Kiswahili

Uundaji Wa Maneno
♿ Accessibility: | | | |
Kiswahili ni Lugha ya kibantu; inatumika kama lugha ya taifa au rasmi katika baadhi ya mataifa ya Afrika Mashariki na Kati kama vile Tanzania, DRC, Kenya, Burundi, Rwanda na Uganda. Hadi hivi sasa lugha ya Kiswahili inakadiriwa kuzungumzwa na watu zaidi ya milioni 60 duniani kote. Mataifa mengine ya Afrika yanayozungumza Kiswahili ni pamoja na Comoro, Zambia, Malawi na Msumbiji. Kiswahili pia kinazungumzwa katika baadhi ya nchi za Kiarabu kama vile Yemen, UAE n.k

Uundaji Wa Maneno

Uundaji wa maneno ni ujenzi au uzalishaji au utengenezaji wa maneno mapya. Uundaji wa maneno mapya husaidia kuongeza msamiati katika lugha ili kukidhi mahitaji ya mawasiliano. Uundaji wa maneno mapya husababishwa na mabadiliko ya kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni na maendeleo ya kisayansi yanayotokea katika jamii. Kwa mfano tunayo maneno mapya, kama vile ufisadi, uwekezaji, ukeketaji, ujasiriamali na mengine mengi kutokana na mabadiliko ya kijamii.
Kutumia Uambishaji
Kubainisha Mofimu katika Maneno
Bainisha mofimu katika maneno
Uambishaji ni nini?
Uambishaji wa maneno ni kitendo cha kupata maneno kwa kubandika Mofimu kwenye kiini cha neno. Uambishaji hutokea kabla ya kiini cha neno au mzizi wa neno. Mfano kiini pig- unaweza kuunda maneno kama inapiga, anayepiga, mpigaji, amepigika nk.
Mofimu zinazopachikwa katika mizizi huitwa Viambishi
Aina za uambishi
Kuna aina mbili za viambishi;
  1. Viambishi awali:Hivi ni viambishi vinavyo pachikwa kabla ya kiini/mzizi wa kitenzi.Kwa mfano anaimba, viambishi awali vya kitenzi anaimba -imba- ni a- na-
  2. Viambishi tamati:Hivi ni viambishi vinavyopachikwa baada ya kiini/mzizi wa kitenzi.Kwa mfano kitenzi anacheza, kiambishi tamati ni a- inayotokea baada ya z-
Dhima za Viambishi
  1. Viambishi awali:Hivi huonyesha nafsi, idadi na wakati.Mfano katika neno anaimba, a- inawakilisha nafsi, nafsi hiyo ni ya tatu.Vilevile, inaonyesha idadi, umoja, na inaonyesha wakati uliopo hali ya kuendelea.Vilevile , viambishi awali huonyesha uyakinishi au ukanushi .Kwa mfano , katika neno anaruka, a- huonyesha uyakinishi lakini katika hali ya ukanushi kitendo hicho kingebadilika na kuwa hataruka na kiambishi awali chake kingekuwa ha-.
  2. Viambishi tamati: Hivi hukamilisha maana ya neno. Kwa mfano kitenzi anakula kama kisingekuwa na kiambishi tamati -a, je neno anakul- lingeleta maana yoyote? Vilevile viambishi tamati huzalisha maneno mapya mfano wanacheza, wanachezeana.
MOFIMU
Fasili ya mofimu ni: Mofimu ni neno au sehemu ya neno yenye maana kisarufi, ambayo haiwezi kugawanyika zaidi bila kupoteza maana. Kwa mfano:
maneno
(a) babu, hewa
mofimu
kila neno lina Mofimu moja
AINA ZA MOFIMU
  1. Mofimu huru
  2. Mofimu tegemezi
MOFIMU HURU
Haya ni maneno kamili ambayo huwezi kugawa zaidi bila kupoteza maana.
Mfano:Baridi, kofia, hewa, kaka, mama, sana, maji. Maneno haya hayawezi kugawanyika zaidi na yakaendelea kuwa na maana hiyohiyo kisarufi.
MOFIMU TEGEMEZI
Ni vipande vidogovidogo vya maneno vyenye maana kisarufi. Mofimu hii maneno yamejengwa kwa kubandika vipashio kadhaa vya kisarufi ambavyo huweza kubadilishwa na maana ya neno ikabadilika.
Mfano: neno anapika lina mfano tegemezi ufuatazo
a-na--pik--a
12kiini3
Mofimu zinazobadilika kwenye kiini cha neno huitwa Viambishi.
Katika lugha ya Kiswahili viambishi hutokea kabla na baada ya kiini cha neno.
Mfano
Wanapendana = Wa-na-pendan-a kiini cha neno ni-pend-.
Mofimu zilizobadilisha baada ya kiini –an-na-a viambishi vinavyotokea kabla ya kiini cha neno huitwa viambisha awali au tangulizi. Viambisha vinavyotokea baada ya kiini cha neno huitwa viambishi tamati au fuatishi.
Example 1
Angalia mifano ifuatayo:
NenoViambisha AwaliKiiniViambisha Tamati
Unapendeleau-na--penda-el-e-a
Waliongozanawa-li--ongoz-an-a
Analimaa-na--lim--a
anayeiimbishaa-na-ye-imb--ish-a
Dhima za Mofimu
Bainisha dhima za mofimu
Baadhi ya dhima za uambishaji ni kama ifuatavyo:
  1. Kuonyesha upatanisho wa usanifu maana ya maneno yanayozalishwa kutofautiana katika msingi wa kusanifu tu, lakini uhusiano wa maneno hayo hutokana na kiini au mzizi wake uleule.Mfano;Fundisha kiini chake ni fund. Unaweza kuzalisha maneno mengine kwa kutumia mzizi/kiini kilichopo kama vile fundishana, mafundisho, mfundishaji, fundishwa, fundishana.
  2. Uambishaji huonyesha nafsi
  3. Uambashaji huonyesha njeo (muda)
  4. Uambishaji huonyesha urejeshi
  5. Uambishaji huonyesha ukanushi
  6. Uambishaji huonyesha hali mbalimbali za kitenzi
Vitenzi vikiambishwa huweza kujenga/kuunda/kuzalisha vitenzi vingine au nomino.
Example 2
Mfano
VitenziKiiniNominoVitenzi
Cheza-chez- Mchezaji, mchezo wanacheza/atamchezea
Piga -pig- Mpigaji, Mpiganajiwatanipiga, aliyempiga/wanaompiga
Uambishaji hutumika kuzalisha viwakilishi na vielezi.
Neno (Kiwakilishi)KiiniKielezi
Huyu, HuyoHuHumu, humo
Wangu, wako, wakewa
Hii, hizo, hikihi
Viambishi awali vina dhima ya kudokeza nafsi, njia, idadi urejeshi na ukanushi.Mfano: Hawakulima
  • Ha-, kiambishi cha ukanushi
  • Ku-, kiambishi njeo/wakati
Viambishi tamati vina dhima mbalimbali hudokeza hali ya utendekaji, ukamilishaji au kimalizio cha neno na kauli za matendo kama vile kutendwa, kutendewa,kutendeka nk.
Dhima:Ukanusho, kutendeana, agizo na mtendwa, ukamilisho, usababishi.
Example 3
Mfano
NenoViambishi Tamati
Anapiga-a
Wanapigana-an
Asipigwe-w
Amempigisha-ish-
Viambishi tamati vina dhima ya kutambulishwa mapema/nomino zilizoundwa kutokana na vitenzi.
NenoKiiniViambishi Tamati
Pigapig--o
Mchezochez--o
Mtembezitembe--z-i
Mfiwa-fi--us-a
Kutumia Mnyumbuliko
Mazingira yanayosababisha Mahitaji ya Maneno Mapya
Elezea mazingira yanayosababisha mahitaji ya maneno mapya
Mnyumbulisho ni neno linalotokana na neno nyumbua. Kunyumbua kitu ni kuvuta, kuongeza urefu wa kitu hicho.
Kunyumbua katika lugha ya Kiswahili ni kuongeza vinyumbulishi katika katika kiini ili kupata msamiati mpya. Hivyo basi, mnyumbulisho ni njia mojawapo na inasaidia kuunda maneno kwa njia ya kunyumbulisha.
Viambishi vinapochukuliwa katika kiini cha neno, basi neno hilo huwa limenyumbulishwa. Kwa mfano neno lima kiini chake lim- huweza kunyumbulishwa na kupata maneno mengine mpya, kama lim-ishwa, lim-ia, lim-w-a.
Pia maneno ya mnyumbulisho yanaweza kuundwa kwa kuongeza viambishi kwenye shina, kwa mfano:
NenoKiiniShinaManeno ya Mnyumbuliko
ElekeaelekelekaElekeana, elekea, elekwa, elekesha
ShikishanashikshikishaShikishana, shikisha, shikishaneni
Kwa ujumla tunawaza kusema kuwa maneno ya kawaida hunyumbulika. Hivyo kiini/mzizi au shina moja huweza kuzalisha maneno mengine mengi ambayo yanatokana na msingi mmoja wa maana.
Dhima ya Uambishaji na Mnyambulikoa wa Maneno
Fafanua dhima ya uambishaji na mnyambulikoa wa maneno
Dhima ya uambishaji ni kuleta upatanisho wa kisarufi, kuonesha idadi na umoja na wingi katika ngeli za majina, kuonesha njeo na kuonesha urejeshi pamoja na hali mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi kabla ya mzizi wa neno. Aidha dhima ya mnyambuliko ni kuonesha matokeo ya tendo na kuzalisha kauli mbalimbali kwa kupachika viambishi baada ya mzizi wa neno.
Kuunda Maneno mbalimbali kwa kutumia Mnyambuliko
Unda maneno mbalimbali kwa kutumia mnyambuliko
Uundaji wa maneno mbalimbali kwa kutumia mnyambuliko hufanyika kwa kupachika viambishi baada ya mzizi wa neno na hivyo kulifanya neno husika liweze kuonesha matokeo mbalimbali ya matendo pamoja na kuzalisha kauli mbalimbali za matendo.
Activity 1
Unda maneno mbalimbali kwa kutumia mnyambuliko
Kutumia Maneno ya Mnyambuliko katika Miktadha mablimbali
Tumia maneno ya mnyambuliko katika miktadha mablimbali
Maneno ya mnyambuliko hutumika katika miktadha mbalimbali ambapo miktadha hiyo hujitokeza katika kauli mbalimbali za vitenzi. Kauli hizo ni kauli ya kutenda, kauli ya kutendwa, kauli ya kutendewa, kauli ya kutendea, kauli ya kutendeka, kauli ya kutendesha, kauli ya kutendana, na kauli ya kutendama.
Activity 2
Tumia maneno ya mnyambuliko katika miktadha mablimbal
Listening to this topic