Kiswahili

UANDISHI
♿ Accessibility: | | | |

UANDISHI

Utangulizi:
Uandishi ni njia ya kuwasilisha mawazo, habari na hisia kwa kutumia maneno yaliyoandikwa. Mtoto hujifunza kuandika ili aweze kueleza anachofikiria kwa uwazi. Katika somo hili, tutajifunza jinsi ya kuchambua habari fupi, kutumia alama za uandishi na kuandika hati zinazosomeka kwa urahisi.
Hati (maneno yasiyozidi mia moja 100)
Utangulizi:
Hati ni sanaa ya uandishi wa herufi na maneno kwa namna inayosomeka, yenye mpangilio, na inayozingatia urembo.
Lengo la Hati:
Usafi: Kuandika bila kufuta-futa au kuchafua daftari. Usahihi: Kuzingatia michoro ya herufi (kubwa na ndogo) na alama za uandishi. Nadhifu: Kupanga maneno katika mstari ulionyooka na kuacha nafasi sawa kati ya neno na neno. Hati bora humsaidia mtoto kuwasiliana kwa ufasaha na humjengea nidhamu ya kazi tangu akiwa mdogo.
Mfano wa hati nzuri:
Kuandika hati nzuri kwa muandiko mzuri ni jambo muhimu sana kwa mwanafunzi. Muandiko mzuri humsaidia mtoto kuandika herufi kwa umbo sahihi na kwa mpangilio mzuri kwenye daftari. Pia humwezesha mwalimu na wanafunzi wengine kusoma alichoandika bila shida.
Kuchambua habari fupi
Kuchambua habari fupi
Utangulizi:
Habari fupi ni maandishi mafupi yanayotoa ujumbe maalumu. Tunapochambua habari, tunatafuta maana yake, wahusika na ujumbe wake.
Dhana:
Habari fupi ni maandishi mafupi yasiyozidi maneno 100 yanayotoa ujumbe mmoja ulio wazi.
Maelezo:
Kuchambua habari fupi ni kusoma au kusikia habari ndogo/kidogo kisha kuelewa na kueleza vipengele vyake muhimu. Kwa maneno mengine, ni kuchunguza habari fupi ili kujua kinachoambiwa, nani, lini, wapi, na kwa nini, kisha kutoa maoni au muhtasari wake. Vipengele vya kuchambua habari fupi: Nani aliyehusika? – Watu au wahusika waliotajwa katika habari. Nini kimeelezwa? – Tukio au matukio yaliyojitokeza. Wapi kilitokea? – Mahali pa tukio. Lini kilitokea? – Muda au siku ya tukio. Kwa nini kilitokea? – Sababu au sababu zinazohusiana na tukio. Matokeo – Nini kilitokea baada ya tukio?
Mfano wa kuchambua habari fupi:
Habari: “Juma alipewa zawadi ya kitabu cha hadithi na mwalimu wake leo shuleni.”
Uchambuzi: Nani: Juma Nini: Alipewa kitabu cha hadithi Wapi: Shuleni Lini: Leo Kwa nini: Kwa sababu ni mwanafunzi mwema au sehemu ya sherehe Matokeo: Juma ana furaha na atasoma kitabu hicho
Activity 34
Kusoma habari kwa vikundi
Activity 35
Kujadili maana ya habari
Activity 36
Kuchora picha ya habari
Activity 37
Kuigiza tukio la habari
Example 32
Mifano. Asha alipanda mti na kuvuna maembe. Aliwashirikisha marafiki. Juma alichelewa shule kwa sababu alicheza barabarani. Mwalimu aliwaongoza wanafunzi kusafisha darasa. Zawadi alimsaidia bibi kuvuka barabara. Wanafunzi walipanda miti shuleni siku ya mazingira.
Exercise 41
Mazoezi na Majibu: Habari ya kwanza inamhusu nani? Asha Kwa nini Juma alichelewa? Alicheza barabarani Taja tendo jema ulilosoma. Kumsaidia bibi. Ni habari ipi inaonyesha ushirikiano? Kupanda miti. Je, kucheza barabarani ni sahihi? Hapana Andika habari fupi ya sentensi 3. (Mfano wowote sahihi)
Exercise 42
Maswali ya Jumla: Habari fupi ni nini? Tunachambua habari kwa nini? Ni hatua gani za kuchambua habari? Ujumbe mkuu ni nini? Nani anaweza kuwa mhusika? Majibu ya Maswali ya Jumla Ni maandishi mafupi yenye ujumbe. Ili kuelewa maana. Kusoma, kuelewa, kueleza. Wazo kuu la habari. Mtu au wahusika wa habari.
Hitimisho:
Kuchambua habari fupi humsaidia mtoto kuelewa ujumbe na kujifunza maadili mema kupitia maandishi mafupi.
Kuelezea matumizi ya alama za uandishi
Kuelezea matumizi ya alama za uandishi
Utangulizi:
Alama za uandishi husaidia maandishi yasomeke kwa urahisi na kueleweka vizuri.
Dhana:
Ni matumizi ya alama kama nukta (.), koma (,), alama ya swali (?) na mshangao (!).
Nini Utajifunza Kwa Ufupi: Kutambua alama za uandishi Kujua matumizi yake Kuzitumia katika sentensi
Maelezo:
Kueleza matumizi ya alama za uandishi ni kujua na kuelezea jinsi alama maalumu (punctuation marks) zinavyotumika katika maandishi ili kufanya sentensi kuwa sahihi na rahisi kuelewa. Kwa maneno mengine, ni kueleza kazi ya alama za uandishi kwenye maandiko, kama vile kuonyesha mwisho wa sentensi, kupumzisha kidogo, au kutofautisha wingi na mali.
Alama kuu za uandishi na matumizi yake:
Activity 38
Kulinganisha sentensi zenye alama na zisizo na alama.
Activity 39
Kujaza alama kwenye sentensi
Activity 40
Kuandika sentensi na kuweka alama stahili.
Mifano sentensi zenye vituo mbalimbali.
Ninaenda skuli. Unaitwa nani? Acha kucheza! Asha, Juma na Ali walikuja. Leo ni Jumamosi.
Exercise 43
Mazoezi na Majibu Taja alama ya swali → (?) Nukta hutumika lini? → Mwisho wa sentensi Weka alama sahihi: Unacheza ___ → ? Ni sentensi ipi ina mshangao? → Acha kucheza! Sentensi bila alama inaeleweka? → Hapana vizuri Andika sentensi yenye koma → Asha, Juma na Ali wanacheza.
Exercise 44
Maswali ya Jumla. Alama za uandishi ni nini? Taja alama mbili. Nukta hutumika wapi? Alama ya swali ina maana gani? Kwa nini tunatumia alama? Majibu ya Maswali ya Jumla. Ni alama zinazosaidia kusoma vizuri. Nukta na koma. Mwisho wa sentensi. Kuuliza swali. Kufanya maandishi yaeleweke.
Hitimisho:
Alama za uandishi hufanya maandishi yawe safi, rahisi kusoma na yenye maana sahihi.
Kuandika hati zinazosomek a kwa urahisi
Kuandika hati zinazosomek a kwa urahisi
Utangulizi:
Hati nzuri huwa na mwandiko unaoonekana wazi, safi na unaoeleweka.
Dhana:
Ni maandishi yaliyoandikwa kwa mwandiko mzuri, mpangilio sahihi na alama sahihi.
Nini Utajifunza Kwa Ufupi: Kuandika kwa mwandiko mzuri Kupanga sentensi vizuri Kutumia nafasi sahihi
Maelezo:
Kuandika hati zinazosomeka kwa wepesi ni kujenga maandishi ambayo mtu anaposoma, anaweza kuelewa kwa haraka, kwa urahisi, na bila kuchanganyikiwa. Kwa maneno mengine, ni kuandika kwa ufasaha, kutumia maneno sahihi, sentensi fupi, na alama za uandishi ili maandishi yawe wazi na rahisi kusoma. Kanuni za kuandika hati zinazosomeka kwa wepesi: Tumia sentensi fupi na rahisi – Epuka sentensi ndefu zisizoeleweka. Tumia maneno sahihi na yanayofaa – Hakikisha maneno yanalingana na umuhimu wa hati. Tumia alama za uandishi kwa usahihi – Nukta, komi, alama ya kuuliza, na alama nyingine zisaidie kutenganisha mawazo. Tumia vichwa vidogo au sehemu tofauti – Kama hati ina sehemu nyingi, toa vichwa vidogo ili kurahisisha kusoma. Panga maandishi kwa mstari au aya – Weka nafasi kati ya aya au sehemu tofauti ili macho ya msomaji yasichoke. Angalia sarufi na tahajia – Hakikisha maneno yameandikwa kwa usahihi.
Activity 41
Kunakili sentensi kwa uangalifu.
Activity 42
Kurekebisha maandishi mabaya.
Activity 43
Kushindana kuandika vizuri darasani.
Activity 44
Kuandika habari fupi.
Example 33
Mifano: Ninaenda sokoni leo. Mama anapika wali. Tunacheza mpira skuli. Ninasoma kitabu kipya. Ninamwagilia maua.
Exercise 45
Mazoezi na Majibu. Mwandiko mzuri ni upi? Mwandiko mzuri ni uliowazi na safi. Kwa nini tuache nafasi kati ya maneno? Ili maneno yasomeke vizuri. Nakili sentensi vizuri. (Mwanafunzi anaandika) Ni ipi bora kati ya mwandiko mbaya na mzuri? Mzuri. Hati isiyo nadhifu ina shida gani? Ngumu kusoma. Andika sentensi 3 kwa mwandiko mzuri. (Mifano sahihi)
Exercise 46
Maswali ya Jumla. Hati inayosomeka ni ipi? Tunaboreshaje mwandiko? Nafasi kati ya maneno ni muhimu? Kwa nini tuandike kwa usafi? Ni vifaa gani hutusaidia kuandika vizuri? Majibu ya Maswali ya Jumla Hati iliyo wazi na safi. Kufanya mazoezi ya kuandika. Ndiyo, husaidia kusoma. Ili maandishi yaeleweke. Kalamu na daftari.
Hitimisho:
Kuandika hati inayosomeka husaidia wengine kusoma na kuelewa ujumbe wetu kwa urahisi.
Imla (habari fupi isiyozidi maneno hamsini 50)
Utangulizi:
Imla ni zoezi la kusikiliza maneno au sentensi ambazo mwalimu anasoma kisha mwanafunzi anaziandika kwenye daftari kwa usahihi. Katika imla, mwanafunzi anajifunza kusikiliza kwa makini, kuandika maneno kwa tahajia sahihi, na kutumia alama za uandishi kama vile nukta (.), koma (,), na alama ya kuuliza (?). Imla humsaidia mtoto kuboresha uandishi wake, kuongeza msamiati, na kuandika sentensi zilizo sahihi. Kwa mfano, mwalimu anaweza kusoma sentensi kama “Amina anasoma kitabu.” kisha wanafunzi wanaiandika kwenye daftari. Kupitia mazoezi ya imla, mtoto hujifunza kuandika kwa muandiko mzuri na kuelewa vizuri maneno anayoyasikia darasani.
Umahiri:
Kupitia ujifunzaji wa mada hii ya imla, mwanafunzi ataweza kukuza umahiri wa kusoma kwa uelewa, kufikiri kwa mpangilio, na kupanua msamiati wake kwa kusikiliza na kuandika maneno au sentensi kwa usahihi. Aidha, mwanafunzi ataimarisha uwezo wa kuwasiliana kwa usahihi, kufanya uandishi sahihi, na kuwa na mawasiliano bora katika lugha ya Kiswahili. Kupitia mazoezi haya, mwanafunzi pia atakuza ubunifu wa lugha, jambo litakalomsaidia kutumia maneno na sentensi kwa ufasaha katika kusoma, kuandika, na kuzungumza.
Kuainisha maneno teule
Kuainisha maneno teule
Utangulizi:
Kuainisha maneno teule ni tendo la kutambua na kuchagua maneno muhimu yaliyopo katika sentensi, kifungu, au hadithi. Katika somo hili, mwanafunzi atajifunza kusoma au kusikiliza maandishi mafupi kisha kubaini maneno maalumu yaliyoteuliwa na mwalimu. Maneno haya yanaweza kuwa majina ya watu, vitu, wanyama, au mahali. Zoezi hili humsaidia mwanafunzi kuelewa vizuri maana ya sentensi, kuongeza msamiati, na kuboresha uwezo wa kusoma kwa uelewa. Kwa mfano, katika sentensi “Asha anacheza na paka,” maneno teule yanaweza kuwa Asha na paka. Kupitia mazoezi haya, mwanafunzi hujifunza kutambua maneno muhimu na kuyatumia kwa usahihi katika mawasiliano ya kila siku.
Umahiri:
Kupitia mada hii ya imla, mwanafunzi ataweza kusoma kwa uelewa, kufikiri kwa mpangilio, kupanua msamiati, na kuainisha maneno teule katika sentensi. Pia mwanafunzi ataweza kuandika kwa usahihi, kuwasiliana vizuri kwa maandishi, na kutumia lugha kwa ubunifu katika mazoezi ya kusoma na kuandika.
Dhana:
Kuainisha maneno teule ni kutambua na kuchagua maneno muhimu yaliyopo katika sentensi au kifungu cha maneno.
Nini Utajifunza Kwa Ufupi. Katika somo hili utajifunza: Kusikiliza maneno au sentensi kwa makini. Kuandika maneno kwa usahihi. Kutambua na kuainisha maneno teule katika sentensi.
Maelezo:
Mwalimu atasoma sentensi au maneno polepole. Mwanafunzi atasikiliza kwa makini na kuyaandika kwenye daftari. Baada ya kuandika, mwanafunzi ataangalia sentensi na kubaini maneno teule yaliyomo. Maneno teule yanaweza kuwa majina ya watu, wanyama, vitu au mahali. Zoezi hili humsaidia mwanafunzi kuimarisha tahajia, uelewa wa sentensi, na msamiati.
Ili uweze kuandika imla vizuri, ni lazima ufuate hatua hizi tatu ambazo ni kama nguzo za nyumba: Kusikiliza kwa Makini: Masikio yako yawe tayari kunasa kila sauti ya mwalimu. Ukikosa sauti, utakosa neno! Kuandika kwa Usahihi: Hapa unatumia mkono wako kuweka herufi mahali pake. Kwa mfano, "Baba" na siyo "Bba". Kuainisha Maneno Teule: Hapa unakuwa kama mpelelezi. Unachagua neno lile ambalo mwalimu amelisititiza au neno jipya ulilojifunza.
Example 34
Mifano ya Maneno Teule Katika Sensensi. Amina anasoma kitabu. Juma anakimbia uwanjani. Paka anakunywa maziwa. Mama anapika wali. Watoto wanacheza mpira. Ndege anaruka angani.
Example 35
Mfano wa maneno teule: Amina, Juma, paka, mama, watoto, ndege.
Activity 45
Sikiliza na andika: Mwalimu aseme sentensi, mtoto aiandike.
Activity 46
Piga mstari: Mtoto apige mstari chini ya maneno teule katika sentensi.
Activity 47
Chagua maneno: Mtoto asome sentensi na achague maneno muhimu.
Exercise 47
A.Andika sentensi hizi kisha piga mstari chini ya maneno teule. (Asha, Simba na Ali) Asha anakula embe. Simba anaishi porini. Ali anasoma darasani. B. Chagua neno teule katika sentensi hizi.(Baba na kuku) Baba anapanda gari. Kuku anakula nafaka. Majibu ya Mazoezi A Asha anakula embe. Simba anaishi porini. Ali anasoma darasani. B Baba Kuku
Exercise 48
Maswali ya Jumla ya Lengo Mahsusi Imla ni nini? Nini maana ya maneno teule? Taja mfano mmoja wa neno teule. Majibu ya Maswali ya Jumla Imla ni kusikiliza na kuandika maneno au sentensi. Maneno teule ni maneno muhimu katika sentensi. Mfano: Amina / paka / mama
Hitimisho:
Imla humsaidia mwanafunzi kusikiliza vizuri, kuandika kwa usahihi, na kutambua maneno muhimu katika sentensi. Kupitia mazoezi ya mara kwa mara, mwanafunzi ataweza kuandika kwa ufasaha na kuelewa maneno mapya.
Kubainisha hatua za uandishi wa imla
Kubainisha hatua za uandishi wa imla
Utangulizi:
Imla ni zoezi la kusikiliza maneno au sentensi zinazosemwa na mwalimu kisha mwanafunzi anaziandika kwenye daftari. Ili kuandika vizuri, mwanafunzi anapaswa kufuata hatua maalumu za uandishi wa imla.
Wanafunzi wakimsikiliza Mwalimu kabla ya kuanza kuandika Imla.
Dhana:
Hatua za uandishi wa imla ni mpangilio wa mambo anayopaswa kufanya mwanafunzi wakati wa kusikiliza na kuandika maneno au sentensi katika zoezi la imla.
Nini Utajifunza Kwa Ufupi. Katika somo hili utajifunza:
  1. Hatua za kuandika imla.
  2. Kusikiliza sentensi kwa makini.
  3. Kuandika maneno kwa tahajia sahihi.
  4. Kukagua ulichokiandika.
Maelezo. Ili mwanafunzi aandike imla vizuri, anapaswa kufuata hatua hizi:
  1. Sikiliza kwa makini: mwalimu anaposoma maneno au sentensi.
  2. Elewa sentensi: inayosomwa.
  3. Andika maneno: polepole na kwa tahajia sahihi.
  4. Angalia alama za uandishi: kama nukta na koma.
  5. Soma tena ulichoandika: ili kuona kama kuna makosa.
  6. Sahihisha makosa: ikiwa yapo.
Hatua hizi humsaidia mwanafunzi kuandika imla kwa usahihi.
Mifano ya Hatua:
  1. Mwalimu anasoma sentensi.
  2. Mwanafunzi anasikiliza kwa makini.
  3. Mwanafunzi anaandika sentensi.
  4. Mwanafunzi anatumia nukta mwisho wa sentensi.
  5. Mwanafunzi anasoma tena alichoandika.
  6. Mwanafunzi anasahihisha makosa.
Activity 48
Zoezi la kusikiliza: Mwalimu asome sentensi, mtoto asikilize bila kuandika kwanza.
Activity 49
Zoezi la kuandika: Mwalimu asome tena, mtoto aandike kwenye daftari.
Activity 50
Zoezi la kukagua: Mtoto asome alichoandika na kusahihisha makosa.
Mazoezi A.
Panga hatua hizi kwa mpangilio sahihi.
  1. Kuandika sentensi
  2. Kusikiliza mwalimu
  3. Kusahihisha makosa
  4. Kusoma tena ulichoandika
Mazoezi B
Jibu maswali haya:
  1. Hatua ya kwanza katika kuandika imla ni ipi?
  2. Kwa nini tunasoma tena tulichoandika?
  3. Taja hatua mbili za uandishi wa imla.
Majibu ya Mazoezi.
A. Mpangilio sahihi:
  1. Kusikiliza Mwalimu.
  2. Kuandika sentensi.
  3. Kusoma tena ulichoandika.
  4. Kusahihisha makosa.
B. Majibu:
  1. Kusikiliza mwalimu kwa makini.
  2. Ili kuona kama kuna makosa.
  3. Kusikiliza mwalimu na kuandika sentensi.
Maswali ya Jumla.
  1. Imla ni nini?
  2. Hatua ya kwanza ya kuandika imla ni ipi?
  3. Kwa nini ni muhimu kusahihisha makosa baada ya kuandika?
Majibu ya Maswali ya Jumla.
  1. Imla ni kusikiliza na kuandika maneno au sentensi.
  2. Kusikiliza mwalimu kwa makini.
  3. Ili kuandika kwa usahihi na kurekebisha makosa.
Hitimisho:
Hatua za uandishi wa imla humsaidia mwanafunzi kusikiliza vizuri, kuandika kwa usahihi, na kugundua makosa katika maandishi yake. Kwa kufanya mazoezi ya mara kwa mara, mwanafunzi ataweza kuandika sentensi kwa ufasaha.
Kuandika imla fupi kwa kuzingatia alama za uandishi
Kuandika imla fupi kwa kuzingatia alama za uandishi
Utangulizi:
Imla ni zoezi la kusikiliza maneno au sentensi zinazosemwa na mwalimu kisha mwanafunzi anaziandika kwenye daftari. Wakati wa kuandika imla, ni muhimu kutumia alama za uandishi kwa usahihi ili sentensi iwe na maana sahihi.
Mtoto akiandika katika daftari wakati mwalimu anasoma sentensi.
Dhana:
Kuandika imla kwa kuzingatia alama za uandishi ni kuandika maneno au sentensi ulizosikia na kutumia alama sahihi za uandishi kama nukta (.), koma (,), na alama ya kuuliza (?).
Nini Utajifunza Kwa Ufupi. Katika somo hili utajifunza:
  1. Kusikiliza sentensi za imla.
  2. Kuandika imla fupi.
  3. Kutumia alama za uandishi kwa usahihi.
Maelezo:
Mwalimu atasoma sentensi fupi. Mwanafunzi atasikiliza kwa makini na kuandika sentensi hiyo kwenye daftari. Wakati wa kuandika, mwanafunzi anatakiwa kuzingatia alama za uandishi. Kwa mfano, sentensi ikimalizika huwekwa nukta (.), na ikiwa ni swali huwekwa alama ya kuuliza (?). Matumizi sahihi ya alama hizi hufanya maandishi yaeleweke vizuri.
Kusikiliza na Kuandika Imla. Katika hatua hii, mwanafunzi anapaswa kukuza "usikivu amilifu." Imla isizidi maneno 25 mpaka 30 ili kutoichosha akili yake.
Hatua za kufuata:
  1. Soma habari yote: Mwanafunzi asikilize tu ili kuelewa muktadha.
  2. Soma kwa vipande: Soma maneno mawili au matatu, kisha mwanafunzi aandike.
  3. Soma tena kwa ukaguzi: Soma kwa kasi ya kawaida ili mwanafunzi asahihishe makosa yake mwenyewe.
Mfano wa Habari ya Imla:
"Mama alienda sokoni mapema. Alinunua samaki, nyanya na mchele. Alipofika nyumbani, alianza kupika chakula kitamu cha mchana. Sote tulifurahi sana."
Kutumia Alama za Uandishi. Kwa sasa, tunajikita katika alama nne kuu za msingi:
Alama Jina Matumizi Mfano . Kituo (Nukta) Huwekwa mwisho wa sentensi kueleza kuwa wazo limeisha. Shule yetu ni nzuri *.* , Mkato (Koma) Hutumika kutenganisha vitu kwenye orodha au kupumzika kidogo. Alinunua maembe *,* machungwa na ndizi. ? Alama ya Kiulizo Hutumika mwishoni mwa sentensi ya swali. Je, unaitwa nani *?* A, B, C Herufi Kubwa Hutumika kuanza sentensi au kuandika majina ya watu/mahali. Zanzibar ni visiwa vya maridadi.
Mifano ya Matumizi ya Alama za Uandishi.
  1. Amina anasoma kitabu.
  2. Baba anapika wali.
  3. Watoto wanacheza mpira.
  4. Mama ananunua matunda, mboga na wali.
  5. Unasoma darasani?
  6. Paka anakunywa maziwa.
Activity 51
Zoezi la kusikiliza na kuandika: Mwalimu asome sentensi, mtoto aiandike kwenye daftari.
Activity 52
Zoezi la kutambua alama: Mtoto atafute na kuzungushia alama za uandishi katika sentensi.
Activity 53
Zoezi la kusahihisha: Mtoto arekebishe sentensi ambazo hazina alama sahihi za uandishi.
  1. Juma anakula wali
  2. Mama anapika chakula
  3. Unacheza mpira
Activity 54
B. Chagua alama sahihi ya uandishi.
  1. Asha anasoma kitabu ( . / ? )
  2. Unakwenda shule ( . / ? )
Majibu ya Mazoezi:
A Juma anakula wali. Mama anapika chakula. Unacheza mpira?
B Asha anasoma kitabu. Unakwenda shule?
Activity 55
Maswali ya Jumla:
  1. Imla ni nini?
  2. Taja alama mbili za uandishi.
  3. Kwa nini tunatumia alama za uandishi katika sentensi?
Majibu ya Maswali ya Jumla:
  1. Imla ni kusikiliza na kuandika maneno au sentensi.
  2. Nukta (.) na alama ya kuuliza (?).
  3. Ili sentensi iwe na maana na ieleweke vizuri.
Hitimisho:
Kuandika imla kwa kuzingatia alama za uandishi humsaidia mwanafunzi kuandika sentensi zilizo sahihi na zinazoeleweka. Mazoezi ya mara kwa mara humwezesha mwanafunzi kutumia alama za uandishi kwa usahihi katika maandishi yake.
Utungaji wa insha fupi za mtiririko wa picha
Utangulizi:
Insha fupi ni maelezo ya kimaandishi ya mawazo, matukio, au sifa za kitu fulani yaliyopangwa kwa mtiririko sahihi na lugha rahisi. Katika ngazi hii ya elimu, insha fupi ina sifa zifuatazo:
Kichwa cha Insha. Muundo wa Aya (Ibara). Matumizi ya Lugha Rahisi. Mtiririko wa Mawazo.
Umahiri:
Kupitia mada hii ya utungaji wa insha fupi, mwanafunzi atajenga uwezo mkubwa wa ubunifu na uandishi utakaomsaidia katika kutoa ufafanuzi wa matukio mbalimbali kwa ufasaha. Mafunzo haya yanalenga kuimarisha mawasiliano kwa lugha na kumwezesha mwanafunzi kufikiri kwa mpangilio kimantiki, huku akizingatia uandishi sahihi wa maneno na alama za uandishi. Aidha, mwanafunzi atakuza ubunifu wa lugha utakaomsaidia katika uandishi wa hadithi zenye mvuto, jambo ambalo hatimaye litamjengea msingi imara wa mawasiliano bora na ya kuvutia katika maisha yake ya kila siku.
Kuainisha aina za insha
Kuainisha aina za insha
Insha ya picha ni hadithi au maelezo yanayotokana na mfululizo wa picha. Picha hutusaidia kuelewa tukio na kutunga sentensi kwa mpangilio mzuri.
Dhana:
Insha ni maandishi mafupi yanayoeleza tukio, wazo au hadithi kwa mpangilio unaoeleweka.
Nini Utajifunza Kwa Ufupi: Kutambua insha ya picha. Kueleza kinachoonekana kwenye picha. Kuelewa mtiririko wa matukio
Maelezo.
Kuainisha insha ya picha ni kuangalia picha kisha kueleza au kuandika maelezo yake kwa maneno, ukitumia sentensi zinazofaa na kwa mpangilio wa wazo. Kwa maneno mengine, ni kutafsiri picha kuwa hadithi au insha fupi inayoweza kueleweka na msomaji bila kuona picha hiyo.
Ili kumfanya mtoto ahamishe picha kutoka machoni kwenda kwenye maneno. Muongoze mtoto aeleze, "Picha hii inakuambia hadithi gani?"
Insha nzuri lazima iwe na mambo haya:Kichwa cha Insha. Muundo wa Aya (Ibara). Matumizi ya Lugha Rahisi. Mtiririko wa Mawazo.
Activity 56
Kutazama picha na kueleza matukio.
Activity 57
Kujadili picha kwa vikundi.
Activity 58
Kupanga picha kwa mpangilio sahihi.
Activity 59
Kuchora picha na kueleza.
Mifano ya Sentensi katika Insha Fupi:
  1. Mtoto anaamka, anaoga, anaenda shule.
  2. Wanafunzi wanapanda miti, wanamwagilia maji, wanacheza.
  3. Mama anapika, watoto wanasaidia, wanakula pamoja.
  4. Mtoto anaanguka, marafiki wanamsaidia, anaendelea kucheza.
  5. Wanafunzi wanafanya usafi darasani, wanakusanya taka, darasa linakuwa safi.
Exercise 49
Mazoezi na Majibu. Insha ya picha ni nini? Jibu a. Picha hutusaidia kufanya nini? Jibu b. Eleza picha ya mfano 3. Jibu c. Ni tukio lipi linaonyesha msaada? Jibu d. Ni muhimu kupanga picha? Jibu e. Chora picha 3 na eleza hadithi. Jibu f. a)Hadithi kutokana na picha. b)Kuelewa tukio. c)Mama anapika na watoto wanasaidia. d)Toa Mifano minne. e)Ndiyo. f)(Mfano sahihi)
Exercise 50
Maswali ya Jumla. Insha ya picha ni nini? Picha hutumika vipi katika insha? Kwa nini mpangilio ni muhimu? Tunawezaje kueleza picha? Ni nani anaweza kutunga insha ya picha? Majibu ya Maswali ya Jumla. Hadithi kutokana na picha Kuonyesha matukio Ili hadithi ieleweke Kwa sentensi fupi Mwanafunzi yeyote
Hitimisho:
Insha ya picha humsaidia mtoto kuelewa matukio na kuanza kujifunza utungaji wa hadithi kwa urahisi.
Kubainisha hatua za utungaji
Kubainisha hatua za utungaji
Utangulizi:
Kutunga insha ya picha kunahitaji hatua maalumu ili hadithi iwe na mwanzo, kati na mwisho.
Dhana:
Utungaji insha za picha ni mchakato wa kuangalia picha na kuandika hadithi kulingana na matukio yanayoonekana.
Nini Utajifunza Kwa Ufupi:
  • Hatua za kuangalia picha.
  • Kupanga Mawazo.
  • Kuandika sentensi kwa mpangilio.
Maelezo.
Kubainisha hatua za utungaji wa insha za picha ni kutambua na kueleza hatua kwa hatua jinsi ya kuandika insha kutokana na picha. Hii inasaidia mtoto kupanga mawazo yake kabla ya kuandika, ili insha iwe na mpangilio mzuri na iwe rahisi kueleweka.
Hatua kuu za utungaji wa insha za picha:
  1. Kuangalia picha kwa makini:
-Angalia kila kipengele kilicho kwenye picha: watu, wanyama, vitu, mahali, na matukio. -Jiulize: Nani yupo? Nini kinatokea? Wapi na lini?
2. Kukusanya Mawazo.
-Andika au kumbuka vipengele muhimu vya picha. - Weka mawazo kwa mpangilio: mwanzo, katikati, na mwisho.
3. Kuanza insha (Sentensi ya utangulizi).
-Andika sentensi ya kuanzisha insha na kueleza picha kwa ufupi. -Mfano: “Leo, watoto wapo bustanini wakicheza pamoja.”
4. Kuandika katikati ya insha (Maelezo ya kina).
-Eleza hatua au matukio yanayoendelea kwenye picha. -Tumia sentensi fupi, rahisi, na alama za uandishi. -Mfano: “Watoto wanapiga mpira. Wengine wanapanda miti. Mwalimu anawatazama kwa furaha.”
5. Kuandika hitimisho (Sentensi ya mwisho).
-Malizia insha kwa kutoa maoni au kumalizia hadithi. -Mfano: “Watoto walifurahia sana kucheza pamoja hadi mchana.”
6. Kutumia alama za uandishi.
-Hakikisha unaweka nukta, komi, alama ya kuuliza, au alama ya mshangao pale inapohitajika.
7. Kukagua insha.
-Soma insha tena kuhakikisha maneno yameandikwa kwa usahihi na mpangilio ni mzuri. -Angalia tahajia, sarufi, na matumizi ya alama za uandishi.
Activity 60
Kuorodhesha hatua za utungaji
Activity 61
Kufanya kazi za vikundi (kila kikundi kipewe eneo lake la kuandika. Mwisho kazi ichanganywe)
Activity 62
Kupanga picha kwa mpangilio. (picha ziekwe bila mpangilio)
Activity 63
Kusoma hadithi darasani.
Mifano ya Hatua.
  1. Angalia picha kwa makini
  2. Tambua wahusika
  3. Eleza tukio la mwanzo
  4. Eleza tukio la kati
  5. Andika mwisho wa hadith
Mazoezi na Majibu.
  1. Hatua ya kwanza ni ipi?Kuangalia picha
  2. Kwa nini tunatambua wahusika? Kuelewa hadithi
  3. Panga hatua sahihi za Insha. Angalia, tambua, Andika.
  4. Ni hatua ipi inaeleza mwisho? Hatua ya 5.
  5. Hatua husaidia nini? Mpangilio mzuri.
  6. Orodhesha hatua zako 3 za kuandika.(Mfano sahihi)
Exercise 51
Maswali ya Jumla. Hatua za utungaji ni zipi? Kwa nini tuanze kwa kuangalia picha? Wahusika ni nani? Mwisho wa hadithi una kazi gani? Ni muhimu kupanga mawazo? Majibu ya Maswali ya Jumla Kuangalia, kupanga, kuandika Ili kuelewa tukio Watu au wanyama kwenye hadithi Kumaliza simulizi Ndiyo
Hitimisho:
Kujua hatua za utungaji humsaidia mwanafunzi kuandika insha ya picha kwa mpangilio na ufasaha.
Kuandika insha kwa mtiririko wa picha
Kuandika insha kwa mtiririko wa picha
Utangulizi:
Kutunga insha ya picha ni kuandika hadithi kulingana na mfululizo wa picha zinazoonyesha matukio tofauti.
Dhana:
Ni hadithi zinazotokana na picha zinazofuata mpangilio wa matukio kuanzia mwanzo hadi mwisho.
Nini Utajifunza Kwa Ufupi:
  • Kuandika sentensi sahihi
  • Kutunga hadithi fupi
  • Kutumia mpangilio wa matukio
Maelezo.
Kutunga insha za mtiririko wa picha ni kuandika insha au hadithi kwa kutumia picha zilizopangwa kwa mpangilio maalumu, ambapo kila picha inafuata hatua nyingine. Kwa maneno mengine, ni kuchukua picha moja baada ya nyingine, kueleza kinachoendelea kwenye kila picha, na kuunganisha maelezo kuwa hadithi moja kamili.
Hatua za kutunga insha za mtiririko wa picha:
  1. Angalia picha zote kwa makini.
-Tambua wahusika, matukio, mahali, na wakati wa kila picha. -Jiulize: Nani yupo? Nini kinatokea?
-Angalia picha ya mwanzo, katikati, na mwisho. -Fikiria jinsi matukio yanavyohusiana ili hadithi iwe na mtiririko mzuri.
-Eleza picha ya mwanzo kwa maneno rahisi. -Mfano: “Leo asubuhi, Juma aliamka mapema na kuanza kuandaa chakula cha asubuhi.”
-Andika matukio yote yaliyo kwenye picha za kati kwa mtiririko unaofaa. -Mfano: “Baada ya kumaliza chakula, Juma alienda shuleni. Wengine walikuwa wakicheza uwanjani.”
-Malizia insha kwa matokeo au maoni ya mwisho. -Mfano: “Mwisho wa siku, Juma alirudi nyumbani akiwa na furaha kwa siku nzuri aliyokuwa nayo.”
-Nukta (.), komi (,), alama ya kuuliza (?), au alama ya mshangao (!) ili kufanya insha iwe rahisi kusoma na kuelewa.
-Hakikisha kuna mtiririko wa wazo, tahajia sahihi, na alama za uandishi zimetumika vyema.
Activity 64
Kuandika hadithi kutokana na picha.
Activity 65
Kuigiza matukio ya picha
Activity 66
Kusoma insha kwa sauti.
Activity 67
Kufanya tathmini ya rika.
Mifano wa picha kwa maelezo yake.
  1. Mtoto anaamka, anavaa sare, anaenda shule.
  2. Wanafunzi wanapanda miti, wanamwagilia, miti inakua.
  3. Mtoto anaanguka, ananyanyuliwa, anaendelea kucheza.
  4. Mama anapika, familia inakula, wanashukuru.
  5. Wanafunzi wanasoma, wanajibu maswali, wanapata sifa.
Mazoezi na Majibu.
  1. Insha ya picha huandikwa kutokana na nini? Picha
  2. Kwa nini tupange matukio? Hadithi ieleweke
  3. Andika sentensi 2 kuhusu mfano 1. (Mfano sahihi)
  4. Ni mfano upi una mafanikio? Mfano 5.
  5. Insha yenye mpangilio mzuri ina faida gani? Rahisi kusoma.
  6. Tunga insha ya sentensi 4 kutokana na picha. (Mfano sahihi)
Maswali ya Jumla.
  1. Insha ya mtiririko wa picha ni nini?
  2. Tunaanzaje kuandika?
  3. Kwa nini mpangilio ni muhimu?
  4. Ni nini kinaunda hadithi nzuri?
  5. Tunawezaje kuboresha uandishi?
Majibu ya Maswali ya Jumla.
  1. Hadithi kutokana na picha.
  2. Kwa kuangalia picha.
  3. Ili hadithi ieleweke.
  4. Sentensi zilizo wazi.
  5. Kwa kufanya mazoezi
Hitimisho:
Kutunga insha za mtiririko wa picha humsaidia mtoto kukuza ubunifu, uelewa na uwezo wa kuandika hadithi fupi kwa mpangilio mzuri.
Kuandika nambari kwa maneno (1-300)
Utangulizi:
Kuandika nambari kwa kutumia maneno kuanzia 201 hadi 300. Mwanafunzi ataelewa kuwa kila nambari inaweza kuandikwa kwa tarakimu (mfano: 215) na pia kwa maneno (mfano: mia mbili na kumi na tano). Kupitia mifano rahisi, kusoma kwa sauti na kufanya mazoezi mbalimbali, mwanafunzi ataweza kutambua na kuandika nambari hizi kwa usahihi. Ujuzi huu utamsaidia mwanafunzi kusoma, kuandika na kuelewa nambari katika maisha ya kila siku, kama vile kuhesabu vitu, kuandika bei au kutaja idadi ya vitu.
Umahiri:
Kupitia mada hii ya kuandika nambari kwa maneno, mwanafunzi atajenga umahiri mkubwa wa kusoma na kuandika nambari kwa usahihi, kuelewa thamani ya kila nafasi ya tarakimu, na kukuza uwezo wa kufikiri kwa mpangilio ili kutoa ufafanuzi na mawasiliano ya kihesabu yaliyo wazi na yenye uelewa mpana.
Dhana:
Kutambua kuwa nambari (tarakimu) zinaweza kuwakilishwa kwa kutumia maneno ya lugha ya Kiswahili kwa kuzingatia thamani ya kila tarakimu.
Kubainisha maneno ya nambari teule
Kubainisha maneno ya nambari teule
Utangulizi:
Nambari teule ni nambari maalumu tunazochagua ili kujifunza namna ya kuziandika kwa maneno. Kujua maneno ya nambari humsaidia mwanafunzi kusoma, kuandika na kuhesabu kwa ufasaha.
Dhana:
Ni kutambua na kueleza nambari kwa kutumia maneno badala ya tarakimu.
Nini Utajifunza Kwa Ufupi:
  • Kutambua nambari 201–300
  • Kuzisoma kwa maneno
  • Kuzilinganisha na tarakimu
Maelezo.
Kubainisha maneno ya nambari teule ni kutambua na kueleza maneno yanayowakilisha nambari maalumu zilizoteuliwa au kupewa kipaumbele. Kwa maneno mengine, ni kuchambua nambari fulani na kuandika au kueleza kwa maneno ni kiasi gani nambari hiyo inaonyesha.
Kubainisha Nambari 201–300.
Katika hatua ya kubainisha nambari 201 - 300, utalazimika kuzitambua na kuzitofautisha nambari kwa kuangalia tarakimu tatu zilizounda nambari hiyo.
  • Mamia: Nambari zote katika fungu hili zinaanza na tarakimu 2 (ikimaanisha Mia Mbili).
  • Makumi na Mamoja: Tarakimu zinazofuata (00 mpaka 99) zinaonyesha thamani ya makumi na mamoja.
  • Lengo: Mtoto aweze kuiona 250 na kuitambua kuwa ni "Mia mbili na hamsini" na si nambari nyingine.
Kuzisoma kwa Maneno.
Huu ni uwezo wa kutamka nambari kwa kutumia lugha sanifu ya Kiswahili. Mwanafunzi anapaswa kufuata utaratibu wa thamani ya nafasi:
  • Anza na Mamia (kila mara itakuwa "Mia mbili").
  • Fuatia na Makumi (kama hamsini, sitini, sabini).
  • Malizia na Mamoja (kama moja, mbili, tatu).
Mfano:
  • 215: Mia mbili kumi na tano.
  • 278: Mia mbili sabini na nane.
Kuzilinganisha na Tarakimu.
Hapa mwanafunzi anajenga daraja kati ya alama (tarakimu) na jina (maneno). Ni muhimu mtoto ajue kuwa "Mia mbili na tisa" ni sawa na kuandika 209 na si 2009.
Mfano wa Kuoanisha Nambari kwa Tarakimu na Maneno:
TABLE
Activity 68
Chukua kadi za nambari ambapo upande mmoja kuna tarakimu (mfano: 264) na Kadi nyengine kuna maneno (Mia mbili sitini na nne).Zigeuze na uzichanganye, chagua moja, ikiwa umechagua Kadi ya Tarakimu, tafuta Kadi ya Maneno inayolingana nayo. Fanya hivyo mara nyingi zaidi.
Activity 69
Kusoma kadi za nambari na maneno.
Activity 70
Kazi za vikundi kuoanisha nambari na maneno.
Example 36
Mifano ya Nambari kwa Tarakimu na Nambari kwa Maneno.
  1. 201 – Mia mbili na moja
  2. 215 – Mia mbili na kumi na tano
  3. 230 – Mia mbili na thelathini
  4. 256 – Mia mbili na hamsini na sita
  5. 300 – Mia tatu
Mazoezi na Majibu.
  1. 201 kwa maneno. Mia mbili na moja.
  2. 230 ni nambari ipi kwa maneno? Mia mbili na thelathini.
  3. Soma 256 kwa maneno. Mia mbili na hamsini na sita.
  4. Ipi ni kubwa kati ya 215 na 230? Kubwa ni 230.
  5. Ni sahihi kusema “Mia mbili na kumi”? Ndiyo (210).
  6. Taja nambari yoyote kati ya 201–300 na uiandike kwa maneno. (Mfano sahihi).
Maswali ya Jumla.
  1. Nambari teule ni nini?
  2. Kwa nini tujifunze maneno ya nambari?
  3. 300 kwa maneno ni nini?
  4. 215 ina maana gani kwa maneno?
  5. Tunawezaje kubaini maneno ya nambari?
Majibu ya Maswali ya Jumla.
  1. Nambari maalumu zilizochaguliwa
  2. Ili kusoma na kuandika vizuri
  3. Mia tatu
  4. Mia mbili na kumi na tano
  5. Kwa kusoma na kufanya mazoezi
Hitimisho:
Kubainisha maneno ya nambari teule humsaidia mwanafunzi kuimarisha uelewa wa nambari na mawasiliano ya kihesabu.
Kujadili maneno ya nambari teule
Kujadili maneno ya nambari teule
Utangulizi:
Kujadili maneno ya nambari humaanisha kueleza maana ya nambari kwa maneno na kuigawa katika mamia, makumi na moja, ni kuzungumza na kueleza maneno yanayoonyesha nafasi ya kitu au mtu katika mpangilio. Mfano wa maneno ya nambari teule wa kwanza, wa pili, wa tatu, wa nne au wa tano.
Dhana:
Ni maneno yanayoeleza nambari kwa kuonyesha nafasi ya nambari na thamani yake. (mamia, makumi na moja).
Nini Utajifunza Kwa Ufupi:
  • Kugawa nambari katika sehemu. Vipindi vya Nambari. (Period of Numbers)
  • Kueleza maana ya Vipindi vya Nambari.
  • Kusoma nambari kwa usahihi
Maelezo.
Mwanafunzi ataweza kufafanua maneno ya nambari teule kwa kueleza sehemu zake. Kufafanua maneno ya nambari teule ni kueleza kwa maneno maana ya nambari fulani iliyoteuliwa au kupewa kipaumbele kwa thamani yake. Kwa maneno mengine, ni kuchukua nambari fulani na kueleza au kutoa ufafanuzi wake kwa maneno ili kueleweka vizuri kwa nafasi ilipo ina thamani gani.
Maana ya Vipindi vya Nambari.
Vipindi vya Nambari ni makundi ya tarakimu tatu-tatu yanayotusaidia kusoma na kuandika nambariri kubwa kwa urahisi. Katika hesabu, tunapoandika nambariri yenye tarakimu nyingi (zaidi ya tatu), tunazigawa nambariri hizo katika makundi kuanzia upande wa kulia kwenda kushoto. Kila kundi linaitwa Kipindi (Period).
Kugawa Nambari katika Sehemu.
Ili kugawa nambari katika vipindi, tunatumia kanuni ya "Tatu-Tatu":
  1. Anza kuhesabu tarakimu kuanzia mwisho (mamoja).
  2. Weka mkato (,) au nafasi baada ya kila tarakimu tatu.
Example 37
Mfano: 7542
  • Tarakimu ya 1 ni 2 (Mamoja)
  • Tarakimu ya 2 ni 4 (Makumi)
  • Tarakimu ya 3 ni 5 (Mamia)
  • Weka mkato hapa: Tunapata 7,542.
Hapa tuna vipindi viwili:
  • Kipindi cha Mamoja (Units Period): Kinajumuisha 5, 4, na 2 (542).
  • Kipindi cha Maelfu (Thousands Period): Kinajumuisha 7 pekee (7,000).
Kusoma Nambariri kwa Usahihi.
Kanuni rahisi ya kusoma nambari kubwa ni kusoma nambari iliyo kwenye kipindi cha kwanza (kushoto), taja jina la kipindi, kisha malizia na kipindi kinachofuata.
Hatua za kusoma 6,205:
  1. Angalia nambari iliyo kabla ya mkato: 6.
  2. Taja jina la kipindi chake: Elfu. (Hapa tunapata: Elfu sita)
  3. Soma nambari zilizobaki: 205. (Mia mbili na tano)
  4. Unganisha: "Elfu sita, mia mbili na tano."
Example 38
Zoezi:
Weke mkato na azisome kwa sauti:
  • 4892→ (4,892) : Elfu nne, mia nane tisini na mbili.
  • 1050→ (1,050) : Elfu moja na hamsini.
  • 9999→ (9,999) : Elfu tisa, mia tisa tisini na tisa.
Activity 71
Kutumia vijiti au mawe kuonyesha mamia.
Activity 72
Kujenga nambari kwa vikundi.
Activity 73
Kujadili thamani ya nafasi
Activity 74
Kuandika ufafanuzi mfupi wa vipindi vya nambari.
Example 39
Mifano.
  1. 245 = Mia mbili + arobaini + tano
  2. 210 = Mia mbili + kumi
  3. 300 = Mia tatu
  4. 278 = Mia mbili + sabini + nane
  5. 201 = Mia mbili + moja
Exercise 52
Mazoezi na Majibu.
  1. 300 ina mamia mangapi? 3
  2. 245 ina makumi mangapi? 4
  3. Fafanua 278. Mia mbili + sabini + nane
  4. Ipi ina moja sifuri? 210 au 278. Ni 210
  5. Je, 201 ina makumi? Hapana
  6. Unda nambari mpya na uifafanue. (Mfano sahihi)
Exercise 53
Maswali ya Jumla.
  1. Kufafanua nambari ni nini?
  2. Nambari ina sehemu gani?
  3. Mamia ni nini?
  4. Makumi ni nini?
  5. Kwa nini tujue thamani ya nafasi?
Majibu ya Maswali ya Jumla.
  1. Kueleza nambari kwa sehemu.
  2. Mamia, makumi na moja.
  3. Sehemu ya mia.
  4. Sehemu ya kumi.
  5. Ili kuelewa nambari vizuri.
Hitimisho:
Kufafanua maneno ya nambari humsaidia mwanafunzi kuelewa muundo wa nambari na thamani ya kila sehemu.
Kuandika nambari na maneno ya nambari
Kuandika nambari na maneno ya nambari
Utangulizi:
Kuandika nambari kwa tarakimu na maneno husaidia mwanafunzi kuwasiliana kwa hesabu kwa njia mbalimbali.
Dhana.
Ni kuandika nambari kwa tarakimu na pia kwa maneno yanayolingana.
Nini Utajifunza Kwa Ufupi:
  • Kuandika nambari kwa maneno
  • Kubadilisha maneno kuwa nambari
  • Kusoma na kuandika kwa usahihi
Maelezo.
Kuandika nambari na maneno ya nambari ni uwezo wa kuonyesha nambari kwa tarakimu na pia kwa maneno kwa wakati mmoja. Kwa maneno mengine, ni kuandika nambari kama “5” na pia kuandika maneno yake “tano” ili kuhakikisha kwamba nambari inafahamika vizuri kwa wote wanaosoma.
Activity 75
Shughuli za Mwanafunzi.
Cheza mchezo wa kuagua Kadi za maneno na Kadi za nambari kwa Tarakimu.
Activity 76
Fanya mashindano ya kuandika Nambari kwa Tarakimu na Nambari kwa Maneno.
Example 40
Mifano.
  1. 205 – Mia mbili na tano.
  2. 222 – Mia mbili na ishirini na mbili.
  3. 240 – Mia mbili na arobaini.
  4. 275 – Mia mbili na sabini na tano.
  5. 299 – Mia mbili na tisini na tisa.
Exercise 54
Mazoezi na Majibu.
  1. Andika 205 kwa maneno. Mia mbili na tano.
  2. Mia mbili na arobaini ni nambari ipi? 240.
  3. Andika 275 kwa maneno. Mia mbili na sabini na tano.
  4. Ipi ni ndogo kati ya 222 na 299? 222.
  5. Je, 240 imeandikwa sahihi? Ndiyo.
  6. Andika nambari mpya na maneno yake. (Mfano sahihi).
Exercise 55
Maswali ya Jumla.
  1. Kwa nini tuandike nambari kwa maneno?
  2. 299 kwa maneno ni nini?
  3. Mia mbili na ishirini ni nambari ipi?
  4. Ni muhimu kujua maneno ya nambari?
  5. Tunawezaje kufanya mazoezi?
Majibu ya Maswali ya Jumla.
  1. Ili kuelewa na kuwasiliana vizuri.
  2. Mia mbili na tisini na tisa.
  3. 220.
  4. Ndiyo.
  5. Kwa kuandika na kusoma.
Hitimisho:
Kuandika nambari kwa maneno na tarakimu humsaidia mwanafunzi kuimarisha ujuzi wa hesabu na uandishi kwa ufasaha.
Listening to this topic