Historia ya Tanzania na Maadili (New) Form 2 Syllabus
-
-
Kutumia maarifa na ujuzi wa chimbuko na ukuaji wa mfumo wa ukoloni kuelewa uhusiano wa kihistoria kati ya Tanzania na mataifa yaliyoitawala
-
Kuchambua chimbuko la ukoloni
-
Kubainisha mataifa yaliyoitawala Tanzania na mifumo yake ya kikoloni katika uchumi, utawala na utamaduni
-
Kujadili mchango wa mifumo ya kikoloni katika uhusiano wa Tanzania na mataifa yaliyoitawala
-
-
Kutathmini athari za mfumo wa ukoloni kwenye maadili ya jamii za Kitanzania
-
Kueleza hali ya maadili ya jamii za Kitanzania kipindi ukoloni unaingia
-
Kuchambua athari za mfumo wa ukoloni katika maadili ya jamii za Kitanzania
-
Kubaini maadili yaliyo- dumishwa na jamii za Kitanzania wakati wa ukoloni
-
-
Kuchambua jitihada za jamii za Kitanzania kupinga ukoloni na maadili ya kikoloni
-
Kubaini sababu za jamii za Kitanzania kupinga uvamizi wa kikoloni, ukoloni na maadili yake
-
Kujadili njia mbalimbali zilizotumika na jamii za Kitanzania kupinga uvamizi wa kikoloni, ukoloni na maadili yake
-
Kufafanua misingi na mbinu zilizotumika kupigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar
-
Kutathmini mchango wa harakati za kupinga uvamizi na ukoloni katika kutunza maadili ya Kitanzania na kujenga uzalendo
-
-
-
-
Kuchambua mifumo ya uchumi, siasa, utamaduni, jamii na maadili iliyojengwa, 1961-1966
-
Kueleza hali ya uchumi, siasa, utamaduni, jamii na maadili mara baada ya uhuru
-
Kutathmini mikakati na changamoto za ujenzi wa Taifa kiuchumi, kisiasa, kiutamaduni, kijamii na kimaadili kipindi cha 1961-1966
-
-
Kumudu historia ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
-
Kueleza chimbuko la Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
-
Kubaini mchango wa Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar katika kujenga umoja, mshikamano na maadili miongoni mwa Wazanzibari
-
-