Kiswahili

SARUFI
♿ Accessibility: | | | |

SARUFI

Nyakati za msingi (wakati uliopo, uliopita na ujao)
Utangulizi:
Sarufi ni kanuni za lugha zinazotusaidia kuzungumza na kuandika kwa usahihi. Kupitia sarufi, mwanafunzi hujifunza namna ya kutumia maneno vizuri ili sentensi ziwe na maana. Katika somo hili, tutajifunza nyakati za msingi: wakati uliopo, uliopita na ujao kwa kutumia mbinu za CBC zinazohusisha ushirikiano, vitendo na ubunifu.
Sarufi ni kanuni za matumizi sahihi ya lugha.
Umahiri.
Kupitia ujifunzaji wa mada hii ya Sarufi, mwanafunzi atajenga umahiri thabiti katika uelewa wa kanuni za lugha, uandishi wa sentensi sahihi, na matumizi fasaha ya vitenzi, jambo ambalo litamwezesha kuwasiliana kwa ujasiri na ubunifu huku akikuza stadi za kusoma na kuandika kwa usahihi wa hali ya juu.
Dhana:
Sarufi inampa mwanafunzi "vifaa" vya kuelezea hisia zake, kutoa maelekezo,kujua jinsi kitenzi kinavyobadilika kulingana na wakati (Uliopita, Uliopo, na Ujao) na kuandika sentensi kwa usahihi.
Kubainisha nyakati
Kubainisha nyakati
Utangulizi:
Baadhi ya maneno hutusaidia kujua tukio lilitokea lini—jana, leo au kesho. Maneno haya hutuonesha wakati uliopita au ujao.
Dhana:
Wakati uliopita huonesha tukio lililokwisha, na wakati ujao huonesha tukio litakalotokea baadaye.
Nini Utajifunza Kwa Ufupi:
  • Kutambua maneno ya wakati uliopita
  • Kutambua maneno ya wakati ujao
  • Kutofautisha nyakati
Maelezo.
Kubainisha maneno yanayoonesha wakati uliopita na ujao ni kutambua maneno au viashiria vinavyoonyesha tukio lilishatokea (uliopita) au litatokea baadaye (ujao). Hii humsaidia mwanafunzi kuelewa muda wa tukio katika sentensi.
Kuelewa Nyakati za Vitenzi ni hatua muhimu inayomsaidia mwanafunzi kueleza matukio katika mtiririko sahihi wa muda.
Wakati Uliopita.
Wakati huu unatumika kuelezea jambo ambalo tayari limeshafanyika na kumalizika.
  • Kiambishi chake: Ni -LI-.
  • Neno la ishara: Mara nyingi huambatana na maneno kama jana, juzi, zamani, mwaka jana.
Example 41
Mifano:
  • Sisi tulicheza mpira jana.
  • Mama alipika chakula kitamu.
  • Mwanafunzi alisoma kitabu chake.
Wakati Ujao.
Wakati huu unatumika kuelezea jambo ambalo bado halijafanyika lakini linatarajiwa kufanyika baadaye.
  • Kiambishi chake: Ni -TA-.
  • Neno la ishara: Mara nyingi huambatana na maneno kama kesho, keshokutwa, baadaye, wiki ijayo.
Jinsi ya Kutofautisha Nyakati.
Mwanafunzi anaweza kutofautisha nyakati hizi kwa kuangalia kiambishi kilichopo katikati ya neno (kati ya kiwakilishi cha nafsi na mzizi wa neno).
Jaduweli la kutofautisha nyakati.
WakatiKiambishiMfano wa SentensiMuda wa Tukio
Uliopita-LI-Juma alikimbia.Tukio limeshapita.
Ujao-TA-Juma atakimbia.Tukio bado kufanyika.
Activity 77
Mchezo wa "Nilikua na Nitakuwa:
Sema kitu kimoja ulichofanya jana (uliopita) na kitu kimoja anachopanga kufanya kesho (ujao). Hii inamsaidia kuunganisha vitendo halisi na sarufi ya lugha.
Activity 78
Kadi za maneno (jana, kesho, baadaye)
Changanya kadi zilizoandikwa. Sentensi za jana, kesho na baadae. Chagua, ifunue na uisome kwa sauti.
Example 42
Mifano ya wakati uliopita na wakati ujao.
  1. Jana nilicheza mpira.
  2. Kesho nitaenda shule.
  3. Tulipanda miti jana.
  4. Tutaimba kesho.
  5. Alisoma kitabu jana.
Exercise 56
Mazoezi na Majibu.
  1. Taja neno la wakati uliopita. Jana
  2. “Kesho” inaonesha nini? Wakati ujao
  3. Chagua sentensi ya wakati uliopita. Mfano 1
  4. Ni ipi inaonesha wakati ujao? Mfano 2
  5. “Nilicheza” ni wakati gani? Uliopita
  6. Tunga sentensi ya wakati ujao. (Mfano sahihi)
Exercise 57
Maswali ya Jumla.
  1. Wakati uliopita ni nini?
  2. Wakati ujao ni nini?
  3. Taja neno la wakati ujao.
  4. “Jana” huonesha nini?
  5. Kwa nini tujue nyakati?
Majibu ya Maswali ya Jumla.
  1. Tukio lililokwisha.
  2. Tukio litakalokuja.
  3. Kesho.
  4. Wakati uliopita.
  5. Ili sentensi ziwe sahihi.
Hitimisho:
Kubainisha maneno ya nyakati humsaidia mwanafunzi kuelewa lini tukio lilitokea au litatokea.
Neno hubadilika kulingana na wakati.
Kutunga Sentensi Sahihi.
Ili kutunga sentensi, unahitaji kufuata mtiririko huu: Mtendaji + Kitenzi (kilichonyambulishwa) + Kitu/Maelezo.
Exercise 58
Mazoezi na Majibu.
  1. “Nilikula” ni wakati gani? Uliopita
  2. “Nitakimbia” inaonesha nini? Wakati ujao
  3. Badilisha “Ninasoma” kuwa uliopita. Nilisoma
  4. Ni ipi inaonesha ujao? Nitaimba
  5. “Nilicheza” ni sahihi kwa jana? Ndiyo
  6. Tunga sentensi 2 za nyakati tofauti. (Mfano sahihi)
Kutumia wakati uliopita na ujao kutunga sentensi.
Utangulizi:
Tunapotunga sentensi, tunachagua wakati sahihi ili kueleza tukio lililopita au litakalokuja.
Dhana:
Ni kuandika sentensi zinazoonesha matukio ya jana au yajayo.
Nini Utajifunza Kwa Ufupi:
  • Kutunga sentensi za jana
  • Kutunga sentensi za kesho
  • Kutumia maneno ya nyakati
Maelezo:
Kutumia wakati uliopita na ujao kutunga sentensi ni kuandika sentensi zinazoonyesha matendo yaliyokwisha kufanyika (uliopita) au yatakayofanyika baadaye (ujao) kwa kutumia vitenzi vinavyoendana na muda.
Ili kutunga sentensi za jana (wakati uliopita) na kesho (wakati ujao), tunabadilisha tu kiambishi cha wakati katikati ya kitenzi.
Kutunga Sentensi za Jana (Wakati Uliopita)
Tunatumia kiambishi cha wakati -li-. Pia, tunaweza kutumia maneno ya ziada kama jana, juzi, au zamani ili kutoa msisitizo.
Muundo:
Nafsi + -li- + Tendo
  • Mimi: Nilifika nyumbani jana.
  • Wewe: Ulinunua matunda juzi.
  • Sisi: Tulicheza mpira asubuhi.
  • Wao: Walimaliza kazi yao mapema.
Kutunga Sentensi za Kesho (Wakati Ujao)
Tunatumia kiambishi cha wakati -ta-. Maneno yanayoambatana na wakati huu ni kama kesho, kuta, wiki ijayo, au baadaye.
Activity 79
Kuandika sentensi binafsi.
Activity 80
Kusoma sentensi kwa sauti.
Activity 81
Michezo ya kubadilisha nyakati
Example 43
Mifano ya Sentensi za wakati uliopita na wakati ujao.
  1. Jana nilisoma kitabu.
  2. Kesho nitaenda sokoni.
  3. Jana tulicheza mpira.
  4. Kesho tutaimba darasani.
  5. Jana alikimbia haraka.
Majina (ya dhahania na ya jumla)
Utangulizi:
Kila kitu unachokiona, unachokigusa, au unachokiwaza kina jina lake. Bila majina, tusingeweza kuitana au kuagiza chakula tunachokipenda! Katika somo hili, tutazama ndani zaidi ili kugundua aina mbili za majina ambazo ni muhimu sana katika lugha yetu ya Kiswahili.
Dhana:
Majina (Nomino) ni maneno yanayotaja mtu, kitu, mahali, hali, au wazo lolote. Leo tutaangalia Majina ya Dhahania (vitu tunavyohisi lakini hatuwezi kuvigusa).
Kubainisha majina.
Utangulizi:
Majina ni maneno yanayotaja watu, vitu, wanyama au hisia. Kuna majina ya jumla kama mtoto, kitabu, mbwa; na majina ya dhahania kama furaha, upendo na amani.
Ni kutambua maneno yanayotaja vitu vinavyoonekana na visivyoonekana (hisia au hali).
Majina ya jumla.
Haya ni majina yanayotaja vitu au viumbe kwa ujumla, si jina maalumu la mtu au kitu fulani.
Example 44
Mifano ya Majina ya jumla:
  • mtoto
  • mwalimu
  • shule
  • kitabu
  • mti
  • mnyama
Example 45
Mfano wa sentensi:
  • Mtoto anasoma darasani.
  • Mwalimu anafundisha wanafunzi.
Majina ya dhahania.
Haya ni majina yanayotaja hisia, hali, tabia, au mawazo ambayo huwezi kuyaona au kuyashika kwa mkono, bali unayahisi au kuyafikiria.
Mifano wa Majina ya Dhahania:
  • furaha
  • huzuni
  • upendo
  • amani
  • ujasiri
  • elimu
Activity 82
Unachotakiwa kufanya:
Chukua mfuko usioonekana ndani au sanduku. Weka vitu 5 tofauti (kama kijiko, rula, tunda, jiwe, na soksi).
Zoezi: Funga macho, ingiza mkono, shika kitu kimoja na ukitaje jina lake kabla ya kukitoa nje. Yale majina unayotaja (kijiko, rula...) ndiyo majina ya jumla!
Example 46
Mifano ya Majina.
  1. Mtoto anacheza mpira. (mtoto – jina la jumla)
  2. Mbwa anakimbia. (mbwa – jina la jumla)
  3. Furaha ilitawala darasani. (furaha – dhahania)
  4. Upendo hujenga urafiki. (upendo – dhahania)
  5. Mwalimu anaandika ubaoni. (mwalimu – jumla)
Kuhusisha matendo na wakati uliopita na ujao katika sentensi.
Utangulizi:
Katika sentensi, majina huunganishwa na vitendo vinavyoonesha wakati uliopita au ujao. Mfano: Mtoto alicheza jana; Mtoto atacheza kesho.
Ni kutumia majina pamoja na vitendo vinavyoonesha tukio lililopita au litakalotokea.
Kuhusisha matendo na wakati uliopita na ujao katika sentensi ni kuonyesha tendo (kitenzi) kwa namna inayoeleza kama tukio lilishatokea zamani au litatokea baadaye. Hivyo, unabadilisha kitenzi kulingana na muda wa tukio.
Kuunganisha Jina na Tendo:
Hapa tunaweka jina (mtu au kitu) pamoja na neno la hatua (tendo) ili kueleza nini kinatokea.
Kutumia Wakati Uliopita (Alama ya -li-)
Tunatumia wakati huu kuelezea jambo ambalo tayari limeshafanyika na kumalizika. Tunatumia kiambishi -li-.
Kutumia Wakati Ujao (Alama ya -ta-)
Tunatumia wakati huu kuelezea jambo ambalo bado halijatokea lakini litakuja kutokea baadaye. Tunatumia kiambishi -ta-.
Activity 83
"Kadi za Wakati"
Unachotakiwa kufanya:
Kata vipande viwili vya karatasi. Moja andika -LI- (Jana) na nyingine andika -TA- (Kesho).
Zoezi: Mzazi au mwalimu anataja sentensi ya jumla (mfano: Paka anakula samaki). Mtoto anapaswa kunyanyua kadi ya -TA- na kusema sentensi hiyo kwa wakati ujao (Paka atala samaki).
Hitimisho:
Kuhusisha majina na vitendo vya nyakati tofauti humsaidia mwanafunzi kuunda sentensi zilizo sahihi na zenye maana.
Kutumia majina katika utungaji wa sentensi.
Majina hutumika kutaja watu, vitu au hisia ndani ya sentensi. Tunapotumia majina ya jumla na ya dhahania, sentensi zetu huwa wazi na zenye maana. Mfano: Mtoto anacheza (jina la jumla) na Furaha imetanda darasani (jina la dhahania).
Ni kutumia majina ya jumla na ya dhahania kuunda sentensi zilizo kamili na zinazoeleweka.
Maelezo:
Kutumia majina katika utungaji wa sentensi ni kuweka majina (nomino) ndani ya sentensi ili kutaja watu, vitu, wanyama, mahali, au hali zinazohusika katika ujumbe. Majina husaidia sentensi kuwa na maana kamili na kueleweka vizuri.
Kutunga Sentensi kwa Kutumia Majina.
Sentensi ni kundi la maneno yanayotoa ujumbe kamili. Tunapotunga sentensi, tunaanza na Jina (nani au nini) kisha tunaweka Tendo (anafanya nini).
Mifano:
  1. Dada anapika chakula. (Dada ni jina la jumla).
  2. Ujasiri unasaidia kushinda hofu. (Ujasiri ni jina la dhahania).
  3. Kalamu imeanguka chini. (Kalamu ni jina la jumla).
Kutofautisha Majina ya Jumla na ya Dhahania.
Hapa mtoto anajifunza kutofautisha kati ya kitu kinachogusika na kile kinachohisika tu moyoni au akilini.
Mifano ya Tofauti:
  1. Chakula (Jumla - unaweza kukila) dhidi ya Njaa (Dhahania - unaisikia tu tumboni).
  2. Maua (Jumla - unaweza kuyanusa na kuyashika) dhidi ya Uzuri (Dhahania - ni sifa unayoiona lakini huwezi kuishika).
  3. Askari (Jumla - ni mtu unayemwona) dhidi ya Amani (Dhahania - ni hali ya utulivu nchini).
Kuandika Sentensi Fupi na Sahihi.
Sentensi sahihi ni ile inayozingatia upatanisho wa kisarufi (maneno yanavyoendana). Kwa mtoto wa darasa la tatu, sentensi fupi ni bora zaidi kwa mawasiliano.
Activity 84
Chemsha Bongo ya Picha.
Zoezi la Kuchora:
Mpe mtoto karatasi iliyogawanywa mara mbili.
Upande wa Kwanza:
Mwambie achore kitu chochote anachokiona darasani (kama dawati) na aandike sentensi fupi: "Dawati ni jina la jumla."
Upande wa Pili:
Mwambie achore uso wenye tabasamu (smile) na aandike chini yake: "Furaha ni jina la dhahania."
Example 47
Mifano.
  1. Mtoto anasoma kitabu. (jina la jumla)
  2. Mwalimu anafundisha darasani. (jina la jumla)
  3. Furaha ilijaa uwanjani. (jina la dhahania)
  4. Upendo hujenga urafiki. (jina la dhahania)
  5. Mbwa anakimbia haraka. (jina la jumla)
Hitimisho:
Kutumia majina katika utungaji wa sentensi humsaidia mwanafunzi kuandika sentensi zilizo wazi, sahihi na zenye maana, hivyo kuboresha ujuzi wa lugha na mawasiliano.
Listening to this topic