Kiswahili Darasa la VI Syllabus

    1. Kusoma kwa Mazoezi (habari ndefu isiyozidi maneno 600 na kusoma nambari za milango sita (100,000-999,999))
      1. Kuainisha alama za uandishi
      2. Kubainisha nambari na maneno ya nambari
      3. Kusoma nambari na maneno ya nambari kwa kasi inayostahiki
      4. Kusoma habari kwa kuzingatia alama za uandishi
    2. Kusoma kwa Ufahamu habari ndefu isiyozidi maneno (600) (Udhalilishaji)
      1. Kueleza taratibu za usomaji
      2. Kubainisha msamiati uliyomo kwenye habari
      3. Kuchambua habari mbali mbali
    3. Ufupisho
      1. Kueleza dhana ya ufupisho
      2. Kufafanua hatua za ufupisho
      3. Kufupisha aya
    4. Maktaba
      1. Kuainisha aina za vitabu na machapisho yanayopatikana maktaba
      2. Kubainisha matumizi ya katalogi
      3. Kuelezea tafauti ya upatikanaji wa taarifa za kusoma katika maktaba
    1. Imla (isiyozidi maneno mia moja na ishirini (120))
      1. Kubainisha matumizi ya alama za uandishi
      2. Kuandika imla kwa kuzingatia alama za uandishi na kasi inayokubalika
    2. Insha
      1. Kuainisha vipengele vya insha
      2. kujadili hatua za uandishi wa insha
      3. Kuandika insha kwa kuzingatia alama za uandishi
    3. Barua Rasmi
      1. Kueleza aina za barua rasmi
      2. Kufafanua vipengele vya barua rasmi
      3. Kuandika barua rasmi kwa kuzingatia hatua
    4. Matangazo ya Biashara
      1. Kubainisha vipengele vya uandishi wa matangazo ya biashara
      2. Kuelezea vipengele vya matangazo ya biashara
      3. Kuandika matangazo ya biashara
    5. Nambari za Milango Sita (100,000-999,999)
      1. Kuainisha matumizi ya kituo kidogo katika uandishi wa nambari za milango sita
      2. Kubainisha nambari za milango sita na maneno ya nambari
      3. Kulinganisha nambari na maneno ya nambari kwa kuzingatia kituo kidogo
    1. Ngeli (N-N na U-N)
      1. Kubainisha majina
      2. Kuonesha viambishi vya umoja na wingi
      3. Kupanga majina katika makundi ya ngeli
    2. Aina za Maneno (Vielezi (E) na Vihisishi (I))
      1. Kueleza dhana ya vielezi na vihisishi
      2. Kuanisha vielezi na vihisishi katika sentensi
      3. Kufafanua aina za vielezi na vihisishi katika sentensi
      4. Kutumia vielezi na vihisishi katika utungaji wa sentensi
    3. Kauli za Vitenzi (Kutendea na Kutendana)
      1. Kubainisha kauli za kutendea na kutendana katika vitenzi
      2. Kutafautisha kauli za kutendea na kutendana
      3. Kubadilisha kauli za vitenzi
    4. Uundaji wa Maneno (Uambishaji)
      1. Kuelezea dhana ya viambishi
      2. Kubainisha viambishi awali na viambishi tamati katika maneno
      3. SKutumia viambishi katika uundaji wa maneno
    1. Misimu
      1. Kuelezea dhana ya misimu
      2. Kubainisha misimu inayotokana na mazingira yake
      3. Kujadili matumizi ya misimu
      4. Kutumia misimu katika mawasiliano
    2. Rejista
      1. Kuelezea dhana ya rejista
      2. Kujadili muktadha wa matumizi ya rejista
      3. Kufafanua matumizi ya rejista
    3. Utata
      1. Kueleza dhana ya utata
      2. Kubainisha sentensi zenye utata
      3. Kufafanua sababu za utata katika neno na sentensi
      4. Kujadili njia za kutatua utata
    1. Utamaduni wa Mswahili
      1. Kufafanua vipengele vya utamaduni wa Mswahili
      2. Kuelezea mambo ya kuigwa yanayotokana na utamaduni wa Mswahili
      3. Kujadili mambo yanayopotosha utamaduni wa Mswahili
    2. Kuimarisha Utamaduni Wetu
      1. Kubainisha njia za kuimarisha utamaduni wetu
      2. Kuelezea faida za kuimarisha utamaduni wetu
      3. Kujadili hasara za kuharibu utamaduni wetu
    3. Utamaduni wa Kigeni (Nje ya Zanzibar)
      1. Kubainisha vipengele vya utamaduni wa kigeni
      2. Kueleza athari za utamaduni wa kigeni
      3. Kujadili njia za kuepuka athari za utamaduni wa kigeni
    1. Utenzi
      1. Kuelezea dhana ya utenzi
      2. Kubuni utenzi wa beti nne
      3. Kughani utenzi
      4. Kuandika utenzi wa beti nne
    2. Misemo
      1. Kubainisha dhana ya misemo
      2. Kufafanua misemo katika matini
      3. Kutumia misemo katika mazungumzo