Kiswahili

MAWASILIANO
♿ Accessibility: | | | |

MAWASILIANO

Utangulizi:
Mawasiliano ni kitendo cha kutoa au kubadilishana taarifa, mawazo, au hisia kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine. Kwa kifupi, ni kuongea, kusikiliza, kuandika, au kusoma ili kuelewana.
Ishara
Ishara.Ishara ni alama au vitendo vinavyoonesha ujumbe fulani. Mfano, mtu akitikisa mkono anaweza kumaanisha “kwaheri”.
Kubainisha mawasiliano ya ishara.
Kubainisha mawasiliano ya ishara.
Utangulizi:
Mawasiliano ni njia tunazotumia kuwasilisha ujumbe kwa wengine. Tunaweza kuwasiliana kwa maneno, picha au ishara. Ishara hutusaidia kuelewana hata bila kuongea.
Umahiri.
Katika tokeo mahsusi hili. Utapata umahiri wa kujadili kwa vikundi, Kusikiliza na kutoa maoni, Kufikiri kwa kina, kujadili kwa vikundi, kusikiliza na kutoa maoni pamoja na kufikiri kwa kina.
Dhana:
Ishara ni alama au vitendo vinavyotumika kupeleka ujumbe bila maneno.
Nini Utajifunza Kwa Ufupi:
  • Maana ya Ishara,
  • Aina za Ishara
  • Umuhimu wa ishara katika maisha
Maelezo.
Mawasiliano ya ishara ni njia ya kuwasiliana kwa kutumia alama, vitendo au miondoko ya mwili badala ya maneno ya kusema. Kwa mfano, kupunga mkono kuashiria “kwaheri”, kutikisa kichwa kuonyesha “ndiyo” au “hapana”, na kuonyesha kidole kuomba ruhusa ya kuzungumza darasani. Mawasiliano ya ishara humsaidia mtoto kuelewana na wengine hata bila kuongea, na hufanya mawasiliano yawe rahisi, ya heshima na yenye kueleweka.
Picha ikionesha Ishara mbali mbali.
Mifano:
  1. Kuinua mkono darasani kuomba ruhusa
  2. Taa nyekundu barabarani
  3. Kutabasamu kuonesha furaha
  4. Kupunga mkono kusema kwaheri
  5. Alama ya kimya maktaba
Exercise 1
Mazoezi na Majibu.
1.Taja ishara mbili ulizowahi kuona. Mf: taa ya barabarani, kuinua mkono. 2. Kwa nini ishara ni muhimu? Husaidia kuelewana bila maneno. 3. Chora ishara ya kusimama.(Chora alama ya STOP). 4. Tofautisha ishara ya furaha na huzuni.Furaha–tabasamu; huzuni–uso wa kununa. 5. Je, ishara zote zinaeleweka kila mahali?Hapana, zingine hutegemea utamaduni. 6. Tengeneza ishara mpya ya “safi sana”.Mf: kidole gumba juu.
Exercise 2
Maswali ya Jumla.
  1. Ishara ni nini?
  2. Toa mifano miwili ya ishara.
  3. Ishara hutumika wapi?
Majibu ya Zoezi la Jumla.
  1. Ni alama au vitendo vya kuwasilisha ujumbe.
  2. Kupunga mkono, taa ya barabarani.
  3. Shuleni, barabarani, nyumbani.
Hitimisho:
Ishara hutusaidia kuelewana kwa haraka na kwa urahisi bila kutumia maneno.
Kujadili ishara za mawasiliano.
Kujadili ishara za mawasiliano.
Utangulizi:
Kuna ishara nyingi tunazotumia kila siku kuonesha hisia au kutoa maelekezo.
Umahiri.
Katika tokeo mahsusi hili. Utapata umahiri wa kujadili kwa vikundi, Kusikiliza na kutoa maoni, Kufikiri kwa kina, kujadili kwa vikundi, kusikiliza na kutoa maoni pamoja na kufikiri kwa kina.
Dhana:
Ni ishara zinazotumika kupeleka ujumbe kwa watu wengine.
Nini Utajifunza Kwa Ufupi:
Maana ya Ishara, Aina za Ishara na Umuhimu wa ishara katika maisha
Maelezo:
Watoto watajadili ishara kwa kutumia picha, maigizo na hadithi fupi darasani. Taa Nyekundu: Inamaanisha Simama. Inatumika kuzuia magari au watu wasiendelee mbele ili kuzuia ajali. Taa ya Njano: Inamaanisha Jiandae. Inatumika kutoa tahadhari kuwa taa inakaribia kubadilika, ama kuwa nyekundu au kijani. Taa ya Kijani: Inamaanisha Nenda. Inatumika kuruhusu magari au watu kupita baada ya kuwa salama.
2. Alama ya Kivuko cha Watembea kwa Miguu (Zebra Crossing) Hizi ni mistari myeusi na meupe inayopakwa barabarani. Maana yake ni sehemu salama ya watembea kwa miguu kuvukia barabara. Inatumika mahali ambapo watu wengi wanahitaji kuvuka, kama vile karibu na shule au sokoni.
3. Ishara ya Hatari (Fuvu la Kichwa na Mifupa) Hii ni alama inayoonyesha picha ya fuvu la kichwa cha binadamu na mifupa miwili iliyopishana. Maana yake ni hatari kubwa ya kifo au sumu. Inatumika kwenye chupa za dawa kali za kuua wadudu, nyaya za umeme mkubwa, au maeneo yenye kemikali hatari.
4. Ishara ya Huduma ya Kwanza (Alama ya Jumlisha) Hii ni alama ya "nyota" au "jumlisha" (+) ambayo mara nyingi huwa na rangi nyekundu au kijani. Maana yake ni mahali pa kupata matibabu au msaada wa kwanza. Inatumika kwenye milango ya zahanati, hospitali, na kwenye magari ya kubebea wagonjwa (Ambulance).
5. Ishara ya Chakula (Kijiko na Uma) Hii ni picha inayoonyesha kijiko na uma vikiwa vimekaa pamoja. Maana yake ni kuna huduma ya chakula au kinywaji. Inatumika kando ya barabara kuelekeza watu kwenye migahawa, hoteli, au sehemu za kupumzikia wasafiri.
Jambo la Kukumbuka: Ni muhimu sana kutii ishara hizi wakati wote. Kwa mfano, usivuke barabara mpaka uone magari yamesimama kwenye mistari ya kuvukia, na usiguse chupa yoyote yenye alama ya fuvu la kichwa kwani inaweza kukudhuru.
Picha ikionesha Ishara mbali mbali.
Mifano:
Kidole gumba juu – sawa. Kupeperushaa mikono – furaha. Kukunja uso – hasira. Alama ya hospitali. Alama ya kuvuka barabara
Mazoezi na Majibu.
Exercise 3
1.Taja ishara ya hospitali. Alama ya msalaba. 2.Kwa nini tunajadili ishara? Kuelewa maana yake. 3. Oneshea ishara ya “njoo hapa”. (Mtoto afanye kwa vitendo). 4. Ni ishara ipi hutumika barabarani? Alama za taa. 5. Ni ishara ipi muhimu zaidi shuleni? Kuinua mkono. 6. Tengeneza ishara ya “soma kimya”. Kidole mdomoni.
Maswali ya Jumla.
Exercise 4
Ishara za mawasiliano ni nini? Toa mifano miwili. Kwa nini tunazijadili? Majibu Ni ishara za kupeleka ujumbe. Kidole gumba juu, alama ya hospitali. Ili kuelewa matumizi yake.
Hitimisho:
Kujadili ishara hutusaidia kuzitambua na kuzitumia vizuri.
Kutumia ishara katika mawasiliano.
Kutumia ishara katika mawasiliano.
Utangulizi:
Tunapotumia ishara vizuri, tunaweza kuelewana hata bila kuzungumza.
Umahiri:
Katika matokeo mahsusi haya utapata umahiri wa Kuigiza. Kushirikiana na Kutatua matatizo
Dhana:
Matumizi ya vitendo au alama kupeleka ujumbe.
Nini Utajifunza Kwa Ufupi:
  • Namna ya kutumia ishara
  • Wakati sahihi wa kutumia ishara
  • Heshima katika mawasiliano
Maelezo:
Kuwasiliana kwa Ishara kwa Heshima.
1. Namna ya Kutumia Ishara
Ishara ni matumizi ya viungo vya mwili kutoa ujumbe bila kutumia maneno. Katika mawasiliano yetu ya kila siku, tunaweza kutumia njia hizi:
Kuitikia kwa Kichwa:
Inamaisha kichwa chini na juu kidogo kuonyesha "Ndiyo" au kukubali jambo. Tikisa kichwa kushoto na kulia kuonyesha "Hapana".
Kutumia Mikono:
Inua mkono juu unapotaka kuuliza swali au kuomba ruhusa ya kusema darasani. Pia, unaweza kupungia mkono kusalimia rafiki aliye mbali.
Sura ya Tabasamu:
Tumia tabasamu unaposalimia au unaposhukuru ili kuonyesha furaha na urafiki.
Kukonyeza au Kunyooshea Kidole:
Kumbuka, si vizuri kumnyooshea mtu kidole cha shahada kwani inaweza kuonekana kama utovu wa nidhamu. Badala yake, tumia kiganja cha mkono kuonyesha upande unakoelekeza.
2. Wakati Sahihi wa Kutumia Ishara:
Ni muhimu kujua ni lini utumie ishara ili ujumbe wako ueleweke vizuri:
Sehemu Zenye Utulivu:
Unapokuwa maktaba au wakati mwalimu anafundisha, tumia ishara (kama kunyoosha mkono) ili usipige kelele na kuwasumbua wengine.
Kutokea Mbali:
Unapomwona rafiki yako kwa mbali na huwezi kumfikia kwa sauti, unaweza kumpungia mkono.
Kutilia Mkazo Maneno:
Unaposema "Asante," unaweza kuambatisha na tabasamu au kuinama kidogo ili kuonyesha unamaanisha unachosema.
3. Heshima Katika Mawasiliano.
Mawasiliano bora ni yale yanayozingatia adabu na heshima kwa kila mtu:
Kusikiliza kwa Makini:
Mtu mwingine anapozungumza, mtazame usoni na usimtishe. Hii inaonyesha unamthamini.
Kutumia Lugha ya Adabu:
Tumia maneno ya heshima kama "Samahani," "Tafadhali," na "Asante."
Kujali Wakubwa:
Unapozungumza na mwalimu au mzazi, simama vizuri na usitumie ishara za dharau (kama kuweka mikono kiunoni au mfukoni).
Subira:
Usimkate mtu maneno. Subiri amalize kusema, kisha na wewe uanze kutoa maoni yako kwa sauti ya upole.
Mifano:
Angalia mifano ifuatayo:
Kuinua mkono kuomba ruhusa. Kupiga makofi kupongeza. Kupunga mkono kusalimia. Kidole mdomoni – kimya. Kuonyesha njia kwa mkono.
Mazoezi ya Majibu.
1.Taja ishara ya pongezi. Kupiga makofi. 2. Kwa nini tunatumia ishara? Kuwasiliana haraka. 3. Onesha ishara ya kimya. Kidole mdomoni. 4. Ni ishara ipi ya heshima darasani? Kuinua mkono. 5. Je, ishara zinaweza kuumiza hisia? Ndiyo, zikitumiwa vibaya. 6. Tengeneza mchezo wa kuwasiliana kwa ishara. Mf: mtoto aseme bila maneno.
Maswali ya Jumla.
Toa mifano miwili ya ishara. Ni lini tunatumia ishara? Kwa nini tuwe na heshima tunapotumia ishara?
Majibu.
Kupiga makofi, kupunga mkono. Tunapohitaji kuwasiliana bila maneno. Ili kuepuka kuumiza wengine.
Hitimisho:
Kutumia ishara vizuri hutusaidia kuwasiliana kwa heshima na kuelewana kwa urahisi
Mazungumzo
Utangulizi:
Mazungumzo ni njia ya kuwasiliana kwa kuzungumza na kusikilizana. Ili mazungumzo yawe mazuri, yanahitaji kuwa na sifa maalum kama heshima, kusikiliza na kuzungumza kwa sauti nzuri.
Katika matokeo mahsusi haya utapata umahiri wa Kusikiliza kwa makini, Kujieleza kwa ufasaha, Kushirikiana na wengine na Kujiamini katika kuzungumza.
Dhana:
Sifa za mawasiliano ni tabia nzuri zinazofanya mazungumzo yaeleweke na yawe ya heshima.
Nini Utajifunza Kwa Ufupi:
Maana ya sifa za mazungumzo. Sifa muhimu za mazungumzo mazuri. Jinsi ya kuwa msikilizaji mzuri.
Kufafanua sifa za mazungumzo
Kufafanua sifa za mazungumzo
Utangulizi:
Mazungumzo yanaweza kuwa ya aina mbalimbali kulingana na watu na mahali. Tunaweza kuzungumza na rafiki, mwalimu au mzazi kwa namna tofauti.
Umahiri.
Katika matokeo mahsusi haya utapata umahiri wa Kusikiliza kwa makini, Kujieleza kwa ufasaha, Kushirikiana na wengine na Kujiamini katika kuzungumza.
Dhana:
Sifa za mawasiliano ni tabia nzuri zinazofanya mazungumzo yaeleweke na yawe ya heshima.
Nini Utajifunza Kwa Ufupi.
Maana ya sifa za mazungumzo. Sifa muhimu za mazungumzo mazuri. Jinsi ya kuwa msikilizaji mzuri
Maelezo.
Mazungumzo ni mawasiliano yanayotokea wakati watu wawili au zaidi wanapoongea na kusikilizana kwa kubadilishana mawazo, habari au hisia. Katika mazungumzo, mtu mmoja huzungumza na mwingine husikiliza kisha hujibu kwa heshima. Kwa mfano, mwanafunzi akimuuliza mwalimu swali na mwalimu akajibu, hapo panakuwa na mazungumzo. Mazungumzo husaidia watu kuelewana, kujifunza na kudumisha uhusiano mzuri.
Mifano ya Sifa za Mazungumzo:
Example 1
Kusikiliza bila kukatiza
Example 2
Kuheshimu maoni ya wengine
Example 3
Kuzungumza kwa sauti ya wastani.
Example 4
Kutumia maneno ya heshima
Example 5
Kuangalia anayezungumza
Exercise 5
Mazoezi na Majibu: 1. Taja sifa mbili za mazungumzo mazuri. Kusikiliza, kuheshimu. 2. Kwa nini tusikatize wengine wanapozungumza? Ni heshima na husaidia kuelewa. 3. Onesha jinsi ya kusikiliza vizuri. Kuangalia mzungumzaji na kukaa kimya. 4. Tofautisha mazungumzo ya heshima na yasiyo ya heshima. Heshima–kusikiliza; yasiyo–kupaza sauti. 5. Ni sifa ipi muhimu zaidi? Kwa nini? Kusikiliza – husaidia kuelewa ujumbe. 6. Tengeneza sheria 3 za mazungumzo darasani. Sikiliza, ongea kwa zamu, tumia heshima.
Exercise 6
Maswali ya Jumla Sifa za mazungumzo ni nini? Taja sifa mbili. Kwa nini kusikiliza ni muhimu? Majibu: Ni tabia nzuri za kuzungumza. Kusikiliza, kuheshimu. Husaidia kuelewa vizuri.
Hitimisho:
Mazungumzo mazuri yanahitaji heshima, kusikiliza na kuzungumza kwa utulivu.
Kueleza aina za mazungumzo
Kueleza aina za mazungumzo
Utangulizi:
Mazungumzo yanaweza kuwa ya aina mbalimbali kulingana na watu na mahali. Tunaweza kuzungumza na rafiki, mwalimu au mzazi kwa namna tofauti.
Umahiri.
Katika tukio mahsusi hili utajifunza. Kutofautisha aina za mazungumzo, Kujieleza kwa kujiamini na Kufanya kazi kwa vikundi.
Dhana:
Ni namna mbalimbali za kuzungumza kulingana na mazingira au watu.
Nini Utajifunza Kwa Ufupi.
Aina tofauti za mazungumzo. Mahali yanapotumika. Namna sahihi ya kuzungumza.
Maelezo.
Uunaweza kujifunza aina kuu 3 za mazungumzo ambazo ni rahisi kuelewa:
Mazungumzo ya kirafiki:
Haya ni mazungumzo ya kawaida kati ya marafiki au familia, kama kusalimiana au kuulizana hali.
Example 6
Juma: "Habari rafiki yangu! Twende tukacheze mpira uwanjani?" Ali: "Sawa Juma, ngoja nichukue viatu vyangu kwanza tukiandane!"
Mazungumzo ya kimasomo:
Hufanyika shuleni kati ya mwanafunzi na mwalimu au wanafunzi kwa wanafunzi wakati wa kujifunza.
Example 7
Mwanafunzi 1: "Samahani, hapa kwenye swali la hisabati tunatakiwa kujumlisha au kutoa?" Mwanafunzi 2: "Hapa tunatakiwa kujumlisha namba hizi mbili ili tupate jumla kuu."
Mazungumzo ya heshima (rasmi)
Haya ni mazungumzo yenye adabu zaidi, kama kuomba msaada, kuzungumza na mgeni au mtu mzima.
Example 8
Mwanafunzi: "Shikamoo Mwalimu. Naomba unielekeze njia ya kwenda ofisi ya Mwalimu Mkuu." Mwalimu: "Marahaba mwanangu. Njia ni hiyo ya kulia, nenda moja kwa moja mpaka mwisho."
Aina hizi hukusaidia kujifunza jinsi ya kuzungumza kwa heshima na kuelewana vizuri na watu tofauti katika maisha ya kila siku.
Exercise 7
Mazoezi na Majibu. 1.Taja aina moja ya mazungumzo. Mazungumzo ya kirafiki. 2. Kwa nini mazungumzo ya darasani hutofautiana na ya nyumbani Mazungumzo ya darasani yana heshima zaidi. 3. Onesha mazungumzo ya kuomba msaada. “Naomba unisaidie tafadhali.” 4. Ni aina ipi hutumika darasani? Mazungumzo ya darasani. 5. Ni mazungumzo gani yanahitaji heshima zaidi? Ya darasani na kwa watu wazima. 6. Tengeneza mfano wa mazungumzo ya kirafiki. Watoto wawili wakisalimiana.
Maswali ya Jumla Aina za mazungumzo ni nini? Toa mifano miwili. Ni wapi tunatumia mazungumzo ya kirafiki? Majibu Ni namna tofauti za kuzungumza. Kirafiki, darasani. Kwa marafiki.
Hitimisho:
Kujua aina za mazungumzo hutusaidia kuzungumza kwa njia sahihi kulingana na mazingira.
Kuwasiliana kwa kuzungumza
Kuwasiliana kwa kuzungumza
Utangulizi:
Tunapozungumza vizuri na wengine tunajenga urafiki na kuelewana zaidi.Kuwasiliana kwa mazungumzo ni kitendo cha kubadilishana mawazo, habari, au hisia kati ya mtu mmoja na mwingine kwa kutumia sauti na maneno. Hii ni njia kuu tunayotumia kuelewana kila siku tukiwa shuleni, nyumbani, au michezoni.
Umahiri
Katika matokeo mahsusi haya uweze Kujieleza kwa ujasiri, Kusikiliza, Kushirikiana na Kutatua changamoto
Dhana:
Ni kutumia maneno kuwasilisha mawazo na hisia kwa watu wengine.
Nini Utajifunza Kwa Ufupi.
Jinsi ya kuanzisha mazungumzo. Namna ya kusikiliza. Matumizi ya maneno ya heshima.
Maelezo.
Kuwasiliana kwa mazungumzo ni kubadilishana habari, mawazo au hisia kwa kuongea na kusikilizana kati ya watu wawili au zaidi. Mtu mmoja huzungumza na mwingine husikiliza kisha hujibu kwa heshima. Kwa mfano, mwanafunzi akimuuliza rafiki swali na rafiki akajibu, hapo wanawasiliana kwa mazungumzo. Njia hii husaidia watu kuelewana, kujifunza pamoja na kujenga urafiki mzuri.
Mifano kuwasiliana kwa Mazungumzo.
Example 9
Kusalimiana
Example 10
Kuuliza swali
Example 11
Kujibu kwa heshima
Example 12
Kuomba ruhusa na Kushukuru
Exercise 8
Mazoezi na Majibu. 1. Taja njia moja ya kuanzisha mazungumzo. Kusalimia. 2. Kwa nini tusikilize wengine? Ili kuelewa ujumbe. 3. Onesha jinsi ya kuomba ruhusa. “Naomba ruhusa tafadhali.” 4. Mazungumzo mazuri yana sifa gani? Heshima na kusikiliza. 5. Je, kupaza sauti ni mazungumzo mazuri? Hapana. 6. Tengeneza mazungumzo mafupi ya salamu. “Habari?” “Nzuri, asante.”
Maswali ya Jumla Kuwasiliana kwa mazungumzo ni nini? Toa mfano mmoja. Kwa nini heshima ni muhimu? Majibu Ni kuzungumza ili kuelewana. Kusalimiana. Hujenga urafiki na amani.
Hitimisho:
Mazungumzo mazuri hutusaidia kujenga mahusiano na kuelewana kwa furaha.
Maandishi
Utangulizi:
Mawasiliano ya maandishi ni njia tunavyotumia maneno yaliyoandikwa ili kuwasilisha ujumbe. Hii inaweza kuwa barua, ujumbe mfupi au picha zilizo na maneno.
Umahiri.
Kutambua aina tofauti za maandishi. Kusoma kwa makini..Kuandika ujumbe mfupi kwa usahihi.
Dhana:
Ni kuwasiliana kwa kutumia maneno yaliyoandikwa ili wengine waelewe ujumbe.
Nini Utajifunza Kwa Ufupi:
Kutambua maandishi kama njia ya mawasiliano Kufahamu umuhimu wa maandishi katika maisha Kuandika ujumbe mfupi
Kuainisha mawasiliano ya maandishi
Kuainisha mawasiliano ya maandishi
Maelezo.
Mawasiliano ya maandishi ni njia ya kupeleka ujumbe kwa kutumia maneno yaliyoandikwa badala ya kuzungumza kwa sauti. Mfano wa mawasiliano ya maandishi ni barua, ujumbe mfupi wa simu, matangazo, vitabu au kazi za darasani zilizoandikwa. Mawasiliano haya humsaidia mtoto kusoma na kuandika ili kueleza mawazo yake kwa uwazi na kuelewa ujumbe wa wengine kwa urahisi.
Mifano ya Mawasiliano ya Maandishi.
Example 13
Kutambua maandishi kama njia ya mawasiliano.
Maandishi ni alama au michoro tunayotumia kuwakilisha sauti tunazozungumza. Badala ya kutumia mdomo kusema, tunatumia mikono yetu kuweka maneno kwenye karatasi, ubao, au simu. Tunayaona wapi? Tunatambua maandishi kwenye vitabu, vibao vya shule, majina ya maduka, na hata kwenye chati za darasani. Maana yake: Kila neno lililoandikwa lina kubeba ujumbe. Ukiona neno "HATARI" limeandikwa mahali, maandishi hayo yanakuambia ukae mbali bila mtu yeyote kusema kwa sauti.
Example 14
Kufahamu umuhimu wa maandishi katika maisha.
Maandishi ni muhimu sana kwa sababu: Kutunza Kumbukumbu: Tunaandika mambo ili tusiwasahau. Kwa mfano, ratiba ya masomo au tarehe ya kuzaliwa. Kufikisha Ujumbe Mbali: Maandishi yanatusaidia kuwasiliana na watu walioko mbali (kama barua au ujumbe wa simu). Kujifunza: Vitabu vimejaa maandishi yanayotupa maarifa mapya kuhusu sayansi, hesabu, na mazingira yetu. Maelekezo: Maandishi yanatusaidia kujua namna ya kutumia kitu, kwa mfano, maelekezo ya jinsi ya kumeza dawa au kutumia mchezo mpya.
Example 15
Kuandika ujumbe mfupi.
Ujumbe mfupi unapaswa kuwa na mambo matatu muhimu ili ueleweke: Mlengwa: Unamuandikia nani? (Mfano: Mama, Mwalimu, au Rafiki). Habari: Unataka kusema nini? (Tumia maneno machache na yaliyo wazi). Mwandishi: Wewe ni nani? (Andika jina lako mwishoni).
Exercise 9
Mazoezi na Majibu. 1.Taja mfano mmoja wa mawasiliano ya maandishi. Barua kwa rafiki. 2.Kwa nini maandishi ni muhimu? Husaidia kuelewa ujumbe bila kuwa pamoja. 3.Andika ujumbe mfupi “Habari za asubuhi.” (Mtoto aweke kwenye karatasi). 4.Tofautisha ujumbe wa maandishi na mazungumzo. Maandishi–umeandikwa, Mazungumzo–unaongezeka kwa sauti. 5.Ni maandishi gani yanatumika shuleni zaidi? Vitabu, vibao, taarifa. 6.Tengeneza ujumbe mfupi wa kuwashukuru walimu “Asante mwalimu kwa kunisaidia leo.”
Exercise 10
Maswali ya Jumla Mawasiliano ya maandishi ni nini? Taja mifano miwili. Ni kwa nini maandishi ni muhimu? Majibu ya Maswali ya Jumla Ni kuwasiliana kwa maneno yaliyoandikwa. Barua, ujumbe mfupi. Husaidia kuelewa ujumbe bila kuwa pamoja.
Hitimisho:
Mawasiliano ya maandishi ni njia muhimu ya kueleza mawazo na hisia kwa wengine kwa maneno yaliyoandikwa.
Kueleza aina za mawasiliano ya maandishi
Kueleza aina za mawasiliano ya maandishi
Utangulizi:
Maandishi hutumika kwa namna tofauti. Tunaweza kutumia barua, kadi, vibao au vitabu. Kila aina inafaa kwa mahali fulani.
Umahiri
Katika matokeo mahsusi haya utaweza Kutofautisha aina za maandishi, Kueleza wakati na mahali yanapotumika na Kuandika ujumbe kwa usahihi
Dhana:
Ni namna mbalimbali za kutumia maandishi kuwasiliana na wengine.
Nini Utajifunza Kwa Ufupi.
Aina mbalimbali za maandishi. Namna ya kutumia aina hizo. Umuhimu wa aina hizo
Maelezo.
Watoto watajifunza kupitia picha, vitabu na michezo ya kuigiza aina tofauti za mawasiliano ya maandishi. Kuna aina nyingi za mawasiliano ya maandishi.ila kwa sasa tunaweza kujifunza aina kuu 3 za mawasiliano ya maandishi:
Example 16
Barua:
Ujumbe unaoandikwa kumpelekea mtu mwingine, kama rafiki au mzazi.
Example 17
Ujumbe mfupi:
Maneno mafupi ya taarifa, kama ujumbe wa simu au dokezo darasani.
Example 18
Matangazo na taarifa:
Maandishi yanayotoa habari kwa watu wengi, kama tangazo la shule au taarifa kwenye ubao.
Aina hizi hukusaidia kujifunza kuandika na kusoma ujumbe kwa usahihi na kwa urahisi.
Exercise 11
Mazoezi na Majibu. 1.Taja aina moja ya mawasiliano ya maandishi. Barua. 2.Kwa nini kadi hutumika? Kuonesha hisia za furaha au shukrani. 3.Andika ujumbe mfupi wa kupongeza rafiki. “Hongera kwa kupata alama nzuri.” 4.Tofautisha barua na SMS. Barua–inachukua muda, SMS–haraka. 5.Ni maandishi gani ni rahisi kuyasoma mara moja? SMS na vibao. 6.Tengeneza aina mpya ya ujumbe wa maandishi shuleni. Vibao vya heshima kwa wanafunzi wengine.
Exercise 12
Maswali ya Jumla Taja aina mbili za mawasiliano ya maandishi. Barua hutumika kwa nini? Kadi hutumika wapi? Majibu ya Maswali ya Jumla Barua, SMS. Kuandikia rafiki au mwalimu. Kuonesha pongezi au shukrani.
Hitimisho:
Kujua aina za maandishi kunasaidia kutumia ujumbe sahihi kwa wakati na mahali husika.
Kuwasiliana kwa maandishi
Kuwasiliana kwa maandishi
Utangulizi:
Kuwasiliana kwa maandishi ni kutumia maneno yaliyoandikwa kueleza mawazo, hisia au taarifa kwa wengine. Hii hufanya ujumbe uwe wazi na unaweza kuhifadhiwa kwa muda mrefu.
Umahiri:
Katika matokeo mahsusi haya utaweza, Kuandika ujumbe kwa usahihi, Kufahamu nani anapaswa kupokea ujumbe na Kusoma na kuelewa maandishi ya wengine.
Dhana:
Ni kutumia maandishi kueleza ujumbe kwa wengine kwa njia ya huru na sahihi.
Nini Utajifunza Kwa Ufupi:
Namna ya kuwasiliana kwa maandishi. Kuandika ujumbe mfupi na wenye maana. Kusoma maandishi ya wengine kwa ufasaha.
Maelezo:
Kuwasiliana kwa maandishi ni kutumia kalamu na karatasi (au kifaa cha kielektroniki) kutoa taarifa bila kuzungumza. Ili uwasiliane vizuri:
Mwandiko Safi:
Hakikisha herufi zako zimechorwa vizuri ili msikilizaji (msomaji) asipate shida kuelewa.
1. Alama za Uandishi:
Tumia alama kama nukta (.) unapomaliza sentensi na alama ya swali (?) unapouliza, ili ujumbe ueleweke vizuri.
Mpangilio:
Anza na salamu, taja jambo unalotaka, na kisha malizia kwa jina lako.
2. Kuandika Ujumbe Mfupi na Wenye Maana.
Ujumbe mzuri hauhitaji maneno mengi, unahitaji maneno sahihi. Ili uandike ujumbe wenye maana: Lenga Shida: Sema moja kwa moja unachohitaji. Tumia Lugha ya Adabu: Hata katika maandishi, maneno kama "Tafadhali" na "Asante" ni muhimu. Mfano wa ujumbe usio na maana: "Niletee kile kitu." (Msomaji hatajua ni kitu gani). Mfano wa ujumbe wenye maana: "Mama, tafadhali niletee kitabu changu cha Hisabati. Asante."
3. Kusoma Maandishi ya Wengine kwa Ufasaha.
Kusoma kwa ufasaha ni kusoma kwa kasi ya wastani, kwa usahihi, na kwa hisia zinazohitajika.
Tazama Maneno: Usiviepushe macho yako kwenye neno mpaka ulimalize lote ili usikosee maana. Zingatia Vituo: Unapoona koma (,), pumzika kidogo. Unapoona nukta (.), tua kabisa kabla ya kuendelea. Sauti ya Kusomea: Ikiwa unasoma kwa sauti, hakikisha unatamka kila neno kwa nguvu ya wastani ili wengine wasikie vizuri ujumbe ulioandikwa.
Mifano.
Kuandika barua ya shukrani. Kutuma SMS ya kumualika rafiki. Kutoa taarifa shuleni. Kadi ya pongezi kwa mwalimu. Vibao vya tahadhari au taarifa.
Exercise 13
Mazoezi na Majibu. 1.Taja mfano wa kuwasiliana kwa maandishi. SMS kwa rafiki. 2.Kwa nini tunatumia maandishi badala ya maneno? Wanaweza kuhifadhiwa na kuonekana tena. 3.Andika ujumbe mfupi wa shukrani kwa mwalimu. “Asante mwalimu kwa kunisaidia leo.” 4.Tofautisha barua na taarifa shuleni. Barua–kwa mtu mmoja; taarifa–kwa watu wengi. 5.Je, ujumbe mfupi unapaswa kuwa mrefu au mfupi? Mfupi na wazi. 6.Tengeneza ujumbe mfupi wa kuomba msaada shuleni. “Naomba msaada kwenye hesabu, tafadhali.”
Exercise 14
Maswali ya Jumla Kuwa waandishi wa maandishi ni nini? Taja njia tatu za kuwasiliana kwa maandishi. Kwa nini ujumbe mfupi ni muhimu? Majibu ya Maswali ya Jumla Ni kutumia maandishi kueleza ujumbe. Barua, SMS, kadi. Kwa kuwa unaeleweka haraka na kwa usahihi.
Hitimisho:
Kuwasiliana kwa maandishi ni njia muhimu ya kueleza mawazo na hisia kwa wengine, kwa usahihi na kwa heshima.
Listening to this topic