kuyatumia nyumbani, skuli au katika jamii.
Dhana: Mafunzo Yanayopatikana katika Mashairi
Mafunzo ni maarifa, maadili au mwongozo tunaoupata kutokana na ujumbe wa shairi.
Ujumbe ni jambo linalowasilishwa na shairi. Funzo ni jambo tunaloweza kujifunza kutokana na ujumbe huo.
Nini Utajifunza kwa Ufupi ?
- Kutofautisha ujumbe na funzo.
- Kubainisha mafunzo katika mashairi.
- Kuthibitisha funzo kwa kutumia mshororo.
- Kutumia mafunzo katika maisha ya kila siku.
Maelezo ya Lengo Mahsusi
Ili kueleza funzo la shairi:
- Sikiliza au soma shairi kwa makini.
- Tambua jambo kuu linalozungumziwa.
- Jiulize: Shairi hili linanifundisha nini?
- Taja mshororo unaothibitisha funzo hilo.
- Toa mfano wa kitendo kinachoonesha namna ya kulitumia.
Shairi moja linaweza kutoa mafunzo zaidi ya moja. Majibu tofauti yanaweza kukubalika ikiwa yanaungwa mkono na maneno ya shairi.
Ufundishaji na Ujifunzaji
Shughuli 5
Kitendo cha 1: Funzo na Ushahidi
Katika vikundi vidogo:
- Chagueni shairi moja.
- Andikeni funzo moja linalopatikana ndani yake.
- Taja mshororo unaothibitisha funzo hilo.
- Pendekezeni kitendo cha kutumia funzo hilo skuli.
- Elezeni majibu yenu kwa darasa.
Shughuli 6
Kitendo cha 2: Funzo kwa Vitendo
Chagua funzo moja na ulitumie katika kitendo kinachofaa, kwa mfano:
- Kupanga na kutunza vitabu.
- Kumsaidia mwenzako kuelewa kazi.
- Kuweka takataka katika chombo chake.
- Kushiriki kutunza bustani ya skuli.
Baada ya kitendo, eleza ulichofanya na funzo lililokuongoza.
Upimaji wa umahiri:
Angalia kama umeweza kubainisha funzo, unatoa ushahidi na unapendekeza matumizi yanayofaa.
Angalia kama umeweza kubainisha funzo, unatoa ushahidi na unapendekeza matumizi yanayofaa.
Mfano 13
Mifano:
| Shairi | Funzo | Ushahidi katika shairi | Matumizi katika maisha |
|---|---|---|---|
| 1. Usafi | Kutunza usafi na kutotupa takataka ovyo. | “Takataka jalalani.” | Kuweka taka katika chombo chake nyumbani na skuli. |
| 2. Ushirikiano | Kushirikiana na kugawana majukumu. | “Kazi zetu tugawane.” | Kugawana kazi katika Kitendo cha kikundi. |
| 3. Mazingira | Kulinda mazingira na viumbe. | “Viumbe vyote vilindwe.” | Kutunza miti na kuepuka kuwadhuru viumbe. |
| 4. Urafiki | Kuheshimiana na kuishi kwa amani. | “Tucheze bila ugomvi.” | Kutatua tofauti kwa mazungumzo na kucheza kwa kufuata kanuni. |
| 5. Elimu | Kujifunza kwa bidii na kuuliza maswali. | “Maswali tuyaulize.” | Kuuliza kwa heshima jambo ambalo hujalielewa. |
Zoezi 5
Maswali na Majibu
| Ngazi | Swali au kazi | Jibu au mwongozo |
|---|---|---|
| 1. Kukumbuka | Taja funzo moja katika shairi la Usafi. | Kutotupa takataka ovyo. |
| 2. Kuelewa | Kwa nini “Kazi zetu tugawane” linatufundisha ushirikiano? | Linahimiza kila mmoja kushiriki jukumu katika kazi ya pamoja. |
| 3. Kutumia | Utalitumiaje funzo la shairi la Elimu darasani? | Nitasikiliza, nitatunza vitabu na nitauliza nisipoelewa. |
| 4. Kuchambua | Tofautisha ujumbe na funzo katika shairi la Urafiki. | Ujumbe unahusu urafiki na amani. Funzo ni kuheshimiana na kuepuka ugomvi katika maisha yetu. |
| 5. Kutathmini | Kikundi kina mwanafunzi mmoja anayefanya kazi yote huku wengine wakitazama. Je, kinatumia funzo la Ushirikiano? Eleza. | Hakikitumii ipasavyo. Shairi linahimiza kugawana kazi ili wote washiriki. |
| 6. Kuunda | Tengeneza bango lenye ujumbe na mchoro unaoonesha funzo la shairi moja. | Mfano: Bango la “Tushirikiane kutunza skuli yetu” lenye wanafunzi wakigawana kazi. Bango liendane na funzo lililochaguliwa. |
Zoezi 6
Maswali ya Jumla
- Mafunzo katika shairi ni nini?
- Taja funzo moja katika shairi la Mazingira.
- Ni mshororo upi katika shairi la Urafiki unaohimiza kuheshimiana?
- Utatumiaje funzo la Ushirikiano katika kikundi?
- Je, shairi moja linaweza kutoa mafunzo zaidi ya moja? Eleza kwa mfano.
Majibu ya Maswali ya Jumla
- Ni maarifa, maadili au mwongozo tunaoupata kutokana na ujumbe wa shairi.
- Kupanda miti, kutunza maji, kusafisha fukwe au kulinda viumbe.
- “Tuheshimiane sote.”
- Nitashiriki kazi, nitagawana majukumu na nitasikiliza mawazo ya wenzangu.
- Ndiyo. Shairi la Elimu linatufundisha kwenda skuli mapema, kuthamini vitabu, kusikiliza na kuuliza maswali.
Hitimisho
Mashairi yanatupa nafasi ya kujifunza na kutafakari maisha yetu. Unapoeleza funzo, onesha ushahidi kutoka katika shairi na utoe mfano wa namna unavyoweza kulitumia. Kutumia mafunzo hayo kwa vitendo kunaonesha kuwa umeuelewa ujumbe wa shairi.
Visaasili
Kusimulia visaasili
Kubainisha wahusika katika visaasili
Kueleza mafunzo yaliyomo katika visaasili
Listening to this topic