<strong>Ujasiriamali</strong>
Ujasiriamali
Ujasiriamali
Ujasiriamali
Maana ya ujasiriamali
Ujasiriamali
Kwa mtazamo wa kiuchumi, ujasiriamali ni sehemu ya vizalisha mali katika nchi. Vizalishia mali vingine ni ardhi, nguvu kazi na mitaji. Ujasiriamali sio tukio la mara moja bali ni mchakato mrefu.
- Ni mchakato wa kuweka pamoja mawazo na rasilimali (watu, fedha, vifaa nk) ili kuanzisha, kusimamia na kuendeleza biashara
- Ni mchakato wa kuwa tayari kukabiliana na vihatarishi (risks) kwa uangalifu bila kuogopa
- Ni mchakato wa kuelekea kutimiza ndoto za kujiajiri
- Ni mchakato wa kutafuta, kuona na kuzitendea haki fursa bila kuogopa changamoto
Ujasiriamali:
- Unahusu kutafuta na kuona fursa za uzalishaji mali
- Huweza kufanywa na yeyote, popote, wakati wowote
- Unahitaji; Udhubutu, Ubunifu, Kujituma na Kuwa tofauti
Mjasiriamali huleta pamoja vizalishia mali hivi na kusababisha uzalishaji, usambazaji na utumiaji wa bidhaa na huduma. Mjasiriamali hujiajiri na kuajiri wengine badala ya kuajiriwa. Mjasiriamali ni mtengeneza ajira sio mtafuta ajira.
Mjasiriamali
- Ni moja kati ya vizalishia mali (factors of production) muhimu sana
- Huwa tayari kwa mabadiliko na kunyumbuka wakati wowote
- Huona fursa pale wengine wasipoona chochote
- Huona fursa pale wengine wanapoona changamoto na vitisho: Tizama Video ya Mende kutoka Ngowi TV (www.ngowitv.co.tz): http://www.ngowitv.co.tz/mende-anapogeuka-kuwa-rasilimali
- Huona na kuibua fursa katika matatizo na changamoto za watu na jamii kwa ujumla
- Hutafuta rasilimali, kuziweka pamoja, kuanzisha biashara na kufanya vitu vitokee
- Hukabiliana na viatarishi (risk taker)
- Huwa na mtizamo wa mafanikio
- Hujiamini
- Huzingatia mipango na malengo
- Huwa na ubunifu na utundu
- Hakati tama
- Anajituma
- Ana nguvu kubwa ya mwili na akili (inatakiwa nguvu ya roho pia)
- Ana fikiria chanya
- Anapenda kuanzisha na kukamilisha mambo/biashara
- Anaweka ratiba ya mambo muhimu ya kufanya kila siku, juma, mwezi etc
Mambo Muhimu Katika Ujasiriamali
- Ni suala la kuamua kuanzisha na kukuza biashara yajo na kuwa mvumilivu
- Ni juu ya kuwa na biashara yako mwenyewe, kujiajiri na kuajiri wengine
- Yeyote anaweza kuwa mjasiriamali bila kujali umri, jinsia, rangi, elimu nk
- Ni lazima mjasiriamali kupangilia mambo na sio kukurupuka
- Ni vizuri kwa mjasiriamali kuwa na mitandao (mfano whatsapp groups)
- Ni lazima kuwa na ndoto, maono na njozi kubwa kuhusu biashara
- Ni lazima kuweka malengo na kuwa tayari kuanza
Umuhimu wa kuwa mjasiriamali
Umuhimu wa kuwa mjasiriamali
Kuna umuhimu mkubwa sana kwa watu wengi iwezekanavyo kuwa wajasiriamali. Sababu kuu ni pamoja na hali halisi ya soko la ajira
- Soko la ajira rasmi ni finyu hivyo sio rahisi vijana kuajiriwa
- Ujasiriamali (kujiajiri) ni jambo la lazima sio chaguo. Ni plan A sio plan B)
- Vijana ni nguvu kazi muhimu na kubwa kwa taifa. Wakiachwa bila kuajiriwa au kujiajiri huweza kuwa bomu la muda na ni fursa iliyopotea
- Vijana wana nguvu, ubunifu, utundu na udhubutu. Vyote hivi vinahitajika sana katika ujasiriamali. Wasipotumia sifa hizi kuwa wajasiriamali itakuwa ni fursa iliyopotea
- Umuhimu na mvuto wa ujasiriamali umeongezeka sana katika miaka ya karibuni hasa baada ya mageuzi ya uchumi Tanzania katikati ya miaka ya 1960. Katika mazingira ya uchumi yaliyobadilika na kutambua, kuheshimu, kukumbatia na kuunga mkono juhudi mbalimbali za ujasiriamali, ni budi watu kutumia fursa ya mabadiliko haya kuwa wajasiriamali
- Hali ya soko la ajira na ujasiriamali: Soko la ajira rasmi ni finyu. Ujasiriamali (kujiajiri): Jambo la lazima sio chaguo (Plan A not Plan B)
Mjasiriamali Mzuri
Sifa za Mjasiriamali Mzuri
Katika tasnia ya ujasiriamali lengo sio tuu kuwa mjasiriamali bali kuwa mjasiriamali mzuri, mahiri, wa mfano na mwenye mafanikio. Kusudi kufikia lengo hili, zipo sifa na tabia za msingi ambazo mjasiriamali anapaswa kuwa nazo. Hizi ni pamoja na hizi zifuatazo:
- Msukumo kutoka ndani na sio kulazimishwa
- Kuwa na maono na njozi kubwa kibiashara
- Kuwa tayari kukamilisha na kuisho maono na njozi za biashara husika
- Kuwa tayari kupambana na changamoto na vikwazo
- Kuwa na hamu ya kukutana na kufanyia kazi vihatarishi (risk)
- Kutoogopa kuanguka na kushindwa
- Kujua kuwa ukubwa na ufaulu haupo katika kutokuanguka bali katika kuinuka kila mara tunapoanguka
- Kuwa na mawazo mengi sana ya biashara
- Kuwa mvumilivu
- Kuwa na udhubutu na utayari wa kuanza na kukuza biashara
- Kuwa tayari kuchukua majukumu
- Kuwa na fikra chanya sio hasi
- Kuwa tayari kufanya maamuzi hata kama ni magumu
- Kufanya kazi kwa bidii maana ujasiriamali sio lelema
- Kuwa tayari kuanzisha biashara mpya baada ya kukamilisha za awali
- Kuweza kutumia rasilimali (hasa fedha) vizuri na kwa nidhamu ya hali ya juu
- Morari wa kushinda
- Hamu ya kujiajiri na kuajiri wengine
- Kuwa mtengeza ajira na sio mtafuta ajira
- Utayari wa kuwajibika kwa maamuzi ya biashara anayofanya
- Kuona kuwa kila kitu kinawezekana kama kitafanywa sawasawa
- Ni mtafuta na mwona fursa 7
- Ni mbunifu, mtundu, hujitofautisha
- Kuwa na hamu kubwa sana ya mafanikio
- Hujiongoza na hasubiri kusukumwa
Jiulize Maswali Haya Kujua Kama Wewe ni Mjasiriamali Mzuri
Kama jibu ni ndiyo, unaweza kuwa mjasiriamali mzuri. Kama ni hapani, huenda wewe sio mjasiriamali mzuri. Uzuri ni kwamba unaweza kufanyia maboresho mapungufu yako na kuwa mjasiriamali mzuri. Jiulize
- Unamaliza majukumu unayojipangia kila wakati?
- Unajipa muda maalumu (deadline) wa kumaliza uliyojipangia?
- Unaweka nguvo zote katika majukumu uliyonayo kwa wakati husika?
- Unamaliza angalau jambo moja muhimu katika biashara yako kila siku?
- Unatumia muda vizuri?
- Unaweka vipaumbele na kuvifuata katika maisha na biashara yako?
- Una uwezo wa kupambana na changamoto na kutatua matatizo au unayakimbia?
- Una ubunifu, utundu, udhubutu, uvumilivu na utayari katika biashara?
- Upo tayari kuomba msaada wa kitaalamu?
- Unaweza kufanya zaidi ya jambo moja vizuri kwa wakati mmoja (multi-tasking)?
- Hukatishwi tamaa?
- Uko tayari kuendelea sio kwa sababu ni rahisi bali kwa sababu ni muhimu?
Fursa za Ujasiriamali
Fursa za Ujasiriamali
Neno fursa limekuwa kati ya maneno makuu katika tasnia ya biashara na uchumi kwa ujumla na mahususi katika mazungumzo ya kijasiriamali. Watanzania wanasisitizwa kutafuta na kuchangamkia fursa katika muktadha tofauti. Katika makala haya mitizamo mbalimbali kuhusu fursa inatolewa kwa lengo la kupanua mitizamo ya kawaida kwa wasomaji.
Tuelewe fursa kihistoria
Uchambuzi wa hali na wingi wa fursa Tanzania utakuwa na maana zaidi kama tutaelewa historia ya uchumi na biashara Tanzania. Fursa zinazoonekana katka miaka ya leo lazima zionekana kama matokeo ya mabadiliko makubwa sana ya kiitikadi ya kisiasa na kiuchumi duniani kiujumla na Tanzania kimahususi. Hali ya fursa za kijasiriamali Tanzania inaweza kugawanywa katika vipindi vikuu viwili. Hivi ni kati ya mwaka 1967 na miaka ya katikati ya 1980 na hadi mwanzoni mwa 1990. Kipindi cha pili ni kile cha kuanzia katikati ya miaka ya 1980 hadi miaka ya leo. Katika kipindi cha kwanza fursa za ujasiriamali na nafasi ya kuziweka katika vitendo na kuzitendea haki zilikuwa finyu. Hii ni kwa saabu ya mfumo wa Ujamaa ambao haukutoa nafasi kubwa sana kwa mambo ya ujasiriamali. Sekta binafsi haikuwa na nafasi kubwa katika uchumi kama tunavyoijua leo.
Katikati ya miaka ya 1980 mpalka sasa kumekuwepo fursa nyingi zaidi na nafasi na mazingira ya kisera, kisheria na kiudhibiti ya kutendea fursa hizi haki. Ni zama zinazokubali zaidi ujasiriamali na nafasi ya sekta binafsi katika uchumi. Mabadiliko makubwa ya kisiasa na kiuchumi yaliyoanza katikati ya miaka ya 1980 yaliwezesha yote haya kutokea. Historia hii ya fursa lazima ieleweke na kuheshimiwa vizuri.
Aina mbalimbali za fursa
Ni vizuri kutambua kuwa fursa zipo za aina mbalimbali. Hivyo wadau wa fursa lazima wajue wanazungumzia na kushughulikia fursa za aina ipi kimahususi. Zipo fursa kubwa na ndogo, fursa za muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu na za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja. Kila aina ya fursa inapaswa kushughulikiwa kwa namna tofauti ili kupata matokeo yanayotazamiwa. Fursa za muda mfupi zikishughulikiwa kama vile zingekuwa za muda mrefu tunaweza kukosa matokeo yanayostahili. Kinyume chake pia ni kweli kwa fursa za muda mrefu kushughulikiwa kama za muda mfupi.
Fursa ziko wapi
Kimsingi fursa zinapaswa kuwa katika mawazo yetu. Mitizamo, maono na njozi za kiujasiriamali ndio hutofautisha anayeona na asiyeona fursa. Uwezo wa kuona, kujenga na kutekeleza wazo la biashara kutoka hutoka katika fikra. Uwezo wa kijasiriamali ndio hufanya fursa kuwepo na kuonekana. Hivyo fursa za kiujasiriamali lazima zitafutwe na kujengwa katika fikra na mawazo yetu. Hili likishatokea ndipo fursa zitaonekana na kutendewa haki nje ya mawazo na fikra zetu. Kimsingi fursa zipo pale penye maupungufu ya mahitaji uhitaji. Uwezo wa kubaini mapungufu haya na kuyatendea haki ndio ujasiriamali wa kutambua fursa.
Mifano ya vyanzo vya fursa
Vyanzo vya fursa vipo vingi. Ni bahati mbaya kuwa wengi hufikiri kuwa vyanzo hivi vya fursa ndio fursa zenyewe. Katika kila chanzo cha fursa kuna fursa nyingi kuliko macho ya wanaotizama chanzo husika. Fursa huonekana kutegemea na mtizamo, uzoefu, maono, elimu na utundu wa mtizamaji wa chanzo cha fursa. Wapo wanaoona fursa nyingi mbalimbali katika malengo endelevu ya dunia, katika dira ya maendeleo ya taifa, katika sera na mikakati, katika miradi mbalimbali, katika bajeti, katika hali ya sayansi na teknolojia, katika majanga, matukio na mambo mengine katika maisha ya kila siku. Kati ya fursa nzuri ya kuwa mjasiriamali ni pamoja na hali ya kukosa ajira inayopelekea ari kubwa ya kujiajiri, malipo na mafao duni yanayopelekea mtu kuanza biashara zake ili kukabiliana na ugumu wa maisha na kadhalika.
Nini cha kufanya
Kwa anayehitaji kutendea fursa haki, ni lazima kubaini vyanzo vya fursa mbalimbali. Ni lazima kufuata fursa badala ya kusubiri fursa zikufuate kwa sababu hazitafanya hivyo. Ni muhimu kutokubali kupitwa na fursa hivyo ni lazima kukaa tayari wakati wowote. Kuweza kuona na kutedea fursa haki inahitaji kuaa kimkakati wakati wowote. Ni lazima kuwa na udhubuti wa kujaribu bila kuogopa kuchekwa au kushindwa.
Tafiti zitaonyesha kuwa yule ambaye hajawahi kushindwa ni yule ambaye hajawahi kujaribu. Katika kuna na kutendea fursa haki ni lazima kuwa tofauti, kuwa mbunifu na mtundu na kufikiria tofauti na wengne. Inabidi kuwa wewe bila kujali wengine watasema nini. Ili kuhakikisha fursa hazipotei ni lazima kuanza kuzifanyia kazi fursa zilizopo mara moja bila kusubiri. Hata hivyo ni lazima kujiridhisha kwanza kabla ya kuishugulikia fursa husika.
Mambo ya kufahamu
Katika kutafuta na kutendea fursa haki kuna mambo mengi ya kufahamu. Haya ni pamoja na ukweli kuwa kutakuwepo kuanguka kwingi. Kuanguka sio mwisho wa kupata na kutendea fursa haki. Kutokuinuka baada ya kuanguka ndio utakaokuwa mwisho wa kupata na kutendea fursa haki. Hivyo ni muhimu kujua kuwa tutaanguka lakini ni muhimu zaidi kujua kuwa kila tuanpoanguka yatupasa kunuka tukiwa wakubwa, warefu na wenhye nguvu zaidi.
Ni lazima kujiinua kutoka katika maanguko yako kisha kuendelea mbele. Ukisubiri kuinuliwa unaweza kusubiri sana. Ukubwa wetu kama wajasiriamali watafuta fursa haupaswi kupimwa kwa kutokuanguaka bali kwa kuinuka kila tunapoanguka. Vivyo hivyo, ukubwa wa wanaopaswa kuwasaidia na kuwainua wajasiriamali wanaotafuta na kutendea fursa haki haupaswi kuwa katika kuwasukumiza na kuwadidimiza wajasiriamali hawa chini bali katika kuwainua katika safari yao ya kutafuta na kutendea fursa haki. katika kuwasukumiza na kuwadidimiza wajasiriamali hawa chini bali katika kuwainua katika safari yao ya kutafuta na kutendea fursa haki.
Katika kutafuta na kutendea fursa haki, ni muhimu kujua kuwa biashara yako inaweza kufa lakini kumbuka nahodha mzuri na makini hazami na meli yake. Usikubali kuzama na biashara yako. Ikizama wewe lazima utafute namna ya kuelea na kuanza tena upya. Utapata hasara lakini endelea baada ya kujifunza kutokana na maanguko na hasara zako na za wengine. Tizama na tafuta kinachowezekana katika kinachoonekana kutowezekana. Tizama kilichobaki na anza nacho badala ya kulalamikia kisichopo na kinachokasoro. Ni lazima kuwa na fikiria chanya sio hasi. Ni lazima kuvuka mstari na mpaka wa uzoefu na kufanya mambo mapya na mambo kwa namna mpya.
Msisitizo Kuhusu Fursa
Nini Cha Kufanya Kuhusu Fursa?
- Fuata fursa usisubiri fursa zikufuate; Usikubali fursa zikupite
- Kaa kimkakati uwe tayari muda wowote
- Tambua na chambua fursa; Zitendee haki vizuri; Thubutu, jaribu
- Kuwa tofauti, kuwa mbunifu; kuwa wewe/mwenyewe bila kujali watasema nini (Sting: Be yourself no matter what they say)
- Anza mara moja usisubiri lakini jiridhishe kwanza;
- Anguka na inuka; Jiinue kutoka katika maanguko yako kisha endeleambele, ukubwa haupaswi kupimwa kwa kutokuanguaka bali kwa kuinuka kila unapoanguka;
- Biashara yako inaweza kufa lakini nahodha mzuri hazami na meli yake – usizame na biashara yako
- Pata hasara na endelea lakini calculated risks na jifunze kutokana na maanguko na hasara
- Tizama na tafuta kinachowezekana katika kinachoonekana kutowezekana
- Tizama kilichobaki na anza nacho; Sio kisichopo na kinachokasoro: Fikiria chanya sio hasi
- Kuwa jasiri
- Thubutu
- Vuka mstari/mpaka wa uzoefu
- Jifunze kwa walijiojiajiri
- Jifunze kwa walioanguka
- Jifunze kwa waliofaulu
Kukazia Maarifa Kuhusu Mambo Makuu Kuhusu Fursa Tanzania
Zipo fursa za aina mbalimbali
- Kubwa na ndogo
- Za muda mfupi
- Za muda wa kati
- Za muda mrefu
Tuelewe fursa Tanzania kihistoria: Mabadiliko ya sera/itikadi Kipindi cha 1967 – mid 1980s:
- Fursa zilikuwa finyu
- Ujasiriamali haukuwa na nafasi kubwa
Katikati ya miaka ya 80 mpalka sasa fursa ni nyingi zaidi
- Sekta binafsi, uchumi wa soko na ujasiriamali vinakubalika zaidi
- Kuna ushirikishwaji wa sekta binafsi katika fursa (Mfano fursa katika bomba la mafuta kutoka Uganda hadi Tanzania).
- Kuna nguvu na msukumo zaidi kutoka kwa wadau wa ujasiriamali
Mipango mbali mbali ya Biashara
Mpango wa Biashara
Ili kufanya vizuri katika ujasiriamali ni lazima kuwa na mpango wa biashara. Mpango wa biashara ni andiko kuhusu biashara unayopanga kufanya. Huitajiwa na wajasiriamali wote bila kujali ukubwa. Kwa bahati mbaya sana, wajasiriamali wengi hasa wadogo na hata wa kati hawana mpango biashara. Hii sio afya kiujasiriamali.
Kwanini Kuwa na Mpango wa Biashara
Kuna sababu mbalimbali za msingi za kuwa na mpango wa biashara. Hizi ni pamoja na zifuatazo.
- Utakusaidia kufikiria
- Vyomb vya fedha vitauhitaji
- Wawekezaji ktk biashara yako watauhitaji iv) Husaidia kupata mawazo ya kuendeleza biashara
Nini Kiwekwe/kiandikwe Katika Mpango Mzuri wa Biashara
Mpango mzuri wa biashara unatakiwa kuwa na baadhi ya mambo ya msingi. Haya ni pamoja na yafuatayo:
i) Maelezo kuhusu kampuni
- Wazo kuu la biashara - concept
- Maelezo ya bidhaa na huduma husika
- Wateja: Ni kina nani na wapo wapi
- Mfumo wa usambazi wa bidhaa na huduma unazoshughulika nazo
- Masuala ya mazingira: Biashara yako ni rafiki kwa mazingira kwa namna gani na kwa kiasi gani?
- Timu ya manegimenti/utawala: Kina nani wapo katika utawala/menejimenti ya biashara husika? Wana sifa gani?
- Sehemu biashahara ilipo: Nchi, mkoa, wilaya, kata, kijiji etc. Toa mawasiliano yako hasa simu na barua pepe
ii) Bidhaa na Huduma Husika
- Elezea ufahamu wako wa kina wa bidhaa na huduma husika
- Elezea kwa kina hatua zote za uzalishaji
- Elezea kwa kina mahitaji ya bidhaa na huduma
- Elexea kwa kina utofauti na ushindani wa biashara yako
- Pambanua vikwazo/mahitaji ili kuingia sokoni
- Elezea kwa kina gharama husika
iii) Hali ya Sekta
- Ukubwa za sekra na ukomavu wake
- Ushindani ukoje? Washindani wako ni kina nani na wanashindana nawe kwa lipi? Je ni bei, ubora, mitandao, huduma bora, ukubwa na ukongwe sokoni?
- Ukuaji: Seka inakua kwa kasi gani kwa mwaka
- Mabadiliko: Mabadiliko gani makubwa yametokea katika sekta?
- Hali ya kifedha : Je ni sekta yenye fedha nyingi au kidogo?
- Teknologia: Teknolojia gani inatumika na kwa sasa teknojia ya hali ya juu zaidi ni ipi?
- Sera, sheria na udhibiti wa serikali
iv) Uchambuzi wa Soko
Ainisha soko lako
- Kidemografia
- Kijiografia
- Utaratibu wa manunuzi
- Tabia za manunuzi – consumer behaviour
Soko mahususi: Market niche
Masuala ya bei
v) Ushindani
- Elezea ushindani ulivyo
- Unatarajia kumili soko asilimia ngapi
- Kuna vikwazo/mahitaji gani kuingia sokoni
- Kuna fursa gani kungia sokoni
vi) Masuala ya Usimamizi
- Masuala ya msingi kuhusu waanzilish wa biashara: Elimu, uzoefu, taarifa binafsi nk
- Filosofia ya kampuni/waanzilishi
- Mfumo wa kisheria wa kampuni
- Mfumo wa uongozi
vii) Mipango ya Fedha
- Mtaji unaohitajika: Aina, kiasi na kwa ajili gani
- Maoteo ya mtiririko wa fedha: Cash flow projection
- Faina inayotegemwea
- Hasara inayotegemewa
- Hasara kuwa sawa na faida: Break even
- Muda wa uwekezaji kujilipa§ Vyanzo vya mtaji
viii) Mipango ya Ukuaji
- Malengo ya muda mrefu
- Kujipanua zaidi§ Kuongeza umiliki wa soko
- Alama/malengo muhumu ya kufikia
- Kuwa kampuni ya umma/soko la hisa
- Kuuza kampuni/biashara/nembo§ Kununua wengine
- Kuungana na wengine§ Kufunga biashara
Vyanzo mbalimbali vya Fedha
Mitaji: Vyanzo vya Fedha
Biashara katika ujumla wake na wajasiriamali kimahususi huitajo fedha katika hayua mbalimbali za kuanzisha, kundeleza na kukuza biashara. Fedha huitajika kwa shughuli mbalimbali kibiashara na kijasiriamali. Hizi ni pamoja na:
- Kununua, kujenga au kukodisha sehemu ya kufanyia biashara/ujasiriamali
- Kununua au kukosisha vitendea kazi kama vile mashine na vyombo mbalibali kutegemeana na aina ya biashara
- Kulipa wafanyakazi
- Kulipa nishati kama umeme na maji
- Kwa ajili ya usalama/ulizi
- Kwa ajili ya usafi
- Kujitangaza
- Kulipia kodi, leseni na vibali mbalimbali
Vyanzo Vya Fedha/Mitaji
Kwa kawaida fedha za kuanzisha, kuendesha na kukuza biashara/ujasiriamali hutoka katoka vyanzo mbalimbali. Hivi ni pamoja na vifuatavyo
i) Vyombo vya fedha
- Hivi ni pamoja na mabenki na vyombo vya fedha visivyo mabenki. Katika mabenki ni vizuri kujua kuwa kuna benki za biashara na benki za maendeleo. Benki za biashara hutoa mikopo ya muda mfupi na yenye riba kubwa zaidi kuliko benki za maendeleo
ii) Akiba binafsi
- Wajasiriamali huweza kuwekeza sehemu ya akiba zao au akiba yote katika biashara
iii) Fedha kutoka kwa watu mbalimbali tandaoni yaani Crowdfunding
iv) Ndugu, jamaa na marafiki
- Mjasiriamali huweza kupata mtaji kutoka kwa ndugu, jamaa na marafiki. Huweza kuwa mkopo au zawadi
v) Kuwekeza Faida Katika Biashara
- Hiki ni chanzo cha fedha kwa wajasriamali ambao tayari wanafanya biashara
- Sehemu ya faida huwekezwa katika biashara badala ya kuitumia kwa njia nyinginezo kama starehe na matumizi mengine yasiyo ya kibiashara
- Faida katika biashara iliyopo na inayoendelea huweza kutumika kuwekeza katika biashara mpya kama mtaji wa kuanzia
- Ni muhimu sana kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha ili chanzo hiki kiweze kuwa mojawapo ya vyanzo vizuri vya mtaji
vi) Mitaji Kutoka Masoko ya Hisa
- Hiki ni chanzo kinachotumika zaidi na kampuni kubwa kuliko ndogo
- Mitaji hupatikana kutoka katika soko la hisa kama lile la Dar Es Salaam
- Kampuni huandaa andiko la kina kuhusu biashara inayofanya ikionyesha mali, madeni, mauzo, faida, hasara, wamiliki nk. Lengo ni kuwa na uwazi kusudi watakaotaka kununua hisa wawe na taarifa nzuri na za kina kabla ya kufanya maamuzi
- Kampuni inapouza hisa inapunguza umiliki wake lakini inapata fedha za kuwekeza
- Soko la mitaji la Dar Es Salaam lina dirisha maalumu kwa kampuni ndogo na za kati kuuza hisa zake
vii) Ruzuku Kutoka Vyanzo Mbalimbali
- Ruzuku sio mkopo hivyo hairejeshwi
- Ruzuku hutolewa na taasisi mbalimbali
- Kwa kawaida watoa ruzuku hukaribisha maombi ya ruzuku kupitia maandiko ya kiushindani
- Wanaoshinda hupata ruzuku ambayo husaidia katika uwekezaki na ukuzaji wa biashara
Mambo ya Kufikiria Kabla ya Kukopa Fedha Kwaajili ya Mtaji
Kuna mambo kadhaa ya msingi yanayopaswa juzingatiwa na mjasiriamali kabla ya kukopa fedha kwa ajili ya mtaji. Mambo haya ni pamoja na yafuatayo.
- Kopa kiasi unachohitaji sio kiasi ambacho mkopeshaji anataka kukukopesha.
- Epuka kuchukua mkopo usiohitaji
- Epuka kuchukua mkopo wenye mitego na masharti usiyoyaweza
- Epuka mikopo yenye gharama zilizojificha. Uliza na kubaliana na mkopeshaji kuhusu garama ZOTE ikiwemo zile za kiutawala na kupitia mkopo wako
- Jua masharti yote ya mkopo na jiulize kama unayamudu na kama huyamudu maana yake ni nini. Masharti haya ni pamoja na haya:
i) Mali za kuweka rehani
- Mali gani itatakiwa? Inayohamishika au/na isiyohamishika?
- Hizi mali unazo? Uko tayari ‘kuzipoteza’ kama ukishindwa kulipa deni?
ii) Riba
- Riba ni asilimia ngapi ya mkopo?
- Biashara yako inalipa kiasi cha kuweza kumudu riba hii? Lazima faida yako iwe kubwa kuliko riba
- Inatozwa kwa kipindi gani? (Siku, juma, mwezi, mwaka)?
- Wakopeshaji wengine wanatoza riba kiasi gani?
- Kwa nini hukopi kwenye vyanzo vyenye riba ndogo zaidi?
iii) Udhamini/mdhamini
- Utahitajika kuwa na mdhamini?
- Kama unahitaji mdhamini, je unaye na ni nani? (Ndugu, jamaa, marafiki, mwajiri, serikali za mitaa nk?)
iv) Muda wa malipo/marejesho
- Utatumia muda gani tangu kukopa uwe umemaliza marejesho?
v) Ratiba ya malipo/marejesho
- Marejesho yatafanywa kila baada ya muda gani?
- Yatafanyika kila tarehe ngapi?
vi) Kiasi cha malipo/marejesho
- Kila unapolipa mkopo utalipa kiasi gani?
- Mapato ya biashara yako yanatosha kutoa kiasi hiki cha marejesho bila kuathiri biashara?
vii) Adhabu ukishindwa kutimiza masharti
- Uliza nini kitatokea kama utashindwa kufanya marejesho kwa muda na kiasi kinachotakiwa?
- Uko tayari kulipa adhabu hii?
Uchambuzi wa Miradi/Biashara
Uchambuzi wa Miradi/Biashara
Kabla ya kufanya mazoezi ya kuwekeza katika shughuli yeyote ya kiujasiriamlai ni lazima kufanya uchambuzi yakinifu na wa kina. Lengo ni kujiridhisha kuwa biashara tunayotaka kufanya ni sahihi na italipa. Hujaribu kupunguza uwezekano wa biashara kutofanikiwa; huakikisha kuwa mambo yote ya msingi yamezingatiwa kabla ya kuwekeza. Ni muhimu kufanya uchambuzi wa kina kuhusu mambo yafuatayo:
i) Uwezekano kitaalumu
- Kwa utaalamu na teknolojia iliyopo, inawezekana kutekeleza biashara unayofikiria?
- Kama huna hiyo teknolojia inayotakiwa, je inapatikana wapi, kwa gharama gani na masharti yapi?
ii) Uchambuzi wa kijamii
- Biashara yako inakubaika katika jamii?
- Biashara yako inalenga kutoa mchango gani katika jamii?
iii) Uchambuzi wa kifedha na biashara
- Garama zote za mradi/biashara ni kiasi gani?
- Mtaji unaotakiwa ni wa aina gani?
- Fedha
- Bidhaa
- Vifaa
- Jamii – mtaji jamii (social capital)
- Je mtaji kiasi gani unahitajika na kwa wakati gani?
- Mtaji utatoka wapi?
- Wewe unachangia kiai ani cha mtaji
- Ni yapi masharti ya kupata mtaji husika?
- Mradi utaanza kutengeneza fedha lini?
- Kabla hujaanza kutengezena fedha/faida utagaramia vipi mradi?
- Lini utaanza kutengeneza faida?
iv) Uchambuzi wa mazingira
- Biashara yako ni rafiki kwa mazingira?
- Biashara itachafua vipi mazingira? (Wanyama na mimea ardhini, majini na katika hewa?)
- Biashara itaungwa mkono na wana mazingira?
- Kama utachafua mazingira, garama za kuyasafisha ni ya nani na ni kaisi gani?
v) Uchambuzi wa masoko
- Fikiria masoko/uhitaji wa unachotaka kuwekeza
- Soko la bidhaa na huduma zako ni lipi?
- Soko lipo wapi na lina ukubwa gani?
- Soko linakua, limesimama au linapungua kwa kiasi gani kwa mwaka?
- Soko ni komavu au change?
- Yapi ni masharti na kanuni za kuingia sokoni?
- Ni soko la muda au la kudumu?
- Hali ya ushindani soko ipoje? (Soko hodhi? Soko shindani?)
vi) Uchambuzi wa ushindani
- Hali ya ushindani ikoje : Hodhi au ushindani?
- Washindani wako ni kina nani?
- Washindani wanashindana na wewe kwa jambo gani? Bei? Huduma nzuri? Uharaka wa kumfikia mteja? Ukubwa? Ujuzi?
- Utafanya nini kuendana/kupambana na kila mshindani wako?
- Wewe unataka kuwashinda washindani wako kwa lipi: Bei?; Ubora wa bidhaa/huduma? ; Uzoefu? Technolojia? etc
vii) Uchambuzi wa kisheria
- Unachotaka kufanya kinakubalika kisheria?
- Ni yapi matakwa ya kisheria katika kila jambo unalopanga kufanya?
- Mikataba gani itahitajika?
Namna ya Ujengaji Uwezo kwa Wajasiriamali
Ujengaji Uwezo kwa Wajasiriamali
Masuala Mengine Muhimu katika Ujasiriamali
Masuala Mengine Muhimu katika Ujasiriamali
Listening to this topic