Kiswahili Darasa la VII Syllabus
-
-
Kutumia msamiati katika kuandaa matini mbalimbali
-
Kufupisha habari/hadithi aliyoisoma kwa kutumia maneno yake na kubainisha mawazo yote ya msingi ya mwandishi na kuyaelezea kwa usahihi
-
Kusikiliza hotuba na kubainisha mambo muhimu yanayotokana na hotuba na kuyahusianisha na maisha ya kila siku
-
Kuandika insha inayoeleweka kuhusu uharibifu wa mazingira kwa kuzingatia alama zote za uandishi
-
Kutunga hadithi fupi na kuelezea maana za maneno yote mapya na kuelezea jinsi yanavyotumika katika maisha ya kila siku
-
-
Kutumia msamiati katika kuandaa matini mbalimbali
-
Kuandika shairi linaloelezea muonekano wa hali ya hewa katika mazingira kwa kuzingatia kanuni za shairi
-
Kuandika habari fupi kwa kutumia majina sahihi ya kazi za watu
-
Kuandika sentensi kwa kutumia maneno yanayoonesha umiliki
-
-
Kutumia msamiati katika uandishi katika kuandaa matini mbalimbali
-
Kuunda maneno mapya kwa kubadili mpangilio wa herufi na silabi (mila-lami, lima, mali) ili kukuza msamiati
-
Kuchanganua vitu mbalimbali na kuvitofautisha kiasi chake katika sentensi kwa kutumia ….ingi.… ....engi….. …kidogo…… ....chache.......
-
Kuandika insha yenye kueleweka kuhusu ugonjwa wa UKIMWI
-
Kuandika kifungu cha habari fupi kwa mpangilio wa sentensi unaoeleweka
-
-
Kutumia msamiati katika uandishi wa matini mbalimbali
-
Kuandika hadithi fupi kwa kuzingatia kanuni na alama za uandishi
-
Kuandika habari fupi kwa mpangilio unaoeleweka kuhusu shughuli za kila siku
-
-
Kuandika sentensi kwa kutumia nyakati mbalimbali (uliopo, ujao uliopita na timilifu)
-
Kutumia maandishi katika mawasiliano kulingana na miktadha mbalimbali
-
Kubaini muundo wa kadi za mialiko, kuandika na kueleza matumizi yake
-
Kueleza kanuni za uandishi wa baruayakirafiki na rasmi, kutaja faida zake na kueleza namna ya kuzitumia barua hizo katika mazingira ya kila siku
-
Kubaini miundo ya barua za kirafikinarasmi na kuiandika kwa kuitofautisha katika miktadha mbalimbali
-
-
Kutumia maandishi katika kuwasiliana kulingana na miktadha mbalimbali
-
Kuandika hadithi fupi yenye maana kwa kuzingatia alama za uandishi na mtiririko wa matukio katika aya
-
Kuandika Insha kimantiki kuhusu elimu ya afya na uzazi
-
Kuandika majina ya ndege waliopo katika mazingira yao na kuelezea sifa na tabia zao
-
Kuandika barua ya kiofisi kwa kuzingatia mtiririko wa vipengele vya uandishi wa barua
-
Kuandika habari kwa kuzingatia taratibu na alama za uandishi
-
Kuandika risala fupi kwa kuzingatia muundo na kanuni za uandishi
-
Kuandika insha kuhusu umuhimu wa kuwa na familia ndogo
-
Kuandika kumbukumbu za mikutano kwa kuzingatia vipengele vyake vya uandishi
-
Kuandika methali zenye mafunzo kulingana na kifungu cha habari
-
Kuandika vipengele vya muundo wa insha
-
Kufupisha habari katika maandishi bila kupotosha maana iliyokusudiwa na kwa kuzingatia alama za uandishi
-
Kuandika kirefu cha vifupisho vya maneno au majina ya msingi (JKT, UDA, TBC TET, BMT)
-
Kuandika matangazo mbalimbali kuzingatia kwa taratibu za uandishi
-
-
Kutumia msamiati katika kuzungumza kwa kuwasilisha hoja kulingana na miktadha mbalimbali
-
Kusoma habari na kubainisha maneno mapya na kuelezea maana zake kwa kutumia kamusi
-
Kuelezea na kubaini maneno mapya katika risala iliyowasilishwa
-
Kubaini aina saba za maneno katika sentensi (Nomino, kitenzi, kielezi, kivumishi, kiwakilishi, kiunganishi na kihisishi)
-
-
Kutumia msamiati katika kuzungumza kwa kuwasilisha hoja kulingana na muktadha mbalimbali
-
Kuelezea idadi ya vitu vinavyohesabika katika umoja na wingi kwa kutumia sentensi kanushi
-
Kutofautisha na kueleza vitu katika hali ya ukubwa na udogo wake
-
Kuelezea muonekano wa hali ya hewa katika mazingira yake kikamilifu (ukungu, upepo, joto, baridi, mvua)
-
Kuelezea shughuli anazotenda mwanafunzi kila siku shuleni na kuandika habari fupi kwa mpangilio
-
Kuelezea shughuli za mwanafunzi anazotenda kila siku nyumbani kwa mpangilio
-
Kufanya ziara nje ya darasa na kubaini majina ya maua tofauti yanayopatikana na kuelezea sifa zake
-
Kusimulia hadithi fupi kwa kutumia majina ya wanyama wa porini
-
Kutunga sentensi kwa kutumia majina ya wanyama wanaofugwa na kuelezea faida zake
-
-
Kutumia msamiati katika mazungumzo kwa kuwasilisha hoja kulingana na miktadha mbalimbali
-
Kusoma magazeti mbalimbali yanayoelezea shughuli za kielimu, kiuchumi na kisiasa na kubaini maneno mapya, kuelezea maana zake na kuyatungia sentensi kwa usahihi
-
Kuandika risala kwa kuzingatia alama za uandishi na kuelezea matumizi yake katika miktadha mbalimbali
-
Kubainisha na kuelezea mambo muhimu ya kuzingatia katika uandishi wa risala na kueleza matumizi yake kwa usahihi kwa kuzingatia miktadha mbalimbali
-
Kutunga hadithi fupi na kuelezea mafunzo yanayopatikana katika hadithi hiyo na kuhusianisha na maisha ya kila siku
-
Kutunga sentensi kwa kutumia aina saba za maneno kwa usahihi kwa kuzingatia miktadha mbalimbali
-
Kubainisha aina saba za maneno na dhima zake katika sentensi na kutambua kifupisho cha kila aina ya neno
-
Kuwasilisha hoja na kuzielezea kwa kufuata mpangilio sahihi wa mawazo katika miktadha mbalimbali
-
-
Kutumia msamiati katika kuanzisha na kuendeleza mazungumzo katika miktadha mbalimbali
-
Kubainisha majina ya wanyama, muonekano, sauti zao na kueleza wanakoishi
-
Kutaja majina ya wanafamilia nyumbani katika kusimulia hadithi fupi na kubainisha uhusiano wao
-
-
Kuanzisha na kuendeleza mazungumzo katika miktadha mbalimbali
-
za nahau na kutumia nahau mbalimbali katika mazungumzo kwa kuzingatia miktadha mbalimbali
-
Kutumia nafsi tatu katika sentensi kwa kuzingatia hali ya umoja na wingi
-
Kutoa taarifa kwa ukamilifu kuhusu tukio lililotokea
-
Kushiriki katika mjadala kuhusu matumizi ya simu ya mdomo
-
Kueleza hatua za uandishi wa habari fupi/ insha
-
Kueleza mafunzo yaliyopatikana katika methali na kulinganisha na maisha ya kila siku katika miktadha mbalimbali
-
Kusimulia mambo yaliyoonekana baada ya kufanya ziara fupi katika mazingira ya jirani na shule
-
Kusimulia hadithi kwa kuzingatia mtiririko wa mawazo
-
Kutafsiri lugha ya picha katika vitendawili na kuelezea maana zake kwa kuhusianisha na maisha ya kila siku
-
Kutunga sentensi kwa kutumia kauli taarifa
-
Kutumia nahau katika sentensi mbalimbali
-
Kubainisha na kueleza taswira za kimawazo zilizo katika nahau kutoka katika hadithi
-
Kusimulia hadithi yenye methali na kuelezea maana ya mafunzo yaliyopatikana katika methali
-
Kuchambua maudhui yote yaliyomo katika mashairi ya kimapokeo na kisasa, kuyaelezea na kuyahusianisha na mazingira ya kila siku
-
Kutunga sentensi kwa kutumia kauli halisi
-
Kutambua methali zinavyotumika katika mazungumzo na kuelezea maana zake
-
Kutafsiri taswira inayoakisiwa na nahau
-
Kughani tenzi na kuelezea ujumbe unaopatikana na kuhusianisha na mazingira ya kila siku
-
Kuelezea vitu vilivyopo katika mazingira yao katika hali ya umoja na wingi kwa vitu vyenye uhai na visivyo na uhai
-
Kuigiza igizo dhima kuhusu elimu ya biashara na kueleza umuhimu wake
-
Kughani shairi kwa kuzingatia kanuni za mashairi (vina, mizani na kituo)
-
Kutumia nahau katika habari fupi na kuelezea maana zake
-
Kutunga mashairi ya kisasa yenye beti sita au zaidi na kuyahusianisha na mazingira ya kila siku
-
Kutaja na Kueleza mawazo makuu yaliyomo katika wimbo wa kizalendo
-
Kutamba ngonjera kwa kuzingatia kanuni za utambaji
-
Kutunga mashairi ya kimapokeo yenye mishororo minne kwa kuzingatia kanuni za utunzi wa mashairi na kuyahusianisha na mazingira ya kila siku
-
Kutega na kutegua vitendawili na kuvihusianisha na vitu vilivyopo katika mazingira kwa usahihi
-
Kubainisha na kueleza sifa za mashairi ya kimapokeo na kisasa na kuyatofautisha
-
Kuimba wimbo wa kizalendo kwa ufasaha (Tazama Ramani)
-
-
Kutumia matamshi sahihi katika kutamka maneno mbalimbali
-
Kutamka matamshi sahihi ya maneno yenye herufi ‘l’ na ‘r’
-
Kutamka maneno yenye herufi ‘z’ na ‘dh’
-
Kutamka maneno yenye herufi ‘s’ na ‘th’ kwa usahihi
-
-
Kutambua sauti mbalimbali katika matamshi ya silabi, maneno sentensi na habari fupi
-
Kutamka sauti za herufi mwambatano ng’w, nyw, shw na nyingine zenye muundo huo katika silabi, sentensi, maneno na habari fupi
-
Kutamka sauti za herufi mwambatano lw, pw, sw, tw na nyingine zenye muundo huo katika silabi, maneno, sentensi na habari fupi
-
Kutamka sauti za herufi mwambatano gh, py, nz, ky na herufi nyingine zenye muundo huo katika silabi, maneno, sentensi na habari fupi
-
-