Kiswahili
Ngeli Za Nomino
Kiswahili ni Lugha ya kibantu; inatumika kama lugha ya taifa au rasmi katika baadhi ya mataifa ya Afrika Mashariki na Kati kama vile Tanzania, DRC, Kenya, Burundi, Rwanda na Uganda. Hadi hivi sasa lugha ya Kiswahili inakadiriwa kuzungumzwa na watu zaidi ya milioni 60 duniani kote. Mataifa mengine ya Afrika yanayozungumza Kiswahili ni pamoja na Comoro, Zambia, Malawi na Msumbiji. Kiswahili pia kinazungumzwa katika baadhi ya nchi za Kiarabu kama vile Yemen, UAE n.k
Ngeli Za Nomino
Kuzielewa ya Ngeli
Upatanishi wa Kisarufi katika Sentensi
Fafanua upatanishi wa kisarufi katika sentensi
Ngeli ni vikundi vya majina ya Kiswahili. Ngeli za nomino ni utaratibu unaotumika kuweka nomino katika matabaka au makundi yanayofanana.
Example 1
Mfano:
- Maji yakimwagika hayazoleki
- Mayai yaliyooza yananuka sana
- Yai lililooza linanuka sana
- Maji liliomwagika halizoleki
Katika mifano hii tunaona kwamba sentensi a, b na c ziko sahihi wakati sentensi d sio sahihi, hii ni kwa sababu imekiuka upatanisho wa kisarufi. Kwa maana hiyo sentensi ‘a’ ipo katika ngeli ya YA-YA na senthensi b na c zipo katika ngeli ya LI-YA. Sentesi d sio sahihi kwa sababu nomino maji haina wingi, kwa hiyo haiwezi kuingia katika ngeli ya LI-YA. Kwa msingi huu ngeli za nomino huzingatia sana upatanisho wa kisarufi.
Jedwali lifuatalo huonesha ngeli za nomino kwa misingi ya upatanisho wa kisarufi.
| NGELI | UFAFANUZI | MIFANO |
| A-WA | Ngeli hii inahusisha majina ya viumbe hai kama vile wanyama, watu, wadudu, ndege n.k | Sungura mjanja ameumia, Sungura wajanja wameumia Mkuu anawasili |
| LI-YA | Majina yenye kiambaisha awali li- katika umoja na ya- katika wingi huingia katika ngeli hii | Jambia la babu limepotea, Majambia ya babu yamepatikana |
| KI-VI | Ni ngeli ya majina ya vitu visivyo hai, yanayoanza kwa KI- au CH- (umoja); na VI- au VY- (wingi). Pia ngeli hii hujumuisha majina ya vitu vingine katika hali ya udogo k.v, kijito, kilima | Chakula kimekwisha, Vyakula vimekwisha, Kijito kimekauka Vijito vimekauka |
| U-I | Huwakilisha majina ya vitu visivyo hai, yaanzayo kwa sauti M- (umoja) na MI(wingi). Pia majina ya baadhi ya viungo vya mwili huingia humu, kewa mfano mkono, mguu, mkia n.k | Mlima umeporomoka, Milima imeporomoka, Mkono umevunjika, Mikono imevunjika, Mto huu una mamba wengi, Mito hii ina mamba wengi |
| U-ZI | Hurejelea majina ambayo huanza kwa U- (umoja) na huchukua ZI- kama kiambishi kiwakilishi cha ngeli katika wingi. Majina yenye silabi tatu au zaidi hubadilishwa kwa wingi kwa kutoa sauti /u/' k.v ukuta-kuta. Majina ya silabi mbili huongezewa /ny/ katika wingi. k.v ufa - nyufa | Ukuta umebomoka, Kuta zimebomoka, Wimbo huu unavutia, Nyimbo hizi zinavutia, Ufa umeonekana, Nyufa zimeonekana |
| I-ZI | Hutumiwa kwa majina yasiyobadilika kwa umoja wala kwa wingi lakini huchukua viambishi viwakilishi tofauti: I- (umoja) na ZI- (Wingi). | Nyumba imejengwa, Nyumba zimejengwa, Salam imefika Salam zimefika |
| U-YA | Ngeli hii inajumuisha nomino ambazo zina kiambishi awali u- katika umoja na ma- katika wingi. | Ukuu umekuponza, Makuu yamekuponza, Unyoya unapepea, Manyoya yanapepea |
| KU | Majina yanayotokana na vitenzi yanayoanza na ku- (vitenzi-jina) | Kusoma kwako kumekusaidia, Kuchelewa kumemponza |
| PA/MU/KU- | Huonesha mahali | Amekaa pale palipo na wadudu wengi Amelala mule mulimojaa siafu. Amepita kule mbali |
Baadhi ya matumizi ya ngeli ni pamoja na haya yafuatayo:
- Hutumika kupanga majina ya lugha katika makundi yaliyoshikamana na kutofungamana kutokana na kigezo muhimu.
- Hutumika kutambulisha maumbo ya umoja na wingi katika majina na vivumishi.
- Hutumika katika upatanishi wa kisarufi katika sentensi.
- Hutumika katika kuonyesha uhusiano uliopo baina ya lugha za Kiswahili na lugha zingine.
Habari zenye Upatanishi wa Kisarufi
Andika habari zenye upatanishi wa kisarufi
Baadhi ya matumizi ya ngeli ni pamoja na haya yafuatayo:
- Hutumika kupanga majina ya lugha katika makundi yaliyoshikamana na kutofungamana kutokana na kigezo muhimu.
- Hutumika kutambulisha maumbo ya umoja na wingi katika majina na vivumishi.
- Hutumika katika upatanishi wa kisarufi katika sentensi.
- Hutumika katika kuonyesha uhusiano uliopo baina ya lugha za Kiswahili na lugha zingine.
Listening to this topic