Historia ya Tanzania na Maadili (New) Form 1 Syllabus

    1. Kuelezea chimbuko la jamii za Kitanzania na maadili yake
      1. Kueleza asili ya jamii za Kitanzania (Wabantu, Wanilo, Wakushito, Wakichembe)
      2. Kubaini shughuli mbalimbali za makundi ya asili ya jamii za Kitanzania
      3. Kueleza maadili ya jamii za asili ya Kitanzania
    2. Kumudu maarifa na ujuzi wa maadili na urithi wa jamii za Kitanzania
      1. Kuchambua maadili na urithi wa jamii za Kitanzania
      2. Kueleza matendo ya msingi yanayokuza na kulinda maadili na urithi wa jamii za Kitanzania
    3. Kutumia maarifa na ujuzi wa historia na urithi kubuni fursa mbalimbali zilizopo katika jamii za Kitanzania
      1. Kubaini fursa mbalimbali zilizopo kwenye urithi wa jamii za Kitanzania
      2. Kueleza namna fursa zilizopo kwenye urithi wa jamii za Kitanzania zinavyoweza kutumika kukuza uchumi binafsi na jamii
      3. Kueleza njia mbalimbali za kutunza urithi wa jamii za Kitanzania
    4. Kubaini fursa mbalimbali za kujenga ushirikiano na kukuza uchumi wa kitaifa
      1. Kuainisha shughuli mbalimbali za kujenga ushirikiano na kukuza uchumi wa Taifa
      2. Kufafanua namna shughuli mbalimbali zinavyochangia kujenga ushirikiano na kukuza uchumi wa Taifa
    1. Kuchambua mifumo ya kijamii (elimu, afya, utamaduni) iliyokuza na kuendeleza maadili ya jamii za Kitanzania kabla ya ukoloni
      1. Kubaini mifumo ya kijamii ya Tanzania kabla ya ukoloni
      2. Kueleza mifumo ya kijamii ya Tanzania ilivyokuza maadili kabla ya ukoloni
    2. Kuchambua mifumo iliyokuza na kuendeleza uchumi na siasa katika jamiii za Kitanzania kabla ya ukoloni
      1. Kubaini mifumo ya kiuchumi na kisiasa katika jamii za Kitanzania kabla ya ukoloni
      2. Kueleza jinsi mifumo ya kisiasa na kiuchumi ilivyokuza na kuendeleza shughuli za kiuchumi na kisiasa kabla ya ukoloni
      3. Kufafanua uhusiano kati ya jamiii za Kitanzania na za Mashariki ya Kati, Mashariki ya Mbali na Ulaya katika kuendeleza shughuli za kiuchumi na kisiasa kabla ya ukoloni
      4. Kutathmini mchango wa mifumo ya kisiasa na kiuchumi katika kukuza maadili ya jamii za Kitanzania kabla ya ukoloni
    3. Kutathmini vichocheo vya mabadiliko ya sayansi na teknolojia katika jamii za Kitanzania kabla ya ukoloni
      1. Kueleza hali ya sayansi na teknolojia katika jamii za Kitanzania kabla ya ukoloni
      2. Kubaini vichocheo vya mabadiliko ya sayansi na teknolojia katika jamii za Kitanzania kabla ya ukoloni